EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Kwa kweli hata mimi sielewi umuhimu wa kuwa na Makamu wa Rais. Katiba ya sasa inasema kwamba Makamu wa Rais ni Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla. Hususan (a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano; (b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais; na (c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.
Kwa Makamu huyu wa Rais ni mambo yapi ya muungano ambayo amemsaidia Rais kufuatilia utekelezaji? Ina maana hizi kazi anazofanya za kuzindua na kuwa mgeni rasmi anakuwa ametumwa na Rais? Halafu kuna hili la kufanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Sasa juzi tuu Rais alikuwa nje ya nchi na kulikuwa na mgomo wa madaktari. Je, Makamu wa Rais alifanya nini la maana kujaribu kushughulikia? Mimi nilmwona tuu alipoenda kumpokea Rais uwanja wa ndege wakati akirejea nchini. Inaonyesha labda hata madaktari walimdharau pale walipoamua kukutana na Waziri Mkuu.
Inavyoonekana ni kwamba Makamu wa Rais huwa anatekeleza madaraka yake chini ya uongozi na usimamizi wa Rais na anaongoza na kuwajibika kwa Rais kuhusu mambo au shughuli zozote anazokabidhiwa na Rais. Kwa hiyo hapa itategemeana na Rais amempa kazi gani. Kama hajampa kazi, hana cha kufanya. Na kwa vile labda hakuna kazi za kumpa, ndiyo maana labda huwa anaishia kuzindua tuu vitu, kukata utepe, kuweka jiwe la msingi na kuwa mgeni rasmi kwenye mambo ambayo yangefanywa hata na mkuu wa wilaya?