Makamu wa Rais ana kazi gani?

Makamu wa Rais ni muhimu kwa kua Rais anaposhindwa kuongoza kwa sababu zilizoainishwa katika katiba,makamu huchukua madaraka katika kipindi cha mpito.Na hii ipo nchi nyingi tu.Hata marekani yupo Joe Biden,alikua Dick Chenney na wote ni wazee wa mikasi.Ni vema makamu wa Rais akawa sio mtu mwenye uchu wa madaraka ili kupunguza msuguano kama ilivyokua kwa Obasanjo na Atiku Abubakar mpaka walikaribia kukunjana mashati
Tutajie na waziri mkuu wa Marekani. Issue hapa ilikuwa kuangalia kama kuna ulazima wa kuwa na makamu wa rais na waziri mkuu. Hapo nyuma waziri mkuu alikuwa pia makamu wa rais. Kwanini tusirudie utaratibu huo kuepuka gharama zisizo za lazima? Tusiige mambo nusunusu kwani hata huko Marekani unakotaja hawana waziri mkuu.
 
mkuu, bajeti ya mzee wa mikasi mfukoni ni takriban sh bilion tisa. bajeti kwa ajili ya mikasi na tepe. tehe.

Wakati shule hazina vitabu, madawati n.k, hospitali hazina madawa, vitendea kazi n.k, ni upuuzi mkubwa!
 
Mmmmh! Huku tunakoelekea itafikia hatua watu watasema cheo cha umama kifutwe ndani ya nyumba, baba na housegirl wanatosha. Mana mmmh, watu wameamka mno.
 
kuhusu makamu wa rais. Watanzania wenzangu kuna umhimu wa kuangalia swala ili kwa umakini zaidi kuhusu makamu wa rais. hamna umhimu wa kuwa na makamu wa rais mfano mzuri tu waziri mkuu Pinda katika sakata la Jairo kuhusu kuchangisha ela ili kuonga kupitisha bajeti ya nishati, PINDA alishema angelikuwa mimi ningesema basi, lakini tusubili Rais harudu. Ktk somo la civics tunaambiwa hivi kama rais atakuwa nje ya nchi makamu anakaimu nafasi ya rais, lakini ilo limeonekana kuwa na kiini macho kwa watanzania k:flypig:ama kweli anakaimu nafasi ya rais ilikuwa kuwaje! Kutotoa kauli kama rais wa nchi? Pia tuangalie wazili alipoongelea kuwa tumsubiri rais mbona hamna tamko lolote kutoka serikalini la kumhoji waziri kumzalilisha makamu wa rais kwa nafasi yake? Ili nidhaili kwamba makamu wa rais yupo tu kama geresha kula nchi na kuujumu kodi za wananchi, maana hii ela anayolipwa engeingizwa ktk uboleshaji wa afya. Maana hii ni ela nyingi ingawa sijui ana lipwa shilling ngapi kwa mwezi, lakini ni dhaili kuwa ni ela nyingi kwanza ukizingatia ela wanayolipwa mawaziri, yeye yuko juu yao. Lakin. kuna swala la katiba mpya ili tuliangalie kwa undani zaidi. Pia kuhusu wakuu wa mikoa na wilaya. Hamna aja yoyote ya kuwa na viongozi awa, maana wakurugenzi ndio wanaofanya kazi katika wilaya na mikoa walio baki ni kula kodi za wananchi tu. Watanzania tuwe tayali kukataa watu awa katika katiba mpya. Angalia mikoa na wilaya tulizonazo katika nchi yetu. Hii ela wanayolipwa ingesaidia ktk uboleshaji wa uduma za jamii.
Pamoja na ayo kuna aja serikali kuliangalia swali ili kwa macho mawili kwa umakini zaidi kwa masilai ya taifa letu.
 
Tutajie na waziri mkuu wa Marekani. Issue hapa ilikuwa kuangalia kama kuna ulazima wa kuwa na makamu wa rais na waziri mkuu. Hapo nyuma waziri mkuu alikuwa pia makamu wa rais. Kwanini tusirudie utaratibu huo kuepuka gharama zisizo za lazima? Tusiige mambo nusunusu kwani hata huko Marekani unakotaja hawana waziri mkuu.
Wakati wa mfumo wa chama kimoja hili liliwezekana kua na makamu wa rais ambae ni waziri mkuu.Ilibadilishwa ulipokuja mfumo wa vyama vingi na kufanya mgombea urais lazima awe na running mate kutoka upande mwingine wa muungano.Kwa maoni yangu...kwa kua bado tuna rais mtendaji ni bora kua na makamu wa rais.kumbuka kenya walikua hawana waziri mkuu,makamu wa rais ndie alikua kiongozi wa serikali bungeni,lakini walijikuta wanachemsha rais anaposafiri wakati huo huo kuna vikao vya bunge
 
