Makanali wa gaddafi watorokea malta

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Makanali kadhaa wa Kiongozi wa Libya aliye kwenye waya mkali hivi sasa,Kanali Muhammar Gaddafi wametua bila ruhusa na ndege zao za kivita katika kisiwa cha Bahari ya Medditerrania,Malta.Walipokamatwa na kuhojiwa,Makanali hao wamedai kuwa wametorokea huko baada ya kukataa kutii amri ya kushambulia kwa mabomu umati wa waandamanaji katika mji wa Benghazi,yalipoanzia maandamano ya kumng'oa madarakani Gaddafi.Baada ya kukataa amri hiyo ya kijeshi,makanali hao walisafiri takribani umbali wa saa moja na kutua kwa dharura Malta.Bado wanashikiliwa na maofisa wa Malta kwa uchunguzi na taarifa zaidi.Je,hawa ni mashujaa au wasaliti?
 
Gadaffi alipitiwa na ile methali yetu isemayo Ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji.. Aliangalia walipo angukia wenzake hakuangalia walipo jikwaa... Step by step tutafika wandugu.
 
Hao ni mashujaa,sababu bado kuna wanaomtii Gadafi wanaweza wakauawa.sidhani polisi wetu na wanajeshi kama wanaweza kuungana na wananchi kupinga ukandamizaji.utadhani ukali wamaisha hauwahusu.ngoja tusubiri.
 
ni suala tete sana libya,unapoona kiongozi anaagiza watu wapigwe na mabomu kwa ndege za kivita?:A S 13:
na anayetoa amri izo ni mtoto wake!ivi ni nani katika jeshi lao?
 
ni suala tete sana libya,unapoona kiongozi anaagiza watu wapigwe na mabomu kwa ndege za kivita?:A S 13:
na anayetoa amri izo ni mtoto wake!ivi ni nani katika jeshi lao?
we subiri Riz1 atakuja toa amri siku haswa haya maandamano yakina CHADEMA tutamuona kwenye taarifa maalum akiamrisha Shimbo afanye mambo!
 
Ni mara mbili, ni wasaliti wa Gaddafi but ni mashujaa wa wananchi na wapiganaji wa kweli!
 
Hao sio wasaliti wala nini na wana ujasiri sana, kuwapiga raia kwa mabomu kisa wanaandama huo ni uuaji uliopitiliza......
 
Hawa ni mashujaa lakini ni waoga. Walitakiwa watoke kwenye makambi yao na kwenda kuungana na wananchi kwenye maandamano na sio kukimbia nchi.
 
makanali kadhaa wa kiongozi wa libya aliye kwenye waya mkali hivi sasa,kanali muhammar gaddafi wametua bila ruhusa na ndege zao za kivita katika kisiwa cha bahari ya medditerrania,malta.walipokamatwa na kuhojiwa,makanali hao wamedai kuwa wametorokea huko baada ya kukataa kutii amri ya kushambulia kwa mabomu umati wa waandamanaji katika mji wa benghazi,yalipoanzia maandamano ya kumng'oa madarakani gaddafi.baada ya kukataa amri hiyo ya kijeshi,makanali hao walisafiri takribani umbali wa saa moja na kutua kwa dharura malta.bado wanashikiliwa na maofisa wa malta kwa uchunguzi na taarifa zaidi.je,hawa ni mashujaa au wasaliti?

hawa ni mashuuja wakweli..... Miaka 40 utatii amri gani yakuuwa raia wema?
 
Hao ni mashujaa,sababu bado kuna wanaomtii Gadafi wanaweza wakauawa.sidhani polisi wetu na wanajeshi kama wanaweza kuungana na wananchi kupinga ukandamizaji.utadhani ukali wamaisha hauwahusu.ngoja tusubiri.

dawa ni kuwanyima lift!!
 
Walinzi wake Gaddafi ni wanawake, na hao makanali ni wanawake pia au mchanganyiko?
 
wala sio kwamba alipitiwa, alikuwa anajua kila kitu..ila ni kiburi tu na kuona kwamba yeye ni yeyee si unajua tena, baaada ya kutoka wa Tunisia akamponda sana na kusema amekosea sana kuachia madaraka..hivyo alijua kabisa kwake hayawezi kutokea...lol
Gadaffi alipitiwa na ile methali yetu isemayo Ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji.. Aliangalia walipo angukia wenzake hakuangalia walipo jikwaa... Step by step tutafika wandugu.
 
Ningewahesabu kama mashujaa wa kweli kama wangeyadondosha ikulu hayo mabomu!
eti..eh hilo nalo ni neno zuri
ngoja tuwasiliane nao ili tuwarudishe wakammalize jamaa.
Ndugu yangu mambo sio marahisi kiasi hicho kwani pale Ikulu panalindwa mda wote, na wao ili kujihami na maisha yao pia wakaona ni bora waende huko Malta
 
Hawa ni mashujaa lakini ni waoga. Walitakiwa watoke kwenye makambi yao na kwenda kuungana na wananchi kwenye maandamano na sio kukimbia nchi.
wapo waliowaunga wananchi pia ni wengi mno, kwani uanaambia wanjeshi wa Benghazi wote walisalimisha silaha na kujiunga na wananchi ndio maana huo mji wote uko chini ya Upinzani mpaka sasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom