Makamu wa raisi yupo wapi?

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Makamu wa raisi wa JMT Dk nani sijui yule (nimemsahau jina), yule mzee wa kizanzibar, yuko wapi? mzima wa afya? Mi nilidhani kwa kusafiri raisi yeye ndiye angeachiwa mikoba, lakini naona Pinda ndiye yuko responsible na kila kitu. Ameenda wapi huyu mzee?
 
Wakati wa uchaguzi nilisema yule ni pazia tu hana kitu kichwani upepo ukija linafunuka

siasa za zanzibar ni tofauti na siasa za bara hakuwa na uwezo wa kuwa hata katibu kata huku bara sembuse Vice president

ila aliwekwa pale kwa siasa za majungu ya zanzibar kwa manufaa yao binafsi na si ya bara.
 
Yuko atakuwa anawatembeza wale wake zake wawili kwa magari ya serikali hana lolote ni makamu picha tu
 
Duh kweli aisee hata mm nilishasahau kama hii nchi ina makamu. Huu ndo ulikuwa wakati wake wa kushine...! Alivalie njuga suala la katibu mkuu wa Nishati na kuwawajibisha wote wanaohisika. Sioni sababu ya kumsubiri Raisi aliyeenda kula raha south na huku nyumba yake yawaka moto.
 
Makamu wa raisi wa JMT Dk nani sijui yule (nimemsahau jina), yule mzee wa kizanzibar, yuko wapi? mzima wa afya? Mi nilidhani kwa kusafiri raisi yeye ndiye angeachiwa mikoba, lakini naona Pinda ndiye yuko responsible na kila kitu. Ameenda wapi huyu mzee?

Yuko harusini ikulu bagamoyo na wakezake, akitoka huo ana rudi serengeti kupumzika lol!
 
Hivi anaitwa Dokta nani tena.... aaah jina lake gumu sanaaaa... aaah... J.K. aliwahi kumuita Shababi... hivi kazi yake ni nini hasa???
 
Alaaaaaaaaaaaaaaaah! hivi hii nchi kumbe tuna makamu wa raisi! Naomba mnitumie picha yake hapa jf angalau niweze kumtambua.
 
Kwani nchi kaachiwa nani jamani, huenda hakuachiwa yeye.

kauli ya mtoto wa mkulima pia inashangaza , inamaana yeye hawezi kuchukua hatua mpaka Rais aje au mtoto wa mkulima yeye ni kutetea pesho za wabunge tu
 
Huyu jamaa kwa sasa unaambiwa kazi yake ni kukata utepe, kufungua miradi mbalimbali ANATEMBEA NA MKASI MFUKONI
 
Huyu nae ni mzigo tu, anashindwa hata kujua nafasi zake, yaani hapa ndio angechomoza kucha maana Rais wakati hayupo nadhani yeye anakuwa steringi sasa si angeaanza na Jairo then Ngereja na Malima , Vasco Kikwete akirudi anakuta taarifa mezani!!!!!! lakini kama kweli ni muelewa na makamu wa rais wa ukweli
 
yupo anachunguza sehemu za kuchimba urenium maana si ni mtaalamu wa nyukilia pekee alayebaki baada ya tanzania kuogopa kumtumia kwa kuwaogopa wamarekani, sasa naona wameruhusu sijui naona harakari pale kwenye hifadhi, naogopa isije lipuka kama mbagara na ukonga, sijui nyie mwasemaje, mtaarumu mnamkimbizia kwenye siasa nchi itaendelea kweli? huyu mtaalam wa nyukilia leo hii yuko kwenye masherehe anatembea na mkasi kukata utepe!!!!
 
Huyu mwamba yupo kweli kitambo sana sijamsikia
 
Back
Top Bottom