Makamba: Mjadala wa EPA ufungwe

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Katibu mkuu wa CCM bwana Yusuph Makamba amedai Mjadala wa EPA ufungwe kwa kuwa watuhumiwa wote wameshafikishwa mahakamani. Je ni kweli watuhumiwa wa EPA wote wameisha fikishwa mahakamani?

Adai suala hilo sasa limekwisha

Na Mussa Juma, Karatu

WAKATI Serikali ikisema inaendelea na mchakato wa kuwashughulikia watuhumiwa waliosalia wa ufisadi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ili waweze kufikishwa mahakamani, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ameomba mjadala wa tuhuma za ufisadi ufungwe kwa madai tayari watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.

Kauli ya Makamba kwamba watuhumiwa wote wa EPA wameishashitakiwa, hivi karibuni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwaambia wahariri wa vyombo vya habarinchini kuwa bado serikali inashughulikia tuhuma hizo na kwamba mengi zaidi juu ya watuhumiwa wa EPA na Richmond yatakuwa hadharani hivi karibuni.

Pia Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, aliahidi kuwa majina zaidi ya 'sangara' wa ufisadi yatafahamika kabla ya mwisho wa mwaka huu ikimaanisha kuwa mjadala wa EPA kuendelea.

"Tunamwogopa nani sisi? Hakuna tunayemwogopa, maji yanachemka. Nakuthibitishia kama Mkurugenzi wa Takukuru kuwa tuna uchungu na mali ya nchi hii. Kuanzia mwezi huu (Novemba) angalieni, mtaona matendo kwa mafisadi," alinukuliwa Hosea.

Hata hivyo watuhumiwa waliofikishwa mahakami ni miongoni mwa walihohusika na ufisadi wa Sh Sh90.3 bilioni za EPA zilizohakikiwa, bila kuwahisisha waliorudisha fedha hizo ambao Mwendeshs Mashitaka wa Serikali, Eliezeri Feleshi alisema wanaweza pia kufikishwa mahakamani.

Mamoja na hayo bado kuna watuhumiwa wa Sh42.6 bilioni za EPA ambazo zinaendelea kuhakikiwa ambaowatajulikana pia wanatakiwa kuchukuliwahatua za kisheria.

Akizungumza na wananchi wilaya ya Karatu na Ngorongoro juzi, Makamba alisema anashangaa kuona bado kuna viongozi wa upinzani wanashabikia ajenda hizo za EPA na ufisadi wakati wakijua suala hilo limekwisha.

Makamba ambaye yupo katika ziara ya kuiimarisha CCM mkoani Arusha, alisema kuna viongozi wa upinzani wamekuwa wakipita mikoani na kuendelea kulizungumza suala la EPA na ufisadi, hoja ambayo sasa imeisha.

“Ndugu zangu mjadala wa EPA na ufisadi umekwisha, Rais Kikwete tayari amechukua hatua watuhumiwa wapo mahakamani, sasa hili jambo kila siku kuendelea kulizungumza ni ajabu sana,” alisema Makamba.

Alisema viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika operesheni Sangara yao na kila kukicha wamekuwa wakizungumzia EPA na ufisadi ambao umeshashughulikiwa. Umefika muda watafute hoja nyingine.

“Mimi najua operation hiyo ni nguvu ya soda na itakuwa operesheni dagaa siku si nyingi kila siku EPA si imekwisha hiyo hoja,” alisema Makamba.

Hata hivyo, alieleza kuwa CCM inajipanga kuyatwaa majimbo ya Karatu na Tarime katika uchaguzi mkuu ujao ili kuonyesha kuwa CCM bado ni chama imara.

“Leo nimefurahi sana kwa mapokezi yenu hapa Karatu na nina imani mmeanza kuonesha kuwa lazima tulichukuwe ili jimbo,” alisema Makamba.

Hata hivyo, alihimiza umoja na mshikamano ndani ya viongozi wa CCM nchini ili kuhakikisha wanashinda uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na hatimaye Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Leo Makamba anatarajia kuendelea na mikutano ya hadhara wilayani Ngorongoro kabla ya kuondoka kesho kutwa kwenda mkoani Kilimanjaro.

Hivi sasa watuhumiwa wote wa mabilioni ya fedha EPA walioshtakiwa wameshaachiwa huru kwa dhamana.


Ufisadi ambao umebainika katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, unahusu Sh90.3 bilioni ambazo ziliibwa na makampuni 13 kwa kutumia nyaraka za kughushi.

Pia unahusu Sh42.6 bilioni zilizolipwa kwa makampuni tisa, katika mazingira yenye utata huku taarifa nyingine za wizi huo zikiwa nje ya nchi, hali iliyomfanya Rais kuongeza muda wa uchunguzi kutoka Agosti hadi leo Oktoba 31.

