Makamo wa Rais Znz atembelea Israel .

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali IddiAtembelea Taasisi ya Utafiti, Uchunguzi na Usimamizi wa Uokozi na KuepukaMajanga Nchini Israel
Writtenby haki | // 0 comments
Makamu wa Pili wa Rais waZanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti,Uchunguzi na Usimamizi wa uokozi na kuepuka Majanga Nchini Israel Bwana GideonKader kwenye Hoteli ya David Ciladel Mjini Jerusalem. Kushoo mwa Balozi Seif niWaziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohdna Kulia ni Balozi wa Israel Kenya na Tanzania Bwana Kasbia Niruel Chirich.
Makamu wa Pili wa Rais waZanzibar Balozi Seif akifahamishwa hatua za mfumo unaochukuliwa wa kukabilianana Maafa katika Miji ya Israel unaotumia Mtandao wa Kisasa. Nyuma ya Balozi niWaziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd naMkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Bwana Ali Juma Hamad.
Mkuu wa Taasisi ya Usalama waRaia Nchini Israel { Home Front Command } Luteni Kanal Tai Peleg akitoa darasakwa Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif namna ya kukabiliana na Maafa
----
Taasisi ya Utafiti, Uchunguzi naUsimamizi wa Uokozi pamoja na kuepuka Majanga Nchini Israel inaangaliauwezekano wa namna ya kuisaidia Zanzibar katika harakati zake za kupambana naMaafa wakati yanapotokezea Maafa.
Kauli hiyo imetolewa na MkurugenziMkuu wa Taasisi hiyo Bwana Gedion Kandel wakati wa mazungumao yake na Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yupo Nchini humo kwa ziaraya Kiserikali mazungumzo yaliyofanyika hapo katika Hoteli ya David CitadelMjini Jerusalem.
Bwana Gedio alisema Taasisi yaketayari imeyapokea maombi ya Zanzibar na kukubali kushirikiana pamoja wakatiyanapotokezea matatizo ya Majanga na hatimaye kupelekea Maafa . Hata hivyoMkurugenzi huyo wa Taasisi ya Utafiti,Uchunguzi na uokozi pamoja na kuepukaMajanga aliishauri Zanzibar kuandaa Mpango Maalum wa maeneo ambayo Taasisi yakeinaweza kusaidia.
Alisisitiza kwamba vitengo vyaMaafa hufanikiwa vyema katika utekelezaji wa majuku yake endapo Bajeti yaVitengo hivyo inakuwa ya kuridhisha.
Kwa upande wake Makamu wa Pili waRais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pia aliiomba Taasisi hiyo kusaidiamafunzo kwa watendaji wa Kitengo cha Maafa Zanzibar ili kiwe na uwezo zaidi yaKitaalamu.
Balozi Seif alisema Majangayanayopelekea kutokea kwa Maafa yanaweza kupungua kutokana na uwajibikajimkubwa wa watendaji hao unaoambatana na Taaluma ya kina. Wakati huo huo Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake alitembelea Taasisi yaUsalama wa Raia inayojishughulisha na Maajanga Home Front Command { HFC } MjiniTelaviv.
Mkuu wa Taasisi hiyo Luteni KanalTai Peleg aliueleza Ujumbe wa Zanzinbar kwamba Taasisi hiyo imeundwa kufuatiaJanga la Maafa yaliyokuwa ayakiikumba Nchi hiyo likiwemo lile la Mashambuliziya Kivita.
Alisema Taasisi hiyo tayariimejijengea umaarufu mkubwa kutokana na watendaji wake kushiriki katika kutoamsaada wa Kiufundi kwenye Matukio ya Maafa mbali mbali Duniani.
Ameishauri Tanzania na Zanzibarkwa Ujumla kutumia fursa ya mafunzo yatakayotolewa na Taasisi hiyo katikaSemina itakayofanyika mnamo mwezi wa Septemba mwaka huu wa 2012.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali IddiAtembelea Taasisi ya Utafiti, Uchunguzi na Usimamizi wa Uokozi na KuepukaMajanga Nchini Israel
Writtenby haki | // 0 comments
...Alisema Taasisi hiyo tayariimejijengea umaarufu mkubwa kutokana na watendaji wake kushiriki katika kutoamsaada wa Kiufundi kwenye Matukio ya Maafa mbali mbali Duniani.

Ameishauri Tanzania na Zanzibarkwa Ujumla kutumia fursa ya mafunzo yatakayotolewa na Taasisi hiyo katikaSemina itakayofanyika mnamo mwezi wa Septemba mwaka huu wa 2012.

Patamu hapo. Baniani mbaya kiatu chake dawa!!
 
Ile ya Papa Benedict kwenda Uturuki mbona hukuleta hapa?? Anyway, ahsante kwa taarifa.
 
Amebarikiwa yule aibarikiye Israel

Naam! Am'barikiye Ibrahim, na Isaka, na Yakobo hakika mkono wa Bwana utakuwa pamoja naye. Kwa mtindo huu hakika Zanzibar itapaa kila idara. Njia waliyoichagua ni njema sana.
 
Ile ya Papa Benedict kwenda Uturuki mbona hukuleta hapa?? Anyway, ahsante kwa taarifa.

Iletwe hapa ya kazi gani? What is Uturuki? Hapa tunaongelea habari za Israel, lile taifa teule.
 
Amebarikiwa anaeibariki israel, amelaniwa aneilani israel. Kama lengo lenu ni zuri hakika sasa hivi mtakuwa mbali. Na hekima hiyo hamjafunuliwa na mwanadamu bali mungu mwenyewe. Hakika mungu hana upendeleo.
 
Leo nimeskia kua wataisaidia sekta ya KILIMO,haya waisrael wameletwa na watanganyika????SEIF IDDI AMEWAFATA MWENYEWE
 
WA kwanza yuko kwa kina Amne Samne kimatibabu zaidi. Siasa za bongo headache lazima uwe ngangari....oohoooo!!
 
Back
Top Bottom