Elections 2010 Makame wa NEC Tz kuwa kama Kivuitu wa NEC ya Kenya?

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Dalili zinaonyesha ushindi mkubwa kwa Dr Slaa wa Chadema kuwa rais mpya wa Tanzania. Lakini kuna kiza kinene kama matokeo yatakayotangazwa yatafanana na maamuzi ya wananchi katika kura. Je Jaji Lewis Makame wa NEC ya Tanzania atageuka kuwa Kivuitu aliyeleta balaa Kenya kwa kukubali kutangaza matokeo ya wizi, ama Makame ataamua kujiuzuru kukataa kutangaza matokeo yaliyopikwa na CCM ili kulinda heshima yake na ya nchi yetu?
 
Makame akileta za Kenya Damu ya watanzania itakayomwagika kwa kupigwa maeneo tofauti tofauti Tanzania ili kukubali matokeo itakuwa juu yake
 
Makame akileta za Kenya Damu ya watanzania itakayomwagika kwa kupigwa maeneo tofauti tofauti Tanzania ili kukubali matokeo itakuwa juu yake

Maluweluwe si unayaona lakini, mara Shimbo, halafu REDET na sasa Takwimu za NEC zinazotia mashaka, huyu Makame naona kama anaishia huko.
 
Makame atake asitake lazima atangaze matokeo kama atakavyoelekezwa na 'mwajiri' wake. Hapo ndipo tutajua umuhimu wa kuwa na tume huru ya uchaguzi. Hivi mnatarajia afanye vinginevyo?

"It's not the people who vote that count. It's the people who count the votes." - Josef Stalin.

Na "wanaohesabu" na kutangaza matokeo tukumbuke ni NEC (inayomilikiwa na walio madarakani). Hivyo tujiandae kuhesabu maumivu! Ni ukweli ingawa unauma!
 
Back
Top Bottom