Makamba: Suala la Masauni kughushi cheti cha kuzaliwa, Kushughulikiwa na Polisi!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba amedai kuwa suala la kughushi cheti cha kuzaliwa na hivyo kudanganya umri sasa litashughulikiwa na Jeshi la Polisi. Amedai pia kuwa hajui Polisi watalishughulikia vipi, ila hawatawaingilia kazi yao!

SOURCE: Tanzania Daima.
 
Mwenyekiti wa CCM, ndg JK alidai kuwa kijana ni mchapakazi na atapangiwa kazi nyingine, yeye kwake udanganyifu sio issue!
 
Danganya toto iyo mbona the so called Dr mpaka leo ni feki hamjashughulikia
 
Mwenyekiti wa CCM, ndg JK alidai kuwa kijana ni mchapakazi na atapangiwa kazi nyingine, yeye kwake udanganyifu sio issue!

Kwani kikwete anasemaga ukweli wowote? Of course tunajua kuwa yeye ni muongo na mwizi!
 
Polisi wenyewe hawafanyi kazi yao kwa mambo yanayohusisha vigogo mpaka waambiwe wafanye.
Wakati mwingine inawezekana kuwa police wanawasaidia vigogo kufanya uhalifu, chukulieni mifano ya EPA, IGP na wenzake walisema wahalifu wale hawakamatiki ingawa wanajulikana, Mwisho wa yote Rais akawasamehe wale waliorudisha pesa na wengine ambao hawakurudisha kama KAGODA n.k. Kisheria Rais anaweza kuwasamehe watu wakishahukumiwa na mahakama, siyo kabla hata ya upelelezi kukamilika.
Tusitegemee chochote kuhusu Masauni kutoka polisi pamoja na kwamba hilo ni kosa la jinai.
Kuhusu JK kumpa kazi nyingine, ni kawaida kwake kwani tumeona akiwaacha watuhumiwa wengi kwenye nafasi zao bila kujali au kuwahamisha tu.
 
Tatizo sio Kikwete wala Makamba bali ni vyombo vya usalama hususan polisi. Hili ni kosa la jinai ilitakiwa polisi wamkamate mara moja na kuvichunguza hivyo vyeti na kumfikisha mahakamani, kinyume chake polisi wetu nao ni tawi la siasa linasubiri Rais awaagize, yaani @&§èçxx

"Moringe wote ni wamasai likini sio kila mmasai ni Moringe"
 
Mwachieni huyo kijana wa watu. Alifoji vyeti ili aweze kupata kazi alishe familia yake. Mbona wale waliofoji madigirii na kujiita DR bado wapo bungeni na katika baraza la mawaziri?. Mbona wale wezi wakuu wa EPA, KAGODA, RADA, NDEGE YA RAISI, RICHMOD, DOWANS, MZEE WA VISENTI wako huru na bado wako katika nafasi zao mpaka sasa?. What the f~#@$& is going on katika nchi hii?. Bora nikaombe uraia Somalia kuliko raia wa Tanzania.
 
kazi hipo kwa wanasiasa kwani karibu 2010 inafika makundi na minyukano ianze, sijui ni akinanani watashinda na wapi wataanguka lakini nchi sasa inayumba sana busara na baraka za mungu ndio kinga ya machafuko na kuleta mabadiliko kwani siasa imeshindwa
 
Mwachieni huyo kijana wa watu. Alifoji vyeti ili aweze kupata kazi alishe familia yake. Mbona wale waliofoji madigirii na kujiita DR bado wapo bungeni na katika baraza la mawaziri?. Mbona wale wezi wakuu wa EPA, KAGODA, RADA, NDEGE YA RAISI, RICHMOD, DOWANS, MZEE WA VISENTI wako huru na bado wako katika nafasi zao mpaka sasa?. What the f~#@$& is going on katika nchi hii?. Bora nikaombe uraia Somalia kuliko raia wa Tanzania.

Unataka kusema kuwa makosa mawili yanafanya kosa la tatu kuwa sio kosa?
 
Mwenyekiti wa CCM, ndg JK alidai kuwa kijana ni mchapakazi na atapangiwa kazi nyingine, yeye kwake udanganyifu sio issue!

Mfanyakazi kwa standard zipi? JK ana standard zake za kufanya kazi ndio maana tunaona madudu tunayoyaona. Utasemaje mtu ambaye ametumia hila kupata madaraka atapangiwa kazi nyingine? Una uhakika gani hatatumia hila kupata mambo mengine kwa gharama kubwa kwa Taifa?
 
Polisi wenyewe hawafanyi kazi yao kwa mambo yanayohusisha vigogo mpaka waambiwe wafanye.
Wakati mwingine inawezekana kuwa police wanawasaidia vigogo kufanya uhalifu, chukulieni mifano ya EPA, IGP na wenzake walisema wahalifu wale hawakamatiki ingawa wanajulikana, Mwisho wa yote Rais akawasamehe wale waliorudisha pesa na wengine ambao hawakurudisha kama KAGODA n.k. Kisheria Rais anaweza kuwasamehe watu wakishahukumiwa na mahakama, siyo kabla hata ya upelelezi kukamilika.
Tusitegemee chochote kuhusu Masauni kutoka polisi pamoja na kwamba hilo ni kosa la jinai.
Kuhusu JK kumpa kazi nyingine, ni kawaida kwake kwani tumeona akiwaacha watuhumiwa wengi kwenye nafasi zao bila kujali au kuwahamisha tu.

Yaani umesema kweli....mfumo mzima uozo mtupu. Siasa imekuwa kila kitu, wezi, vihiyo, na watenda maovu wote wanapeta ili mradi wawe upande wa chama tawala! JK anaendelea kukumbatia uozo kila kukicha!
 
JK ameongea vapour na Makamba ndio anaongea matapishi kabisa.. Hujui polisi watashuhulikia vipi forgery and fraud kubwa kama hiyo. Inamaana CCM hawana policy dhidi ya wanachama wao kuvunja sheria na kukikuka maadili. Baada ya kuwahimiza polisi wafanye kazi yao Rais na Katibu Mkuu wana support uvunjaji wa sheria. Bora ata Makamba mwenye digrii ya mafenesi angesema hivyo na huyu Dr wetu Honoris Causa..lol nae ameshindwa kukemea hivi vitu.. Tanzania = Taarabu mipasho..
 
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba amedai kuwa suala la kughushi cheti cha kuzaliwa na hivyo kudanganya umri sasa litashughulikiwa na Jeshi la Polisi. Amedai pia kuwa hajui Polisi watalishughulikia vipi, ila hawatawaingilia kazi yao!

SOURCE: Tanzania Daima.
Ndio maana masauni yupo hivi?
 
Na suala la kijana wa kolomije kugushi cheti limefikia wapi?

Back
Top Bottom