Makamba kung'olewa ukatibu?

Tulishaandika haya mara baada ya uchaguzi. Ila wengi tulikuja kutukanwa na kubezwa saaana.

Kuna madudu mengi sana yalifanyika wakati wa uchaguzi. Kuna majimbo ambayo watu walikuwa wakinunua vituo na kwa hiyo kutangaza matokeo yoyote wanayotaka wao. Kuna majimbo unakuta wamejiandikisha watu 9,000 na katika hao kuna wengi hawajalipia kadi na wengine hawapigi kura ila unashangaa mtu anashinda kwa kura 12,000. Hapo ndipo unaona kweli maneno ya Dr. watu wanayatumia kikwelikweli yaani "Kura za kupewa, changanya na za kwako."

Jambo zuri alilolifanya Mkapa ni kuachia uongozi watu wabovu. CCM na Muungano vitamlipukia mtu mikononi. Na hapo kitakachofuata na mtu baki aje kutawala/kuongoza Tanzania. Nitafurahi kuwaona Mkapa na Mkewe Anna na mume mwenza Mramba wakipanda kizimbani Kisutu. Imma Advocate na Mkono Advocate nao lazima wapande. Nina imani mtoto wa Karume atarudi kwao Zanzibar na wengine wote watakaobaki watasaidia kujibu shutuma kubwa za BoT, Deepgreen nk nk nk

Hao viongozi wanaollialia kama watoto shame on them. Yaani walikuwa wanamlea Makamba siyo, hihihiiiiiiiii
Ukicheza na Nyani, MMEVUNA MABUA WAJOMBA. Msahaulike Milele.

I have the same prayer Sikonge (tusamehewe kama ni dhambi)
 
No bora abaki maana watu wa upinzani ni dhahiri kuwa huyu jamaa anachemsha na hivyo kudhoofisha CCM na hiyo itakimbiza watu wengine kwenye kambi ya upinzani.

Mang'ula aliyekuwa KM kabla ya Makamba hakuwa na manjonjo kama ya huyu bwana ila alikuwa ni smooth operator na aliijua kazi yake, viongozi na makada wengi wa ccm wanajutia ujio wa huyu bwana ni kibaraka na mropokaji, hana jipya...
 
sio rahisi kumuondoa kwa sababu jamaa ameji-identify na mafisadi ambao sasa wameshikilia mpini wa chama na hata akiondolewa bado atarudi kwani tayari amefanikiwa kuingiza watu wake kibao kupitia kura za maoni akiwamo kijana wake jym
 
No bora abaki maana watu wa upinzani ni dhahiri kuwa huyu jamaa anachemsha na hivyo kudhoofisha CCM na hiyo itakimbiza watu wengine kwenye kambi ya upinzani.

Mang'ula aliyekuwa KM kabla ya Makamba hakuwa na manjonjo kama ya huyu bwana ila alikuwa ni smooth operator na aliijua kazi yake, viongozi na makada wengi wa ccm wanajutia ujio wa huyu bwana ni kibaraka na mropokaji, hana jipya...
na mimi naona asifukuzwe maana anasaidia upinzani zaidi ya chama chake.
 
CCM ilikosea sana kumpa Makamba cheo cha ukatibu mkuu, maana katibu mkuu wa chama ni sawa na cheo cha CEO ni professional lazima mtu awe na vision uwezo na kipaji maalum kitu ambacho hakionekani kwa Makamba.

Shirika au kampuni yeyote yenye CEO bomu maisha yake huwa ni mafupi sana yaani hufilisika kwa muda mfupi. Kwa vile CCM si kampuni si rahisi kuona inavyofilisika lakini kama chama kinapoteza nuru yake ya awali tuliyoizoea ni dalili kuwa chama kinafilisika.
 
Mimi huwa nawaambia watu kuwa watu wanakurupukia professional za watu. Amin nawaambia kama makamba atajiunga na ze comedy atatengeneza pesa kuliko mnavyoweza kufikiri na alivyoweza kuota angeweza. Huku kwingine mtamlalamikia mpaka kesho.
 
Siri ya kuachwa Chiligati yatajwa.