Asalaam,
Katika mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya uliomalizika kwa awamu ya kwanza, nimebahatika kuhudhuria mikutano miwili katika wilaya ya Bagamoyo na mmoja katika wilaya ya Bukoba. Nilitoa maoni yangu katika mikutano miwili kati ya hiyo mitatu.
Kitu nilichotilia mkazo ni hiki cheo cha "MAKAMU WA RAIS". Kwa kweli binafsi sioni sababu za msingi za kuwa na Rais, makamu wake, na waziri mkuu kwa wakati mmoja. Nimegundua ni uharibifu wa mapato kuwa na taasisi nyingine yenye wizara mbili, huku mkuu wa taasisi hiyo akiishia kusoma magazeti, kualikwa kwenye warsha, na kukata utepe. Pia Makamu wa Rais wa sasa ameishia kuvikwa mataji ya maua na kutoa hutuba kama mhitimu wa shule.
Ndugu zangu watanzania, nawaomba mkipata nafasi katika awamu inayofuata ya utoaji maoni, mlizungumzie jambo hili, kwakua, Rais ni Mkuu wa nchi na Mkuu wa serikari na pia ni Amri Jeshi Mkuu., Waziri Mkuu ni mtendaji mkuu wa shughuli za serikali na msimamizi wa serikali bungeni. JE?
Makamu wa rais anaumuhimu gani?
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.

Ni kweli kabisa nchi nyingi sana makamu wa rais huwa hana umuhimu mpaka yatokee kama yale ya Malawi, Ghana et al. You can not underestimate the importance of a VP
 
makamu wa raisi ni cheo cha ki protocol tu na lengo lake ni awe kiongozi wa kisiasa sio mtendaji

ukiangalia practically hata waziri mkuu ni mkubwa kuliko makamu wa rais
 
Rais,na waziri Mkuu wanatosha.Either uwe na makamu wa Rais usiwe na waziri mkuu au Uwe na waziri mkuu usiwe na makamo wa Rais.Tunakua na watumishi wengi sana ili hali tuu maskini



Mi naona hata tusingekuwa na rais ingekuwa poa tu!
Angetosha waziri mkuu tu!
 
Ungejenga hoja yako kivingine lakini sio " ... hana umuhimu ...". Utaona umuhimu wake pale Rais "atakaposhindwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na ugonjwa au mapenzi ya Mwenyezi Mungu"; yaani, hapo nchi itakapokosa kamanda mkuu - tutageuka Somalia mara moja.
Hoja yangu hapa sio Makamu wa Rais, bali tupe mbadala mwingine wa nani achukue majukumu ya Rais endapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Tunayo mifano ya hivi karibuni kabisa kule Malawi na Ghana tumeona Makamu wa Rais wakichukua madaraka baada ya marais wao kufariki.

Aaaha mkuu mbona jibu ni simple, kwani si atakuwa waziri mkuu ndo mwenye dhamana na ndiye ataongoza nchi.
 
Bora ata makamu wa rais mbele ya huyu rais wa Zanzibar yeye kazi yake ni kuzindua maskani na matawi mapya ya CCM hana lingine analofanya
 
Cheo hiki pia kimekuwa na utata/kudharaulika hata USA ambako Senator mmoja amekitaja as "not worth a bucket of warm spit". Nadhani ni cheo cha kuzawadi washikaji au wakorofi ili kuwa nyamazisha. hnn.us/articles/53402.html
 
Asalaam,
Katika mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya uliomalizika kwa awamu ya kwanza, nimebahatika kuhudhuria mikutano miwili katika wilaya ya Bagamoyo na mmoja katika wilaya ya Bukoba. Nilitoa maoni yangu katika mikutano miwili kati ya hiyo mitatu.
Kitu nilichotilia mkazo ni hiki cheo cha "MAKAMU WA RAIS". Kwa kweli binafsi sioni sababu za msingi za kuwa na Rais, makamu wake, na waziri mkuu kwa wakati mmoja. Nimegundua ni uharibifu wa mapato kuwa na taasisi nyingine yenye wizara mbili, huku mkuu wa taasisi hiyo akiishia kusoma magazeti, kualikwa kwenye warsha, na kukata utepe. Pia Makamu wa Rais wa sasa ameishia kuvikwa mataji ya maua na kutoa hutuba kama mhitimu wa shule.
Ndugu zangu watanzania, nawaomba mkipata nafasi katika awamu inayofuata ya utoaji maoni, mlizungumzie jambo hili, kwakua, Rais ni Mkuu wa nchi na Mkuu wa serikari na pia ni Amri Jeshi Mkuu., Waziri Mkuu ni mtendaji mkuu wa shughuli za serikali na msimamizi wa serikali bungeni. JE?
Makamu wa rais anaumuhimu gani?
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.