Source: Mwananchi
 
Acha baadhi ya Wabunge wa CCM watake huyu jamaa aondolewe kwenye nafasi hiyo. Anaropoka kila kukicha vitu visivyokuwa na kichwa wala miguu. JK inabidi amtafute mtu mwingine katika nafasi hiyo maana kuwepo kwake kunazidi kuiharibia CCM.
 
Huyu Makamba aache kamba zake hapa. Unajua wazee kama hawa upumbavu na ujinga unazidi uwezo wao wa kufikiri. Halafu mtu kama huyu ndio unaambiwa ni mtendaji mkuu wa chama oops! nilisahau kumbe ni mtendaji mkuu wa Chama Cha Majambazi.
 
..wazee kama hawa ndio sababu kubwa nchi haina maendeleo!
 
Makamba akili yake kubwa ni kwa wahindi kuomba pesa za kuendeshea chama na zingine anaweka mfukoni .So msameheni hajui yuko wapi sasa .
 
Tuetegemee kusikia nini kutoka kwa fisadi anayekosa usingizi kwa ndoto kuwa huenda yeye nae ataburuzwa mahakamani kwa tuhuma za EPA?
 
Anataka watu waamini kuwa kuna kitu anaficha, kuna mijitu mijinga kuliko nilivyofikiri.
 
atakuwa amebanwa na haja kubwa.. its one thing that makes people want to hurry things up.. iliwawahi idara husika.. Huyu mzee sijui alisoma wapi.. He's a wasteman.. And the damage that CCM inasuffer by not having a strong CEO itakuwa irreversible.
 
Ushauri kwa wana CCM - kama hakuna mwanaccm mwingine wa kuweza kuwa katibu mkuu basi afadhali kiti kiwe vacant kuliko kuwa na mtu kama huyu!!
 
Hana aibu kuzungumza jambo kama hilo hapo Karatu, Jimbo la Uchaguzi la
Dr. Wilbrod Slaa aliyeibua jambo. Haraka angerekebisha usemi wake.

___________________________________
If the blind lead the blind, both shall fall into the ditch. Matthew 15:14:
 
Swala la Kagoda si linahusiana na CCM wao wenyewe?
Anaomba mjadala ufungwe ili kagoda tusahau lakini wapi mzee utakwenda na maji na wewe.
 
Anataka watu waamini kuwa kuna kitu anaficha, kuna mijitu mijinga kuliko nilivyofikiri.

Kuna watu wengine ukisoma kauli zao au kuwasikiliza, unapata maswali mengi kuliko majibu. Hivi Makamba alifikaje alipofika?

Nina hasira na huyu babu...ngoja niishie hapa...!!! Damn!!!!!
 
I heard he is having a thinking sickness so he fails to think clearly-its crap!!; Amekariri vifungu vya biblia na quran na ndivyo vimemfikisha hapo otherwise its real a crap; sijui kwa nini JK anamshikilia lakini kwa majambaza anafaa sana
 
Mabaka oh sorry Makambakamba ni kikaragosi katumwa na mganga wake aropoke na tusishangae kusikia mengi atakayoendelea kuzungumza. Sasa hoja za CCM hapa ni zipi? Akisema Operesheni Sangara haiendi mbali - hoja yake ni ipi kama kada? Hana kitu ndio maan anarudia ya wenzake. Akapimwe upstairs!!!!!!
 
wana sababu zao za kuwapa watu vilaza madaraka kama hayo.
Hawajiamini kwa sababu ya mapungufu yao,wanajua nini kitatokea kipindi cha uchanguzi
itakapotokea wamemweka mtu strong katika nafasi nyeti halafu baadaye
naye akataka kushindana nao.
 
CCM chini ya Makamba kama katibu mkuu ina kazi nzito 2010. Serikali ya CCM chini ya mawaziri waliopo sasa wanaofanya mikutano ya siri kutumia kodi ya watanzania ili kupanga njama za kihalifu kumuhujumu raia kibiashara kutetea matumbo yao ina ngoma zito machoni mwa wananchi. Kiini cha yote haya ni Rais Bomu. Makamba mpumbavu na mawaziri wasiobebeka, wote ni wateule wa kikwete!!! Jahazi linazama.
 
huyu mzee msimlaumu sana ni kuchanganyikiwa kwani wahusika ndio wanaomhonga lela za kuendeshea hicho chama chake cha majambawazi sasa unafikiri tuhuma zikiwafika atakula wapi si atakufa na njaa lakini sisi twasema tumechoka iliobaki Mgosi wa kaya mbwai ni mbwai tu hapa hakuna cha osie wala nini hatupo lushoto hapa.
 
Back
Top Bottom