*Makamba upepo si mzuri ndani ya CCM.
*Kamati kuu kukutana D'Salaam kesho.
*Msekwa naye atoboa, ajenda ni moja.



Na John Daniel.

HATIMAYE siri ya kuachwa kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Baraza jipya la
Mawaziri, Bw. John Chiligati, imefichuka.

Siri hiyo imetajwa kuwa ni kuandaliwa kwa Bw. Chiligati kurithi mikoba wa Katibu Mkuu wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yusuf Makamba, anayetakiwa kupangiwa kazi maalum au kupumzika kabisa siasa.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya CCM vimeeleza kuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kupitia vikao husika vya chama hicho ana mpango kumpa nafasi hiyo, Bw. Chiligati kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni uwezo wa kuhimili kuweka sawa makundi yote na ushirikiano mzuri ndani ya chama.

Sababu nyingine iliyotajwa ni uzoefu wake ndani ya chama hicho pamoja na kushughulikia nyufa zilizotokana na Uchaguzi Mkuu ambapo ushindi wa CCM ulipungua ikilinganishwa na mwaka 2005.

"Mmekuwa mkiandika sana kuondolewa kwa Mhe. Makamba katika nafasi yake lakini safari hii habari hizo ni za kweli, chama kinahitaji mabadiliko ya Katibu Mkuu kama mtendaji mkuu.

Anayeandaliwa kuchukua nafasi yake muda wowote kuanzia sasa ni Mhe. Chiligati, anaonekana kuwa ni mzuri na mtu mwenye msimamo wa kati, anayemudu makundi yote, mwenye uhusiano mzuri na waandishi wa habari, anaweza kukisaidia chama kundoa nyufa za Uchaguzi Mkuu,"kilisema chanzo chetu.

Ilielezwa kwamba tayari Rais Kikwete amejiandaa kuwasilisha hoja hiyo katika kikao maalum cha Kamati Kuu (CC) kinachotarajiwa kufanyika kesho mjini Dar es Salaam kama ajenda ya mengineyo kutoka kwa Mwenyekiti.

Vyanzo vyetu vilieleza kuwa Rais Kikwete ameamua kubaki na ajenda hiyo mkononi mwake na kuhusisha wazee wachache ndani ya chama hicho bila kutaja sababu za kufanya hivyo.

Hata hivyo duru za kisiasa zimeeleza kuwa huenda uamuzi huo unatokana na kutaka kukwepa makundi na mgongano wa kimaslahi kuhusu suala hilo.

Majira ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bw. Pius Msekwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo hakuwa tayari kuzungumzia taarifa hizo kwa kile alichoeleza kuwa hawezi kuzungumza kitu ambacho hakijaamuliwa na vikao rasmi vya chama hicho.

Alisema CCM si mali ya mtu mmoja hivyo maamuzi ya kumwondoa Katibu Mkuu na masuala yote yanayohusu chama hicho huamuliwa na kikao na si mtu mmoja huku akimtaka mwandishi wa habari hizi kumweleza kwanza alikopata taarifa hizo za kuenguliwa kwa Bw. Makamba.

Hata hivyo alipoulizwa kama ana taarifa za kikao cha CC cha kesho na ajenda zake, alikiri kwamba ana taarifa na kikao hicho huku akieleza kuwa kinatarajiwa kuwa na ajenda moja tu ya kupitisha majina ya wagombea umeya katika manispaa na majiji.

"Usipende kuandika habari za kufikirika, hayo ni maneno ya mitaani, hayana ukweli wowote wala hao waliokwambia hawawezi kuthibitisha, siwezi kuzungumzia jambo ambalo halijatoka kwenye kikao, maadili ya CCM ni kwamba taarifa inayotolewa ni ile iliyoamuliwa na kikao.

"Ni kweli kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu tarehe moja Desemba hapa Dar es Saalam, tayari tumepewa ajenda ya Kamati Kuu, ni moja tu ya kupitisha majina ya wagombea umeya, kama ipo nyingine mimi sijui na si kweli, ni maneno ya uwongo tu,"alisisitiza Bw. Msekwa.

