Makamba kweli umeshindwa kusoma nyakati,unatetea mafisadi?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida, Bwana Makamba bado anaendelea kushindwa kusoma nyakati.Inashangaza kuona kwamba hata kijana wake wa kazi,Bwana Komba anapotuhumiwa kutafuna mishahara ya wale alioapa kuwatetea,bado aanamkingia kifua na kumtetea.Mimi binafsi nimefika mahali sasa nasema hawa watu hawako 'serious'.Wapo kwa niaba yao binafsi,ndugu zao na marafiki zao.Watanzania inabidi tufike mahili tuseme 'enough is enough'.Tutaendelea hivi mpaka lini?
 
Mimi ninavyoona bado yuko nyuma ya wakati.Ni heri akabadilika kwani anadhani anakisitiri chama kumbe ankiua Ramadhani jema
 
Ninyi msiomjua Makamba mnateseka sana!!!
Kwanza pokeeni huruma nyingi kutoka kwangu mimi ndugu yenu ambaye sishangazwagi na lolote analofanya Makamba.

Kwa sisi tunaomjua Makamba tunakuhakikishieni kuwa hiyo ndiyo standard yake kamili. Hajakosea hata kidogo.

Mimi nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakimwamini alipokuwa mkuu wa Mkoa wa DSM. Akaja mtu akaniambia "Mkuu humjui huyu mtu ni kichekesho sana huyu" NIkampinga yule mtu. Na nikaendelea na msimamo wangu hadi alipopewa ubunge wa kuteuliwa na hatimaye Ukatibu Mkuu wa CCM. Hapo ndo niliona yale niliyoambiwa kuhusu Makamba yapata miaka 3 kabla.
 
Back
Top Bottom