Makanali wa gaddafi watorokea malta

Walinzi wake Gaddafi ni wanawake, na hao makanali ni wanawake pia au mchanganyiko?

Na wewe sasa unachanganya Mambo! Siyo kwamba jeshi lote la Libya ni wanawake! Hao unaozungumza wewe ni walinzi wa Ghaddafi na siyo wanajeshi tu wa kawaida. Hivyo utaona kwamba hao waliotoroka ni wanajeshi wa kawaida na siyo walinzi wa Rais.
 
Makanali kadhaa wa Kiongozi wa Libya aliye kwenye waya mkali hivi sasa,Kanali Muhammar Gaddafi wametua bila ruhusa na ndege zao za kivita katika kisiwa cha Bahari ya Medditerrania,Malta.Walipokamatwa na kuhojiwa,Makanali hao wamedai kuwa wametorokea huko baada ya kukataa kutii amri ya kushambulia kwa mabomu umati wa waandamanaji katika mji wa Benghazi,yalipoanzia maandamano ya kumng'oa madarakani Gaddafi.Baada ya kukataa amri hiyo ya kijeshi,makanali hao walisafiri takribani umbali wa saa moja na kutua kwa dharura Malta.Bado wanashikiliwa na maofisa wa Malta kwa uchunguzi na taarifa zaidi.Je,hawa ni mashujaa au wasaliti?
Hawa ni mashujaa wa mapinduzi, wameandika historia kwenye nchi yao wamegoma kuua raia wasio na hatia!!!!!!!!!Sio rahisi kugomea amri, hiyo inaitwa amri halali ukigoma unalamba chuma baba huko ni jeshini si umangani!!!!!!!! Kudo's Gadafi Col's!!
 
Asili ya mtu mkamilifu ni kwamba humuasi kila mtu isipokuwa Mungu.
Hawa wanajeshi ni kwamba wao sio maroboti kutii kila amri hata kama inakiuka misingi ya kiutu.
Alaah! Na wao wana utashi wa kuweza kutambua jema na ovu.
Ndio maana kwa utashi wao wamemwasi shetani kwa kumtii Mungu.
Kifupi hawa ni mashujaa watakaoingizwa kwenye historia hii ya kuikomboa Libya ya dictator Gadafi.
.
 
PHP:
Makanali kadhaa wa Kiongozi wa Libya aliye kwenye waya mkali hivi sasa,Kanali Muhammar Gaddafi wametua bila ruhusa na ndege zao za kivita katika kisiwa cha Bahari ya Medditerrania,Malta.Walipokamatwa na kuhojiwa,Makanali hao wamedai kuwa wametorokea huko baada ya kukataa kutii amri ya kushambulia kwa mabomu umati wa waandamanaji katika mji wa Benghazi,yalipoanzia maandamano ya kumng'oa madarakani Gaddafi.Baada ya kukataa amri hiyo ya kijeshi,makanali hao walisafiri takribani umbali wa saa moja na kutua kwa dharura Malta.Bado wanashikiliwa na maofisa wa Malta kwa uchunguzi na taarifa zaidi.Je,hawa ni mashujaa au wasaliti?

May the Lord bless them............................
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom