Makamu Mwenyekiti Chadema Taifa Kuunguruma Ukonga Kesho 15/07/2012

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Ndugu wadau wa JF,
Napenda kutumia fursa hii kuwatangazia kwamba kesho kutakuwa na mkutano wa hadhara katika mtaa wa Mongolandege Kata ya Ukonga, Jimbo la Ukonga kuanzia saa nane kamili mchana. Mkutano huo umeandaliwa na uongozi wa Chadema Kata ya Ukonga.

Mgeni wa heshima katika mkutano huo atakayeongoza mashambulizi jukwaani atakuwa ni Kamanda Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar).

Wadau wote wa kata ya ukonga, kata nyingine za jimbo la ukonga, pamoja na wanademokrasia wote toka majimbo jirani ya segerea, ilala na temeke mnakaribishwa sana.

M4C with no apology!
 
Niliona juzi Mbunge wa Ukonga analialia Bungeni kwamba anataka 2015 awepo mjengoni....nilimuonea huruma mno
 
Sasa hivi moto wa mageuzi uwake pande zote zote ili magamba yakose pa kushika!!
 
Mie nimefarijika kuona ni kata ndio wameitsha mkutano huo. hii ina maana ukombozi unakuja sasa Tanganyika
 
Ataunguruma Kizenji?

Zomba kazana kufundisha na kuwashika wanafunzi kwa akili zako hizi ni dhahiri unawaza kama Chemba Mgulu maana hata ukisoma ila ukawa mwana CCM lazima uwe kizomba zomba .Kazana labda unaweza kupata u VC hapo Chuoni siku za usoni ial sijui lini maana CCM inaishia .
 
Ntaendelea kutoa darsa wala hilo usiwe na hofu nalo, nadhani hata wewe unajifunza mengi humu JF.
 
Mie nimefarijika kuona ni kata ndio wameitsha mkutano huo. hii ina maana ukombozi unakuja sasa Tanganyika

Bruker katika jimbo letu la Ukonga tumekubaliana kwamba uongozi ngazi ya kata ndio wasimamie zoezi la kuieneza M4C. Na hadi sasa tumeshafanya mikutano kama hii katika kata za kitunda, majohe, chanika, pugu na Ukonga. Hii ni mara ya pili kwa kata ya Ukonga kuwa na mkutano ndani ya kipindi cha miezi miwili.
Ni dhahiri kwamba watu wameamua kufikisha elimu ya uraia na ukombozi kwa nguvu zote. Kinachotakiwa ni kuwaunga mkono tu ili moto uendelee kuwashwa!
 
Last edited by a moderator:
Basi ataunguruma kibara! Natamani nisikilize anavyoiga sauti za wachungaji wa kondoo wa bwana, kama afanyavyo Slaa na Mbowe na wengineo.

Tehe tehe tehe.
Karibu sana zomba kesho umsikilize mpemba mwenzako anavyokandamiza kibara.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wadau wa JF,
Napenda kutumia fursa hii kuwatangazia kwamba kesho kutakuwa na mkutano wa hadhara katika mtaa wa Mongolandege Kata ya Ukonga, Jimbo la Ukonga kuanzia saa nane kamili mchana. Mkutano huo umeandaliwa na uongozi wa Chadema Kata ya Ukonga.

Mgeni wa heshima katika mkutano huo atakayeongoza mashambulizi jukwaani atakuwa ni Kamanda Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar).

Wadau wote wa kata ya ukonga, kata nyingine za jimbo la ukonga, pamoja na wanademokrasia wote toka majimbo jirani ya segerea, ilala na temeke mnakaribishwa sana.

M4C with no apology!

Pamoja sana Kamanda....
 
Huyu ni bendera tu hana lolote,mzanzibari na chadema wapi na wapi.chadema na mchaga plus church mzanzibar aende zake kupiga rakaa hukooo masjid,kaingia choo cha kike huku
 
Back
Top Bottom