Makamishna wawili wa ZEC wasema hawatambui uamuzi wa kufuta matokeo

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Makamishina wawili kati ya saba wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) leo wamesema hawatambui uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar.

Wamesema uchaguzi wa marudio ni batili.

Ni msamiati tu huo,mods uvumilieni,
katika taarifa ya habari (ITV) ,wamejitokeza kamishna na kuzidi kuusema ukweli kuwa mambo ya jecha hayana uhusiano na ZEC ni yake binafsi na yasichukuliwe ndio msimaamo wa ZEC.

Wakizidi kumruka Jecha kama CCM walivyoanzaa kumkimbia Jecha ,makamishna wamedai kuwa hawajui wapi Jecha anapokeaa maagizo na malalamiko kibao yaliyowakilishwa na CCM yalitupiliwa mbali hata jechaa alishiriki katika msimamo wa kuyakataa maombi ya CCM ambayo Tume ilikuwa hayawahusu ni mambo ambayo yalitakiwa kupelekwa mahakamani ,jecha alitoweka na kutoa misimamo akiwa hajulikani alipo .

kwa kweli CCM hawana pa kujificha , eti na wao hawakupendelea kutangazwa uchaaguzi kurudiwa kwa kuwa walikuwa wamekwisha shinda ,suaali walijuaje kama walikwisha shinda ? Mbona hawadai kumtaka Jecha aendelee kutangaza matangazo ,

jecha hebu zuka uendelee na matangazo japo mafichoni ITV hawana noma !
 
Makamishina wawili kati ya saba wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) leo wamesema hawatambui uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar.

Wamesema uchaguzi wa marudio ni batili.
Wana wazimu hao.. Kuna Makamishna saba na wawili wamekataa inamaanisha watano wamekubali kwa hivyo majority imeshapatikana hapo.. ili uamuzi uwe batili makamishna wane wakatae.. sasa hao wanapiga zogo bure na kujitafutia umaarufu...maneno yao hayana uzito wowote
 
Siku zote nilitamani kusikia kauli za hawa makamishina.Hii hatua ya wao kutoa kauli imechelewa sana.But wazungu wanasema: "better late than never."Tunawashukuru.
 
Makamishina wawili kati ya saba wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) leo wamesema hawatambui uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar.

Wamesema uchaguzi wa marudio ni batili.
Kweli ni batili, iweje kura za rais wa muungano ziwe halali na zilijumulishwa akapatikana Magufuli. Na zile za wawakilishi wazanzibar na rais Zanzibar zifutwe,wakati tume ni moja, nayo ni ZEC. Huo ni upuuuzi mtupu,.
 
Wana wazimu hao.. Kuna Makamishna saba na wawili wamekataa inamaanisha watano wamekubali kwa hivyo majority imeshapatikana hapo.. ili uamuzi uwe batili makamishna wane wakatae.. sasa hao wanapiga zogo bure na kujitafutia umaarufu...maneno yao hayana uzito wowote
Naona hujielewi wewe! Hawa ni wale waliojitokeza wazi wazi,wale wengine wanaogopa kutoka hadharani hatujui nyoyo zao zina nini.
 
Wana wazimu hao.. Kuna Makamishna saba na wawili wamekataa inamaanisha watano wamekubali kwa hivyo majority imeshapatikana hapo.. ili uamuzi uwe batili makamishna wane wakatae.. sasa hao wanapiga zogo bure na kujitafutia umaarufu...maneno yao hayana uzito wowote
Kabla ya Jecha kufuta matokeao kuna kikao walikaa na kupiga kura kupitisha uamuzi wa kufuta matokea?Kana hawakukaa,tangazo la Jecha lina uhalali gani kisheria?
 
Wana wazimu hao.. Kuna Makamishna saba na wawili wamekataa inamaanisha watano wamekubali kwa hivyo majority imeshapatikana hapo.. ili uamuzi uwe batili makamishna wane wakatae.. sasa hao wanapiga zogo bure na kujitafutia umaarufu...maneno yao hayana uzito wowote
Meza mate mkuu. Naona umepaniki. Kwani umeambiwa wanahitaji akidi ili kutoa mawazo yao?
 
Back
Top Bottom