umeongea kweli napia nami ningependa tuirejeshe serikali yetu ya tanganyika ili kuipunguzia mzigo wa kubebesha ndani ya serikali ya muungao na suali hili kwanini wengi wetu hawalizungumzii ama hatupendi irejeshwe?huu ndo muda
 
Makamo wa Rais yupo pale ili kuziba ombwe la uongozi pindi likitokea. Kumbuka Malawi na Ghana. Malawi ingekuwa kimbembe kama wasingekuwa na Makamo wa Rais.
 
Nimeelewa sababu kubwa ya uwepo wa Makamu wa Rais yaani kusubiri tu kuchukua madaraka ya Rais wakati Rais anapokuwa hawezi (au ameshindwa!) kutekeleza madaraka yake LAKINI KWA GHARAMA HII. Inabidi tutafakari upya, tusiwe wajinga kiasi hiki.
 
Nimeelewa sababu kubwa ya uwepo wa Makamu wa Rais yaani kusubiri tu kuchukua madaraka ya Rais wakati Rais anapokuwa hawezi (au ameshindwa!) kutekeleza madaraka yake LAKINI KWA GHARAMA HII. Inabidi tutafakari upya, tusiwe wajinga kiasi hiki.

Mkuu Makucha nadhani utaratibu wa zamani wa kuwa na Makamo wa Rais ambaye pia ndiye waziri mkuu ulikuwa mzuri. Makamo wa Rais alikuwa akionekana anafanya kazi za utendaji kuliko kazi za sasa ambazo ni too ceremonial. Kwa sasa tunatapanya mali manake makamo ana security detail yake na marupurupu meeeeengi na huku PM naye ana detail na marupurupu meeeeengi inakuwa ni mzigo kwa walipa kodi. Mtu mmoja anaweza kumsaidia Rais na ikizingatiwa kunakuwa na mawaziri kibao wa nchi kwenye ofisi za PM na VP.
 
Last edited by a moderator:
Bado msimamo wangu uko palepale. Sioni sababu ya kuwa na mgombea mwenza ili aje kuwa makamu wa Rais.
Hili jambo la urithi pindi Rais anapokufa, au pindi rais anaposhindwa kazi kwa sababu ya ugonjwa linaweza kujadiliwa kwenye katiba na kulitafutia mbadala.
Makamu wa rais hana makucha, hawezi kutoa agizo lolote, hawezi kuhutubia nchi, na kibaya zaidi anatumia mali za umma kwa pasipo na manufaa kwa nchi.
Tuchague moja, kuwa na makamu wa rais au waziri mkuu, lakini sio wote kwa pamoja.
 
Mkuu Kimbunga nakubaliana na mapendekezo yako ya kuwa na Makamo wa Rais ambaye pia ndiye Waziri Mkuu au wazo lingine lile zuri zaidi lengo kuu ni kuepuka gharama kubwa hizi zisizo za lazima kuanzia mshahara, marupurupu, gharama za ofisi yake na malipo kibao baada ya kustaafu. Sababu hana kazi mbali na 'ceremonial duites'. Mawazo yangu ni haya:
  1. Kama nafasi ya Makamu wa Rais ni kutokanan na hisia za muungano, mapendekezo yangu ni Tanganyika na Zanzibar kuwa nchi moja ambayo ninaamini ndiyo hatima ya muungano wa ukweli na dhati.
  2. Kama kuwa nchi moja haiwezekani, basi lengo la muungano limefeli na muungano utafeli kwa sababu ya viongozi wa juu na si kwa sababu ya wananchi wengi kati ya bara na visiwani. Muungano ukivunjika, naamini bado tutabaki katika 'strong deplomatic relationship'. Zaidi watakaoumia ni viongozi kuliko wananchi wa kawaida.
  3. Kama ni bara kuhofia usalama Zanzibar wakijitenga, hilo si tishio tena kwani sasa tunaelekea katika Shirikisho la Afrika ya Mashariki na kwa busara yote Zanzibar pia wataingia humo. Vinginevyo wakijitenga nje ya Afrika ya Mashariki, tishio la usalama kutoka pale ni tishio kwa Shirikisho la Afrika ya Mashariki. kazi ipo, wewe unasemaje?
  4. Kwa sasa hakuna upande unaokiri wazi wazi kufaidika na huu muungano hasa kiuchumi. Hitimisho; it is high time we called a 'stone' a 'stone'.
 
kazi yake kubwa ni kutembea na mkasi kukata utepe na kuzindua vizima.........................
 
Back
Top Bottom