Makamu wa rais dk Bilal ahudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Uganda

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Rais Yoweri Museveni wa Uganda akimkaribisha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye sherehe za maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala,Uganda.
DSC_0161-1024x685.jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gaharib Bilal (kulia) akibadilishana mawazo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 yaUhuru wa Uganda. Sherehe hizo zimefanyika jana katika Uwanja wa Kololo jijini Kampala. Wanaoonekana nyuma yao ni wake zao, Bibi Janneth Museveni (kulia) na Mama Zakia Bilal.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda kwenye Uwanja wa Kololo, jijini Kampala jana. Wengine kutoka kushoto ni Rais wa Somalia Hassan Shekhe Mahamoud na Makamu Rais wa Sudan, Bwana Haji Adam Yusufu.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 
Yaani mzee meno yametangulia utadhani fuko! Heri yake anajifurahisha kwa kutafuna kodi zetu kwa majirani huku watoto wetu wakiketia tofali shuleni bila kitabu wala mwalimu. Jamaa ni dhaifu kama DHAIFU tu hakuna tofauti!
 
Back
Top Bottom