Makamu Mwenyekiti Taifa mstaafu (TLP) ahamia CHADEMA

SAKATA la wimbi la viongozi wa vyama vya siasa nchini kujiunga na Chadema, limeendelea mkoani hapa baada ya Makamu Mwenyekiti mstaafu wa TLP, Tanzania Bara, Westgate Rumambo kujiunga na chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati hivi karibuni, Rumambo alisema amejiunga Chadema baada ya kubaini ndicho chama pekee kinachotetea wanyonge.

"Jamani hivi sasa TLP haina mvuto tena, kwa wana mageuzi nchini kimeonekana ni chama cha mtu mmoja kuliko Chadema ambacho kina malengo mazuri ya kukomboa Watanzania hasa wa ngazi ya chini," alisema Rumambo.

Alisema atatumia uzoefu wake wa harakati za kuongoza mageuzi nchini, kuhamasisha jamii na kuiimarisha Chadema mkoani hapa, ili uhuru na mabadiliko ya kweli vipatikane.

Katibu Mwenezi wa Chadema Babati Mjini, Zahir Musa alisema wanampokea kwa mikono miwili Rumambo kwani ni mtu makini mwenye uchungu na mabadiliko.

Musa alisema watashirikiana na Rumambo katika uendelezaji wa Chadema mkoani hapa na wanatarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwake kwani ana uzoefu wa uongozi wa mageuzi nchini.

"Tumempokea mwanachama mpya wa Chadema na tunatarajia kumkabidhi kadi ya Chadema na kuanza mapambano ya kuhakikisha mwaka 2015 tunachukua jimbo la Babati Mjini," alitamba Musa.

Rumambo hakukabidhi kadi yake ya TLP kwa madai kuwa ilishapotea muda mrefu na baadhi ya wafurukutwa wa Chadema mjini Babati walimpongeza kwa uamuzi wa kujiunga Chadema.

Walisema hivi sasa chama pekee cha upinzani kilicho na nia ya mabadiliko makini na chenye lengo la kuwafikisha wananchi wanakotaka ni Chadema pekee na ndiyo sababu vijana wengi wanaiunga mkono.

Source HabariLeo.

Nampongeza mtoa mada kutujuza ila naomba wanachadema waje ni misemo mpya tofauti na huo hapo kwenye BLUE (wafurukutwa!!!) hii ni misemo ya kimagamba tuje na misemo kama;
>Makamanda
> Wanaharakati
>Wapigania haki
> Wachapa kazi
>Viongozi bora
> Wanadira
> Wanamwongozo
> Watetezi wa wanyonge
> Wasemakweli daima
> Wakombozi wetu
> Watenda Haki
> Wawakilishi bora
> Majemedari
> Wachapa kazi
> Wanademokrasia wakweli
>Watetezi wa wanyonge
 
Karibu kwenye harakati kama lengo ni kuwaunga mkono wana harakati katika kuleta ukombozi
 
habari zinazo uza ni za cdm za ccm ni hasara tu.

He!, kumbe ndio maana gazeti la uhuru alinunuliwi. Hata kwenye za ofisi za ccm sikuhizi wakitaka kupata habari za ukweli utakuta wanaperuzi gazeti la nchi Tanzania daima,mwanannchi na kidooogo mwanahalisi.
 
...

Rumambo hakukabidhi kadi yake ya TLP kwa madai kuwa ilishapotea muda mrefu na baadhi ya wafurukutwa wa Chadema mjini Babati walimpongeza kwa uamuzi wa kujiunga Chadema.

...
Source HabariLeo.

CHADEMA, kemeeni upuuzi huo hapo kwenye red; misemo ya kimagamba. Misamiati ya magamba na makuwadi zao isiruhusiwe kuingizwa wala kuhusishwa kwa namna yoyote na mfumo wa ukombozi wa taifa letu.

Mkuu dudus,
Napenda nikuhakikishie kwamba huo msamiati ni msamiati wa CHADEMA. CCM wanatumia neno la Wakereketwa!

Last edited by a moderator:
Mkuu dudus,
Napenda nikuhakikishie kwamba huo msamiati ni msamiati wa CHADEMA. CCM wanatumia neno la Wakereketwa!

Mkuu nafikiri 'wafurukutwa' ni msamiati wa CUF toka miaka ya 90 wakati CCM wanatumia 'wakereketwa', inaendana sambamba na Ngangari ya CUF na Ngunguri ya CCM enzi za Mahita. Wapenzi wa Chadema wanajulikana kama 'makamanda' ingawa kuna baadhi ya magazeti yanalazimisha kuwaita 'wafurukutwa'.
 
Mkuu dudus,
Napenda nikuhakikishie kwamba huo msamiati ni msamiati wa CHADEMA. CCM wanatumia neno la Wakereketwa!

Mkuu TUMBIRI shukrani sana kwa ufafanuzi japo nahisi kwa leo kidogo umeteleza. Nakubaliana na Mkuu Feedback hapo chini.

Mkuu nafikiri 'wafurukutwa' ni msamiati wa CUF toka miaka ya 90 wakati CCM wanatumia 'wakereketwa', inaendana sambamba na Ngangari ya CUF na Ngunguri ya CCM enzi za Mahita. Wapenzi wa Chadema wanajulikana kama 'makamanda' ingawa kuna baadhi ya magazeti yanalazimisha kuwaita 'wafurukutwa'.
 
Nadhani sasa ni muda mwafaka kwa TLP chenyewe kufikiria kuhamia CDM maadam mbunge wake ni mmoja tu.
 
vyama vya upinzani kama tlp, nccr, udp cuf viko tu hapo kuchukua ruzuku zao but zinajua hazitakaa zishinde uchaguzi kwa ticket ya urais...sasa hivi siasa inavyoenda ni either ccm or cdm...hivyo vyama vingine vingekua kweli vina uchungu na hii nchi wangewaambia wafuasi wao wote kuungana na kuipigia kura chadema...wakifanya hivyo ccm inaondoka hata waibe kura vipi..but kwa sababu akina mrema, cheyo, lipumba wanataka na wao kula yao hapo...that would never happen
 
Mkuu EasyFit naona una utani na Bwana Ngongo!

Mimi simo, maana hili chama la Ngongo ni chama la watu makini, wastaafu wake hawawezi kuhama hama tu wakati yeye anaendelea kuijenga TLP. Ngongo nisamehe bure, nimeona watu huku wanataja chama chetu pendwa, sasa sijui wamevizia wakati ukiwa mapumzikoni?
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa taarifa. Mara nyingine ikiwezekana mtumegee kidogo wasifu wao (hasa waliowahi kuwa viongozi wa vyama vingine) ili tuwajue kidogo.
 
Nampongeza mtoa mada kutujuza ila naomba wanachadema waje ni misemo mpya tofauti na huo hapo kwenye BLUE (wafurukutwa!!!) hii ni misemo ya kimagamba tuje na misemo kama;
>Makamanda
> Wanaharakati
>Wapigania haki
> Wachapa kazi
>Viongozi bora
> Wanadira
> Wanamwongozo
> Watetezi wa wanyonge
> Wasemakweli daima
> Wakombozi wetu
> Watenda Haki
> Wawakilishi bora
> Majemedari
> Wachapa kazi
> Wanademokrasia wakweli
>Watetezi wa wanyonge
Kazi nzuri rafiki, nimejifunza misamiati kadhaa hapo!
 
Back
Top Bottom