Alisema Katibu Mkuu mwenyewe, Bw. Makamba ndiye aliyewapa ajenda hiyo moja ya CC na kusisitiza kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu hakuna kikao kilichoketi kujadili suala lolote kuhusu mabadiliko ya uongozi wa chama hicho.

Licha ya tetesi za kuenguliwa Bw. Makamba duru za kisiasa zilieleza kuwa Idara ya Usalama na Maadili pamoja na Kitengo cha Propaganda cha chama hicho, pia vinatarajiwa kukumbwa na mabadiliko makubwa kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mbali ya Bw. Chiligati kutajwa kurithi mikoba ya Bw. Makamba pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana Dkt. Emmanuel Nchimbi, anatajwatajwa katika nafasi hiyo.

Juhudi za kumpata Bw. Makamba ili kuzungumzia tetesi hizo zilishindikana kutokana kile kilichoelezwa kuwa amefiwa na yuko mkoani Tanga. Hata simu zake zote za mkononi hazikuweza kupatikana hadi tunakwenda mitamboni.

Kuondolewa kwa Bw. Makamba katika nafasi hiyo imekuwa gumzo la muda mrefu sasa, kwa mara ya mwisho ilidaiwa kuwa Katibu huyo alimsihi Rais Kikwete kumwacha ili akamilishe awamu ya kwanza ya ya miaka mitano kwa sababu mbalimbali
 
pat groly (QUOTE)

Mimi huwa najisikia vibaya sana mtu akikosea lugha ya wengine. hakuna kitu kama pat groly bali ninavyofahamu mimi ipo party glory
 
Makamba ni mtu anayeongea kwanza na kufikiri baada ya kuongea.
Kumwondoa Mangula ndio waliua chama chao cha Mapinduzi
 
Mjadala huu ungewafaa wana-CCM wenyewe lakini kwa kuwa CCM inagusa maisha ya kila Mtanzania ni muhimu suala hili likajadiliwa. Hapana shaka yoyote ile kuwa MAKAMBA amesaidia mno kuyumba kwa CCM tangu alipoingia madarakani JK.

Nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM inahitaji mtu mwenye sifa za utendaji. Makamba hana sifa hizi zaidi ya uwezo wake wa kubwabwaja jukwani na kunukuu biblia. Siasa za sasa zinahitaji mipango na mikakati ndani ya chama na siyo siasa za majukwani. Ndio maana wengi wanalilia Mangula kwani yule alikuwa mtendaji mzri asiye na makeke wala mbwembwe na majivuno. Kauli za Mangula zilikuwa ni za kisomi na hata suala la uteuzi wa makatibu wa mikoa na wilaya uliegemea kwenye merits zaidi kuliko urafiki.

Katika enzi hizi za Makamba mtu akijua kukata kiuno tu kwenye ngoma tayari anaweza kukwaa ukatibu wa wilaya, au pengine hata mkoa. Kwa hiyo tatizo lililopo pia ni kwa watendaji huko mikoani na wilayani ambao wengi wao hawana uwezo. Wamepewa nafasi hizo kutokana na urafiki au kwa baadhi yao kwa kujua kupiga majungu.

Katika enzi hizi za MAKAMBA chama (CCM) kimejaa makundi jambo ambalo lilikuwa ni nadra wakati wa Mangula. Wale ambao hawakuwa katika kundi la kumuunga mkono JK katika uteuzi wake kuwania urais wanaonekana kuwa ni maadui. Kwa hiyo ipo kazi kubwa kweli kweli ndani ya CCM kwa sasa lawama ambazo MAKAMBA hawezi kukwepa kuzibeba.

Ni wazi kuwa MAKAMBA hafai kuwa KATIBU MKUU wa CCM kwa hali ya sasa. Ikiwa hataondolewa katika muda mfupi ujao ni wazi kuwa CCM itakuwa kwenye matatizo zaidi.
 
Hawawezii kumngoaaa MAKAMBA UKATIBUU MKUU...




