Makampuni kuchangia vyama vya siasa ruksa

kizunguzungu wandugu, kampuni inapiga kura ngapi kwenye uchaguzi, huona wakiombwa kura wananchi mmoja mmoja kwa uwingi wao, ------------------------mwenye duka, una panadol hapo!! naam tembe ya blista, ---- nitarudi baadae..

Ni kweli hayapigi kura lakini ndiyo yamebeba hatima ya maisha ya wapiga kura baada ya chaguzi kwa kupitia ajira na kodi kama nilivyosema.Wananchi wakitaka barabara utajengea nini? kodi na kodi kubwa si zile ndogo.Kampuni ndio zina hizo hela za kodi.Ndio maana marekani na usomi wao wanasiasa hunyenyekea makampuni .Nyerere alikataa kunyenyekea makampuni matokeo tuliyaona makampuni yaliisusa tanzania.Watu walivaa hadi magunia,biashara zilikuwa tupu na serikali ilikuwa haina hata hela za kununua mafuta.Kodi zilikuwa ndogo.Serikali ilishindwa kutimiza matakwa ya raia wapiga kura wakereketwa walioipigia kura serikali kwa asilimia 90 na zaidi.Baadaye ikarudisha makampuni kwa mlango mwingine.Nyerere akagoma kugeuka jiwe akatumia neno la kiutu uzima la kung`atuka.Ukweli aliamua kuweka nyundo chini baada ya kuona nchi nyeupe haina kodi.Mtu mzima akitoroka magumu tunaita kung`atuka siyo kutoroka magumu.

Ndiyo makampuni hayakuwa wapiga kura lakini yalishikilia hatima za kodi na maisha ya mtanzania.Hivyo chama chochote kikishambulia makampuni ambayo ndio walipa kodi wakubwa kinajiweka pabaya na kuiweka nchi pabaya na wapiga kura pabaya.Mwisho wa siku chama cha namna hiyo hata kikishinda makampuni yakisusa waliokipigia kura watakiponda na mawe kwa kwa kuona matumaini yao ya maendeleo na hivyo kuhisi wametapeliwa na chama husika.Siasa za kutangaza vita na makampuni yawe ya ndani au nje ni siasa za maji taka ambazo zitarudisha taifa nyuma enzi za karne za mawe kama inavyotokea zimbabwe.
 
Back
Top Bottom