Makamu wa Rais ana kazi gani?

(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.

Sijawahi ona au sikia huyu mtu akifanya kazi zozote za raisi wakati raisi hayupo. Nitoe mifano.
1. Ishu ya Jairo inaibuka raisi alikua nje ya nchi. Sikumsikia makamu wa rais.
2. Mgomo wa madaktari unatokea rais hayupo. Sikumsikia rais.

Sasa nitolee mfano wa lini kafanya kazi za raisi wakati raisi yupo nje ya nchi. Huwa namsikiaga tu waziri mkuu.
 
Kwa kweli hata mimi sielewi umuhimu wa kuwa na Makamu wa Rais. Katiba ya sasa inasema kwamba Makamu wa Rais ni Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla. Hususan (a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano; (b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais; na (c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.

Kwa Makamu huyu wa Rais ni mambo yapi ya muungano ambayo amemsaidia Rais kufuatilia utekelezaji? Ina maana hizi kazi anazofanya za kuzindua na kuwa mgeni rasmi anakuwa ametumwa na Rais? Halafu kuna hili la kufanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Sasa juzi tuu Rais alikuwa nje ya nchi na kulikuwa na mgomo wa madaktari. Je, Makamu wa Rais alifanya nini la maana kujaribu kushughulikia? Mimi nilmwona tuu alipoenda kumpokea Rais uwanja wa ndege wakati akirejea nchini. Inaonyesha labda hata madaktari walimdharau pale walipoamua kukutana na Waziri Mkuu.

Inavyoonekana ni kwamba Makamu wa Rais huwa anatekeleza madaraka yake chini ya uongozi na usimamizi wa Rais na anaongoza na kuwajibika kwa Rais kuhusu mambo au shughuli zozote anazokabidhiwa na Rais. Kwa hiyo hapa itategemeana na Rais amempa kazi gani. Kama hajampa kazi, hana cha kufanya. Na kwa vile labda hakuna kazi za kumpa, ndiyo maana labda huwa anaishia kuzindua tuu vitu, kukata utepe, kuweka jiwe la msingi na kuwa mgeni rasmi kwenye mambo ambayo yangefanywa hata na mkuu wa wilaya?

Mimi ninacho jiuliza ni je raisi haamini uwezo wa makamu wake au hauthamini? Maana katiba inasema raisi atampangia kazi makamu wake. Sasa ni kazi zipi JK kampangia Bilal? Pia inasema raisi akiwa nje ya nchi makamu ndiyo raisi. Juzi migomo inatokea raisi hayupo lakini sikumsikia makamu wa raisi.
 
Mwenye note book na aandike maneno haya, haitakuja kamwe Mzanzibar kuwa Rais wa Tanzania mpaka mwisho wa muungano huu, kwahiyo hiyo nafasi hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwapa ulaji wa Muungano Wazanzibar, hivi hamjiulizi kwani hata yule Seif Sharrif Hamad ana kazi gani kwenye serikali ya Zanzibar?
 
Jamani mbona mnamsakama au kukisakama na kuusakama wadhifa huo?

Wengine badala kuiattack Katiba,wanamuattack as a person!! Aah..si vema jamani..

Kwani hii si tumeicope US.. Mambo ya Running Mate?? Hata kama ilitumika kisiasa lakini,jamani,kwani Joe Bidden anasikika mara kwa mara kwenye US politics?

Mara ngapi Obama amelazimika kuiacha familia yake kwenye vacation na kuja kuattend matters tofautitofauti?
 
Jamani naomba mnijuze , hivi kutembea na wake zake tanzania yoooote vijijini hadi wilaya ndio kazi ya huyu mhe mohamedi gharib bilali........? hana ofisi........?
 
na yeye anataka kuwa rais wa JMT watu wengi hawamjui sasa afanyaje kama si kwenda kwao kujitambulisha, ofisi anayo lakini cha kufanya ndiyo hamna.
 
Wana jf kila uchao ninachokiona anakifanya makamu wa rais ni kufungua shule,kuhudhuria mahafali, na mengine kama hayo.Hivi hiki cheo kina umuhimu gani hasa kwa nchi kama Tz ikizingatiwa tunaye waziri mkuu!?
 
Akifariki Rais yeye ndiyo anakuwa Rais, labda hilo ndiyo la maana zaidi pamoja na kulinda Muungano.
 
Muungano ni Kiunganishi kati ya Tanganyika na Zanzibari hivyo Nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ni Moja kati ya Dawa ya Maumivu kwa kuwatuliza Wazanzibari katika Muungano.

Aidha kwa Zanzibari pia Makamu wa Kwanza wa Rais ni Dawa ya Maumivu kwa Chama kikuu cha Upinzani kwani nao pia ni Kelele kila kukicha na ndio maana wote wawili wamekabidhiwa Mikasi kwa Ajili ya Ufunguaji na Ufungaji wa Shughuli mbalimbali ndani ya Nchi kwani ni Kitulizo tosha kwao!.

Vilevile katika Mamlaka ya Kimaamuzi hawa wote wawili ni Mashahidi tu kwa Maamuzi katika Mabaraza ya Mawaziri ya Pande zote kwani Tanganyika yuko Rais na Waziri Mkuu na Zanzibari yuko Rais na Makamu wa Pili wa Rais.
 
kazi yake ni kutembea na mkasi wake maalum wa kuzindulia shule,hospitali n.k
amemwagiza baba mwanaasha aka Mzamiaji amletee mkasi mpya kutoka brazil kwani alionao sasa umeaanza kuwa butu
 
kazi yake ni kutembea na mkasi wake maalum wa kuzindulia shule,hospitali n.k amemwagiza baba mwanaasha aka Mzamiaji amletee mkasi mpya kutoka brazil kwani alionao sasa umeaanza kuwa butu
yap! Umejibu kwa ufasaha kabisa
 
kazi yake ni kutembea na mkasi wake maalum wa kuzindulia shule,hospitali n.k
amemwagiza baba mwanaasha aka Mzamiaji amletee mkasi mpya kutoka brazil kwani alionao sasa umeaanza kuwa butu
Si utani!
 
Wana jf kila uchao ninachokiona anakifanya makamu wa rais ni kufungua shule,kuhudhuria mahafali, na mengine kama hayo.Hivi hiki cheo kina umuhimu gani hasa kwa nchi kama Tz ikizingatiwa tunaye waziri mkuu!?

leo yupo mwanza kuzindua semina ya GEPF, sijui ndo katiba inasema hivyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Unafahamu lile tangazo la Voda la baba mdogo wake Clement? Basi ndio hapo hapo kabisa mwanangu, yaani ile nataka kufungua tu uzi ndio nakuta umeshafungua
 
Kila unapomuona sala zake ni baba mwanaasha afe tu! ili ashike nchi! yule ndio adui namba moja wa kikwete!
 
Back
Top Bottom