Makamo wa Rais yuko wapi mgomo unapoendelea?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Rais anapokuwa nje ya nchi ni makamu wa rais anayeshika madaraka siyo waziri mkuu. Tangu mgogoro huu uanza tumemsikia sana waziri mkuu. Najiuliza yuko wapi makamo wa rais na kwa nini impression inaachwa kuwa in the absence of the president it is the prime minister who is incharge?
 
Kukata utepe, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kushirlki warsha ndio kazi za dr bilal a.k.a mzee wa mkasi hayo mengne co shughuli yake.
 
Hiki ni cheo cha kisiasa kilichobuniwa ili kuepuka mgogoro wa kisiasa/kiuongozi iwapo CUF ikishinda ZNZ, huku CCM ikishinda Bara hivyo kuwa na mamlaka ya kuunda serikali ya muungano chini ya katiba ya sasa. Ni muundo ambao Tume ya Jaji Bomani iliuazima kutoka kwenye mfumo wa marekani. Otherwise ni title isiyokuwa na maana yoyote zaidi ya kumaliza fedha za walipa kodi. Cheo hiki kilionekana kuwa na kazi za kufanya miaka ya nyuma kwasababu tu kilibebwa na vyeo vya 'waziri mkuu na makamo wa kwanza wa rais', na Rais wa ZnZ na makamo wa pili wa rais'; Cheo hiki hakina maana bila ya kubebwa na cheo kingine practical; Bilal kwa mfano akipewa cheo kingine kama - Makamo wa Rais na Waziri wa Maji, hapo ndio tutaona umhimu wake ambao utakuwa ni maji lakini akiwa kidogo na nguvu za kisiasa kuliko mawaziri wengine; uwaziri wa maji ni mfano tu wa kusisitiza kwamba hiki cheo ni useless;

Pia, ingawa in theory katiba inasema hes second in line, in practice, he is fourth in line after Rais was Muungano, Waziri Mkuu, Rais wa ZnZ. Huu muungano unaumiza sana kichwa - Kwa mfano, Makamo wa kwanza Wa Rais ZNZ (Maalim Seif) na makamo wa pili wa Rais Znz (Balozi iddi), wana uhusiano gani kikazi na makamo wa Rais wa Muungano (Bilal) zaidi ya kukutana kunywa kahawa na kuteta udhaifu wa muungano?
 
Rais anapokuwa nje ya nchi ni makamu wa rais anayeshika madaraka siyo waziri mkuu. Tangu mgogoro huu uanza tumemsikia sana waziri mkuu. Najiuliza yuko wapi makamo wa rais na kwa nini impression inaachwa kuwa in the absence of the president it is the prime minister who is incharge?

He is just a ceremonial leader.
 
Rais anapokuwa nje ya nchi ni makamu wa rais anayeshika madaraka siyo waziri mkuu. Tangu mgogoro huu uanza tumemsikia sana waziri mkuu. Najiuliza yuko wapi makamo wa rais na kwa nini impression inaachwa kuwa in the absence of the president it is the prime minister who is incharge?

Labda hajapangiwa kufanya hiyo kazi na mkubwa wake kwa mujibu wa katiba.
 
Kukata utepe, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kushirlki warsha ndio kazi za dr bilal a.k.a mzee wa mkasi hayo mengne co shughuli yake.

He he he he he JF kuna mambo jamani! Hahahahahha, mkuu Degedege hiyo avarta yako imeniacha hoi. Back to topic, Dr Bilal hana shida ya kujihangaisha na hizi ngojera, kazi yake ni lainiii.
 
Hicho ni cheo maalum cha Wazanzibar ili kubalance muungano feki, huyo hana hata uwezo wa kumfukuza kazi Mtendaji wa kijiji.
 
Makamu wa Raisi ana nguvu sana kikatiba, huyu tulimpigia kura pamoja na mh. Raisi, yupo kwa ridhaa yetu, si kama mh.Pinda aliyewekwa kiushikaji, tatizo lilopo ni migongano ndani ya uongozi wa mh. Kikwete inawezekana kabisa hajishughulishi sana kutokana na makundi yanagongana kila siku ndani ya serikali, tusisahau kuwa serikali inajiendesha kiushikaji. Bilali ni msomi mzuri sana na uwezo wa kuongoza bila matatizo.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom