Makamba: Msifadhaike!

uropokaji wake na kusema hovyo ndio vitu nilivyokuwa na mpendea makamba kwasababu vilisababisha kuimarika kwa chama chetu na kupata majimbo mengi kwenye uchaguzi uliopita. Alitakiwa aendelee kuwepo ili tujihakikishie ushindi wa kishindo 2015.

Tatizo watu hajakuelewa! Unanposema "CHAMA CHETU" wanadhani unamaanisha CCM, wakati wewe unamaanisha chama chetu kileeee au sio?
 
Huo ni mwanzo kwa CCM, Finally 2015 Chadema watakapochua nchi. Peoplesssssssssssssssssssss poweeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!
 
Sijui kama kweli ni CC ndiyo tatizo ndani ya CCM. kujiuzulu kwa CC na Makamba siyo dawa hata kidogo. Mweneyekiti ndiyo tatizo, anafuata upepo wa kisiasa unakoelekea ndiko anakoegemea. Mfano Siku moja Kamati kuu ilipitisha kuwa Dowans lazima walipwe fedha zao baada ya kushinda kesi, baada ya siku mbili kwenye kikao cha wabune Raisi/Mweneyekiti wa chama akageuka maamuzi aliyofanya na wenzake akasema wasilipwe.
Mfano mwingine, Kwa sasa nchi ina shida kubwa ya miundombinu ya barabara, Waziri wake anachukua uamuzi w kusimamia sheria ili maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya upanduzi wa barabara yabomolewe yawe wazi. Wapambe wakamtumia Mesege Raisi/ Mwenyekiti wa chama akaigeuza sheria kuwa waache tu waliojenga kwenye eneo la barabara waendelee kukaa, hakujali kabisa sheria inasemaje. Mtu kama huyu utafanyaje naye kazi?

Kwa mifano hii michache, siamini kabisa kuwa tatizo au gamba la CCM limevuliwa, hii kuchukua mvinyo mpya kuweka kwenye chupa ileile.

Natabiri migogoro zaidi.
 
Mbona hata huyo Mukama ni mtu wa jaziba jaziba tu. Nadhani kwa wana CCM wanaoshangilia kuondoka kwa mzee Makamba watafadhaika watakapo gundua hata huyo mpya hana jipya!
 
Nilivyomwelewa Yusufu Makamba, alipotoa neno lake alipotakiwa aseme neno la kuaga wakati wa kikao cha kuvuana magamba Dodoma: <Naenda kuwaandalia makao ili nilipo nanyi muwepo>.

  • Si mimi peke yangu katika sakasaka hili wakuvuliwa gamba, tuliomagamba tuko wengi humu,mimi nimeanza nanyi mnafuata.
  • Sikubali kuondoka peke yangu, wale wote tulioshiriki kuundika/ kuunda magamba, nitakuwa nanyi huko niendako.
  • Chama cha Magamba si mimi tu niliyegamba, wote tunahusika kuanzia watendaji wa vitongoji/ serikali za mitaa, madiwani,wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa tumedhihirisha magamba tuliyonayo kuanzia kwenye kura za maoni. Hivyo basi nilipo kinara wao, nao wapaswa kuwepo.
 
kwa wale waliofuatilia mchakato wa cha chama chao wa kujivua gamba na kuzaliwa upya ulioambatana na vikao muhimu viwili yaani CC na NEC ambapo tulishuhudia secretariet ya chama chao iliamua kujuuzulu.

Wakati katibu mkuu wa chama hicho bwana yusufu makamba alipokubali kuachia ngoma hiyo ambayo kwa sasa inaonekana kuwa nzito, aliweza kutoa hotuba ya mwisho kwa wajumbe wa kikao.

Cha kushangaza sana huyu jamaa aliweza kuwaaga wenzake kwa kutumia maneno yaleyale aliyoyatumia bwana wetu yesu kristo alipowaaga wanafunzi wake.

Bwana makamba aliaga kwa kusema hivi: Msifadhaike nyumbani kwa baba yangu kuna makao mengi na mimi nakwenda kuwaandalia makao.

Hivi kweli kama huyu jamaa ni mcha mungu na ukizingatia mazingira yaliyochukulia mpaka yeye na secretariet yake kujiuzulu ilikuwa ni sahihi kutamka maneno haya?
Na je yeye anakwenda sijui uraiani kuandaa makao gani na kwa wakina nani?
Je wakati wanaamua kuachia ngazi kulikuwa na masikitiko yoyote kwa wajumbe/wanachama kama ilivyokuwa wakati yesu anawaaga wanafunzi wake. Happy easter
 
mi naona ni sahihi. alikuwa ni mtu ambaye kauli zake zilikuwa zinawanyima usingizi chadema kwa kiasi fulani kama kauli za Yesu zilivyokuwa zinawanyima usingizi Banisrail..

lakini huyu kipara wa magamba ameanza kufulia kabla hata hajaanza.
 
mi naona ni sahihi. alikuwa ni mtu ambaye kauli zake zilikuwa zinawanyima usingizi chadema kwa kiasi fulani kama kauli za Yesu zilivyokuwa zinawanyima usingizi Banisrail..

lakini huyu kipara wa magamba ameanza kufulia kabla hata hajaanza.

Usiingilie mambo ambayo huya jui. Yuda askari yote afananishwe na nani? Kwani Yesu alikuwa na tamaa na madaraka au fedha. Yeye anacheza na imani za watu kunasiku itamjibu hiyo biblia hataamini. Tuangalie wakina nani wanatumia zile vipande thelathini kwa ajili ya kuuza utu wao! Kama imani yako ipo upande wa kikristo si uende ukabatizwe. Yesu hakubagua mtu yeyote na sijawahi kumuona mtu anajisifia mwenyewe mtu akijisifia mwenyewe anamatatizo. kama alifanya vizuri angesubiri watu wamsifie. Kwanza anajisafisha na biblia kwa sabu anajua alichokifanya dhamira itamsuta tu.
 
Ukweli ni kwamba alikufuru kwa kauli zake zote mbili; Ile ya kusema mda kidogo hataoneka......;na vile ile ya kusema msifadhahike.........Kauli zote hizi mbili zinamhusu Yesu Kristo na amezinukuu kutoka kwenye Biblia takatifu. Kwa namna alivyozitumia ni dhahiri zinajenga hisia ya kuwa anajilinganisha na Yesu. Hata hivyo kwakuwa mzee Makamba si muumini wa kikristo hana budi kusamehewa kwasababu aliyoyasema hajui maana yake.
 
Kwani huyu mzee kuropoka kaanza leo ? Ukimshangaa Makamba kwa uropokaji wake watu wanaweza kukushangaa weye.

Huwa anasema lolote linalomjia kichwani, bila kufikiri uzito. Kama hii kauli wenye kuamini Yesu wataona ni kama kufuru fulani hivi mtu mzima kujilinganisha na Yesu.
 
Hana lolote mnafiki mkubwa! Hawezi kufanana na Yesu hata kdogo, anatumia mifano ya Biblia bila kujua maana yake. Sina hakika kama kichwani kwake zipo zote!
 
Makamba anenda kuwaandalia makao wote waliomtema. Kwa baba kuna makao mengi anamaanisha nini? Tutaona baadae kitakachofuata. Akalale pazuri kwa baba huko anakokusema
 
Makamba anenda kuwaandalia makao wote waliomtema. Kwa baba kuna makao mengi anamaanisha nini? Tutaona baadae kitakachofuata. Akalale pazuri kwa baba huko anakokusema

Anamaanisha, ukishakuwa Capo Tanzania, kuna madili mengi hata kama inaonekana umepukutishwa na Magamba, hivyo watu wasimuone kalosti na kumdharau kwani bado channel za ulaji anazo na kama watamuheshimu atawaandalia ulaji vizuri tu.
 
kwanza kabisa makamba ni mzalilishaji kwanza analeta udini maana iweje ajifananishe na Yesu wakati yeye mwislamu wizi mtupu hata kama kavua gamba sumu ipo palepale jamani makambba ingekuwa bora ujivue gamba na uhamie chadema au nccr mageuzi HABARI NDO HIYO
 
Alishindwa kuoingea ukweli, hata Mwenyekiti wao JK ni gamba. Tofauti yao kubwa ni aina ya magamba. Makamba ni gamba la juu, JK ni gamba ambalo limeshikana na ngozi kabisa. kulivua ni kukiacha chama bila ngozi, TOTALLY DIED. BUT THE DAY IS ON THE WAY!!!!!
 
Back
Top Bottom