Dr. Shein alikuwa Makamu wa Rais wa Mkapa ambaye wakati wa utawala wake ufisadi ulijengwa na kuimarishwa kikamilifu. Sasa ni Makamu wa Rais wa Kikwete anayeendeleza ufisadi huo uliojengwa na Mkapa akisaidiwa na Shein. Hadi leo sijamsikia akikemea ufisadi kwa nguvu zake zote. Shein siyo mwanasiasa bali ni mtu aliyechukuliwa kutokana na uzezeta (upole?) wake ili aendelee kutekeleza majukumu ya Bosi wake bila kuhoji kinachoendelea. Yeye ni aina ya "NDIYO BWANA"! Hafai kuwa Rais ajaye. Labda awe Rais wa Wapemba.