IshaLubuva
JF-Expert Member
- Dec 4, 2008
- 250
- 11
Kabla ya Juni 2010 ilikuwa ukipita kwenye barabara zenye bahati ya kuwa na nguzo za taa za ummeme zinazomulika barabarani ilikuwa ni kawaida kuona mabango ya kampuni mbalimbali za simu za mkononi yakiwa na matangazo yao ya kujinadi. Lakini kwa sasa hali iko tofauti sana kwani badala ya kuona matangazo ya kampuni za simu, kuna picha za Jk zikiwa na ujumbe wa chaguo letu, ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Hakuna hata sehemu moja ambayo utaona tangazo la mgombea wa chama kingine.
Je inamaana hayo mabango huwa ni ya CCM au vipi?. Kama siyo kwani vyama vingine havina haki ya kuyatumia kwa ajili ya uchaguzi hata kama ni kwa kuyalipia (kwa kuzingtia kwamba nguzo za umeme ni mali ya shirika la umma) kama ambavyo huwa kuna fursa ya vyama vyote kutumia vyombo vya habari vya serikali?