Makampuni 210 ya Clearing & Forwarding yasimamishwa kutoa huduma na TPA

Hii ni pigo kwa Tz . Ajira nying zimepoteaa.

Kuna ajira nyingine mpya zinaibuka.Kampuni zilizokuwa hazifanyi biashara zitaanza kufanya biashara kukaba nafasi ya hao waliofungiwa.Zitaajiri watu wengine ambao hawakuwa na ajira ,Kuna wanaopoteza ajira na kuna wanaopata .

Dunia ni barabara ambayo wengine kwenye barabara hiyo hiyo muda huo huo wako kwenye msafara wa msiba na maiti wakilia wengine muda huo huo kwenye barabara hiyo wako kwenye msafara wa harusi na matarumbeta wanaimba anameremeta,anameremeta wakimwimbia bwana harusi na bibi harusi wakipiga vifijo na vigelegele.
 
Hahahaa haswa Tabata wanatusumbua sana,ila dah!!sifurahii kuna mmoja ni client wangu ananipa kazi za ramani za majengo naona amepigwa kufuli,so sad...
Wengi wapo weekend wapo kwetu pazuri, na pale opposite ya st mary's sijui panaitwaje.
 
Hii list ya makampuni ukiangalia inahusisha hata zile kampuni kubwa (multinational) ambazo kwa maadili na kutokutoa rushwa ni sera katika uendshwaji wao.
Kuna hatari, maana wengi wanadai wamelipa na wana ushahidi wa nyaraka (receipts) lakini wakienda bandarini database yao haizimo hivyo wanaonekana hawakulipa. Kikubwa kabisa wakati wa kutoa mizigo ICD na TRA ziliridhia kuwa wamelipa na kuwakabidhi mizigo kwa receipts hizo hizo!

Ukifuatilia kwa ukaribu ni wazi zikifunguliwa kesi (hata kwenye mahakama za kimataifa) tusije kushangaa bandari ambalo ni shirika la umma linatakiwa kuwalipa gharama kubwa zaidi ambazo ni kodi zangu mimi na wewe!
Acha waende wakafungue case kama wanaona wameonewa hii ni dunia huru na tuna ishi kwenye nchi ya kidenokrasia! Kama umesoma hii habari kwa makini utagundua waliambiwa walete documents zinazo thibitisha wamelipa kodi lakini walishindwa ...ulitaka waendelee kuchekewa? Kama wamelipa kwanini wasipeleke hizo documents?
 
Waliodakwa kwa uhalifu huu wako wa kuanzia ICD,TRA na wafanyakazi wa hayo makampuni!! Ushahidi sio risiti peke yake.Risiti yaweza kuwa forged.Je pesa ziliingia kwenye akaunti husika? Swala si database ya bandari tu ya benki inasemaje?
Wote walipewa muda wa kupeleka documents wameshindwa kwanini wasiondolewe kwenye mfumo? hao ni wezi...
 
Kazi ya dereva ni kuhakikisha mzigo alionao kwenye gari una nyaraka zote.Utaendesheje Lori hujui umebeba mzigo wa halali au wizi?
Anyway wewe unawatetea sana hao madereva na unasema wao hawana kosa kosa wanalo matajiri na malori yao kwa hiyo unasemaje? Kuwa baada ya hao madereva kusimamishwa kutokana na kampuni za matajiri wao kusimamishwa unashaurije? Waajiriwe kuendesha magari ya CHADEMA au unashauri nini? Maana naona umeshupalia tu hueleweki.
Wewe kweli ni punguani . hivi dereva akipewa nyaraka zilizoghushiwa au feki je, yeye ni kazi yake kugundua hilo!? Mwisho utasema ni kosa LA dereva pale nyaraka zitakapoonesha mzigo ni Wa matairi wakati kontena limejaa silaha.
 
Hao si watajibadilisha gamba na kurudi na majina mengine sijui xyz and co ltd. Wangekatazwa kutumia hayo ma a.k.a ili watambulike wenye makampuni ili wakiharibu wasijibadilishe tena na kurudi kwa majina mengine.
 
Safi sana bila kuwagusa hao wakubwa, yatakuwa yale yale ya serikali zilizopita ambao hao jamaa walikuwa ni miungu watu
 
Wanadaiwa, nadhani watalipa kama wamiliki wa vyombo wa Radio na Tv walivyofungiwa na wakalipa chap chap na shughuli zikaendelea kama kawaida
 
Wameshavuna vya kutosha hawana cha kupoteza.Ila cjaona ile ya Liz mock Transit & shifting Co.Ltd.
 
Back
Top Bottom