Makamu M/kiti BAVICHA taifa ni pandikizi au kapewa pesa haramu?

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,192
791
Hatumsikii kwenye kazi ya kujenga Chama ila tunamsikia kwenye kubomoa, ni mmoja wa waliopandikizwa na ccm au kapewa fungu aichafue Chama? Kiongozi mzuri katika jamii au hata katika familia ni yule anayemkosoa kiongozi mwenzake kwenye vikao vya ndani au amfuate moja kwa moja kujua sababu ya kiongozi huyo kufanya jambo hilo.

Hivi katika familia mzazi mwenzako ukihisi amekosea unaita press conference ili kuwatangazia maadui zako? Dada yetu ajiangalie kama yuko sawa, vijana tutaanza kupoteza imani na uwezo wake wa kufikiri na kutatua matatizo kiuongozi katika jamii.

Nawasilisha wakuu.
 
kiukweli bwana JFM hata mm leo ndo nimemsikia huyu mtu na hii kauli ya wadada au wanawake wakuwezeshwa wanaweza ndo nn kwanini wasijiwezeshe wenyewe hebu watutolee balaa hapa na mm nimesha tuma sms zangu kwa viongozi wa juu wachukuliwe hatua za kinizamu pamoja na huyo mamluki wake (shubuda)
 
unajua njaa kitu kibaya sana. Hivi ana profession gani yule dogo? Hii ndo hasara ya kuchagua watu kwa sababu ya sex. Hawa vijana wenye tamaa za kuja kugombea ubunge watadundana ngumi mbele za watu. Kwani ukiwajibu waandishi wa habari kwamba siwezi kulizungumzia kuna shida?
 
Huyu binti sijawahi kumsikia popote.leo ndo namsikia...kwenye kupiga kazi ya kukitambulisha chama kwa watu haka kabinti kako kimya...yakija mambo ya ajabu ndo anakuwa mstari wa mbele kutoa maneno..ni nani hamjui heche kazi anayofanya...kaka kaza buti

kwanza kabisa napenda kuwapongeza wapambanaji wote walioko frontline, pili ni jambo la huyo dada yetu ambaye ni mkamu wa m/kiti na mr heche, inawezekana mr heche amekosea lkn kuna sehemu za kuwekana sana, vikao vya chama ndivyo vitakavyo fanya watu warekebishane, huyo mwanadada kukimbilia press conference ana maana gani? kauli alizo toa ni mbaya na hatari kwa mshikamano wa chama ktikatika kipindi hiki kigumu cha kuondoa ukoli mamboleo wa ccm, chadema ni chama cha watu makini mwangalieni huyo dada kwa makini kabla hajafanya damage kubwa,
 
Wakuu naombeni mnifungue macho, maana mwenzenu nimeshindwa kutofautisha CCM na CDM.
Changamoto ndogo kihivyo watu wanapoteana uwanjani utadhani Man U au Yanga?
 
Ninachomshukuru Mungu ni kwamba huu upuuzi umejitokeza mapema,na sasa tumejua rangi halisi za watu bila kuchelewa naomba uongozi wa juu CDM,warekebishe hizi kasoro zilizojitokeza ili 2015 tufike tukiwa na nguvu na mshikamano,
CHADEMA FOR LIFE.
 
Huyu mwanadada so called Juliana Shonza na makamu mwenyekiti wa Bavicha aliniacha hoi sana tu na niko na hasira naye sana tu iweje kwanza hatujawahi kumsikia hata siku moja kuwa kavuna wanachama leo hii sijui kapewa kitu kidogo na Shibuda ili nae achafue hali ya hewa hapa,hana maana kabisa na sio mpambanaji wa kweli dada angu acha njaa kama ushanza kutumiwa na Magamba ni afadhali uachie ngazi wapo wadada makini sana tu kuliko wewe.
Pili kupingana kwako na mwenyekiti mapambanaji wa kweli kila leo anavuna wanachama wapya lakini wewe umekaa tu hata wengi wetu tulishasahau kwamba kuna makamu mwenyekiti sio ustaarabu uliotumia i hope mko na ofisi moja i mean kwenye jengo moja yaaani umeshindwa kwenda kumuona Mwenyekiti naa kuongea nae? kusema kweli wewe ndio umeanza kuonyesha tabiaa mbaya.
Unatakiwa ukumbuke kuwa Shibuda sio mara yake ya kwanza kufanya mambo ya ajabu ndani ya chama sasa huo uwezo wa wewe kumsemea au kumkingia kifua Shibuda umeupata wapi kama kweli wewe ni mpamabanaji basi fanya mikutano kila sehemu kwani sio haramu hata kama una majukumu mengine ili siku moja tusikie makamu mwenyekiti kamanda Juliana Shonza katingisha sehemu flani .Nakupa akiba ya maneno uombe msamaha au urekebishe kauli yako on the same media na hapo huenda tukakuelewa kwa mbaliiii.
 
ni mapungufu na busara zingetumika kumaliza huu mkanganyiko,inawezekana heche akawa amekosea ila before mdada kukimbilia press kungekuwa na nafasi ya kulizungumza iwe ni kati ya heche na makamu wake au kwenye vikao vyao na kulimaliza vinginevyo heche na makamu wake hawana mawasiliano kiasi kwamba kila mtu sasa anajiamulia kutoa tamko kitu ambacho kinatia mashaka nyazfa zao na utendaji kazi wao kwa ujumla
 
Upepo wa Nassari umepita sasa mnatafuta wa Heche na M/mwenyekiti. Mbona hakuna issue hapa, kama mtu anatoa kauli kukanusha ya mwenzake kwa kuwa tu haikupitishwa kwenye vikao rasmi na pia anayesema hivyo nae yake haikupita kwenye vikao rasmi basi itakuwa kazi sana kuongoza. Nini maana ya mtendaji (katibu)?. Hawa vijana wa CDM wote wapo sahihi kwa ulewa wao. Ila kibaya zaidi ni kwamba they are all WRONG KWA KUENDELEZA KUMZUNGUMZIA SHIBUDA MAJUKWAANI. SHIBUDA NI WA KUPUUZWA NA KAMA KANJANJA AKIKUULIZA SWALI MWAMBIE KUWA WEWE SI MSEMAJI WA SHIBUDA WALA MSEMAJI WA ALIYEMKOSOA SHIBUDA HIVYO WATAFUTENI MUWAULIZENI WAO.
 
Hatumsikii kwenye kazi ya kujenga Chama ila tunamsikia kwenye kubomoa, ni mmoja wa waliopandikizwa na ccm au kapewa fungu aichafue Chama? Kiongozi mzuri katika jamii au hata katika familia ni yule anayemkosoa kiongozi mwenzake kwenye vikao vya ndani au amfuate moja kwa moja kujua sababu ya kiongozi huyo kufanya jambo hilo. Hivi katika familia mzazi mwenzako ukihisi amekosea unaita press conference ili kuwatangazia maadui zako? Dada yetu ajiangalie kama yuko sawa, vijana tutaanza kupoteza imani na uwezo wake wa kufikiri na kutatua matatizo kiuongozi katika jamii. Nawasilisha wakuu.

Huyu ni mamluki aliyekuja kuvuruga chama.Atimuliwe haraka iwezekanavyo
 
Back
Top Bottom