Sawa kabisa. Ni vigumu kumng'oa makamba kwa sasa wakati chama bado hakijatulia kitayumba. Kwahivyo watamng'oa baada ya chama kuwa na stamina yaani 2012 wakati wa Uchaguzi mwingine. Hapo ndipo Mwenyekiti wake ataamua kumchinjia baharini.
 
mnaota nyny makamba jembe na hatuwezi kulitupa kwa leo katika kipindi cha kilimo kwanza


maana tumejua wapinzani wote wanamuogopa na wanataka tumuondoe kiboko yao hatufanyi hayo sisi si wendawazimu
 
Let them kill each other, after all they are animals. TEHE TEHE TEHE TEHE !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Thank you God (QUOTE).


Huyu DOUGLAS SALLU lugha yake kwenye JF mara nyingi ni kali sana. Huwezi kuwaita binadamu wenzako 'they are animals'. Chuki zako kwa CCM zimezidi na kuvuka mpaka. Punguza jazba DOUGLAS. Uwe na lugha ya ustarabu. Hao CCM wamekufanya nini hata uwachukie hivyo. JK amechaguliwa na watu zaidi ya milioni tano. Kwa hiyo bado kuna watu wengi ambao wanaipenda CCM. Actually CCM ina peoples power kuliko CHADEMA. Mimi huwa nashangaa namna MBOWE anavyotamba kuwa CHADEMA watasaidiwa na PEOPLES POWER. Sijui ataitoa wapi labda Karatu, na Moshi.
 
Let them kill each other, after all they are animals. TEHE TEHE TEHE TEHE !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Thank you God (QUOTE).


Huyu DOUGLAS SALLU lugha yake kwenye JF mara nyingi ni kali sana. Huwezi kuwaita binadamu wenzako 'they are animals'. Chuki zako kwa CCM zimezidi na kuvuka mpaka. Punguza jazba DOUGLAS. Uwe na lugha ya ustarabu. Hao CCM wamekufanya nini hata uwachukie hivyo. JK amechaguliwa na watu zaidi ya milioni tano. Kwa hiyo bado kuna watu wengi ambao wanaipenda CCM. Actually CCM ina peoples power kuliko CHADEMA. Mimi huwa nashangaa namna MBOWE anavyotamba kuwa CHADEMA watasaidiwa na PEOPLES POWER. Sijui ataitoa wapi labda Karatu, na Moshi.
Kwenye bold, nafikiri hujaielewa slogan ya CDM, Peoples power..... si uwingi wa watu bali uwezo wa elimu ya uraia ya hao watu. CDM hawaendi kupigana mtu kwa mtu wanaenda kushindanisha hoja kwa wapiga kura ni sawa na wabunge watano wa CDM walivyowafunika wabunge zaidi ya mia mbili wa CCM hiyo ndiyo maana halisi ya Peoples power, lakini kama wewe ni mwana CCM huwezi ku interpret sawa na CDM wanavyo interpret.
 


Mimi nilikuwa nawambia mwanzoni kuwa hakukuwa na Card fake za CCM ni ETHICS ilivurugwa hamkunielewa kwani nilijionea kwa macho yangu mwanachama ameandikishwa siku mbili au moja kabla kupiga kura za maoni ulisha ona wapi na jina unalikuta kwa Reja??

Card maelfu na maelfo hazikuwa na picha wala stakabadhi ya ndani au malipo ya uanachama ya miezi mitatu tu nyuma?? ati kupiga kura card iwe na stamp(mhuli wa katibu tawi) na jina la mwenye kadi utathibitishaje kuwa yeye ni ndie mwenye Card halali ya CCM?

Ndio Hayo mambo Mtangazanji Mmoja wa Clouds FM G. Hando kipindi cha PB alisema CCM wao wenyewe watatatua matatizo yao wenyewe na wasijaribu kuyahusisha na watu wengine wao ndio walio sababisha madudu yote hayo leo wanaanza kugeukana tena.

Kwahio tukubaliane kuwa matokeo yote haya ya kura za maoni ni batiri??Au???


very good observation mkuu.yaani kata ya sinza walipiga kuwa mpaka mahausigeli ,yaani beki tatu kusoma hajui anaambia weka tiki kwa yule wa kwanza kushoto kwako...na jamaa akapita kura za maoni lakini kwenye uchaguzi mkuu CHALI.....
 
Back
Top Bottom