Makamba atumia Biblia kuwalaani Chadema: HUYU MZEE KACHANGANYIKIWA

Au padiri mwenye wake wawili

Bwana zoba you amaize me my friend,nimeona thread yako ukilaani CDM kwa kitendo chao.Huwa najiuliza inakuaje mtu kama wewe educated(at least you can use the internet) unaona sakata za wana Chakachua Chako Mapema wizi,very poor leadership,ufujishaji mkubwa wa mali za umma,uchakachuaji wa haki za raia na ukawa na ujasiri mkubwa na kujivunia kuwa mwana Sisiem,people like you amaize me.
 
Embu subirini kwanza ! Ivi bibilia haikusema hivyo ? Hapa kuna waumini wa dini ya Yesu ,mnaweza kuitetea bibilia hapo,kwani kama Makamba amenukuu sawasawa basi hakukosea ,au mnaongeaje ,amesema uongo na kuizulia bible ?
 
"Ukisoma Biblia katika kitabu cha Warumi Sura 13, imeandikwa " Itiini Mamlaka inayowazidi nguvu; hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu,"

Hivi ni kweli tunatakiwa kutii kila mamlaka kwa kuwa imetoka kwa Mungu?
 
Wewe ni mshabiki tu, hujui unachozungumza,, Quran inasema Wameruhusiwa kupigana wale ambao wamedhulumiwa haki yao, ispokuwa kama dhalim akitaka suluhu AMANI itawale.
The Qur’an also tells us that Christians insist
on their (false) theological positions and that they are “turned away” (5:75). They “confound
the truth with falsehood and knowingly conceal the truth” (3:71) and therefore “Allah fights
against them. How perverse are they!” (9:30), because they stick to the sonship of Jesus.

Also many exhortations “to kill (or slay) the unbelievers” are found in the Qur’an (e. g. 2:191;
4:89) as well as the statement that the unbelievers “will abide in the fires of hell”.
 
Kuhusu kutumia biblia wala sishangai manake hawa jamaa washaona vitabu vya dini ni vya kuchezea, leo wanaapa kwa kutumia vitabu vitakatifu na kesho wanavunja viapo vyao!
 
Embu subirini kwanza ! Ivi bibilia haikusema hivyo ? Hapa kuna waumini wa dini ya Yesu ,mnaweza kuitetea bibilia hapo,kwani kama Makamba amenukuu sawasawa basi hakukosea ,au mnaongeaje ,amesema uongo na kuizulia bible ?
Kinachoongelewa hapa ni kwa nini asitumie kitabu anachokiamini yeye,Aache kutumia kitabu asichokiamini kwa kuhalalisha mauaji ya wana Arusha. Cha muhimu hapa ni yeye kusikitikia mali wakati kuna watu wamepoteza maisha na kuna watu wanaugulizia majeruhi hospitali.
 
Akizungumza na gazeti hii jana, Makamba alisema kitendo kilichofanywa na Chadema ni cha kinyama na kinapaswa kulaaniwa na watu wote wanaoitakia mema nchi hii "Ukisoma Biblia katika kitabu cha Warumi Sura 13, imeandikwa " Itiini Mamlaka inayowazidi nguvu; hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu," alisena Makamba na kuaongeza: "Sasa mamlaka imesema msiandamane, ninyi mnaandamana.

lakini pia nalilia mali za CCM zilizoharibiwa. Gari la katibu wangu wa Mkoa limevunja vioo na ofisi yetu imeharibiwa vibaya," alisema Makamba mwisho
Mzee hovyo kweli analilia mali s*******
 
Wakuu wapi ndugu Kinen*#...ooops sorry KINANA, maana kila chaguzi zinapokwisha naye anapotea, ina maana yeye huwa ni mtaalam wa kuchakachua akishamaliza anapotea.
 
Wakuu wapi ndugu Kinen*#...ooops sorry KINANA, maana kila chaguzi zinapokwisha naye anapotea, ina maana yeye huwa ni mtaalam wa kuchakachua akishamaliza anapotea.
Kesha maliza kazi yake, keshapokea cheque yake ya miaka mitano mpaka 2015

 
Wakuu wapi ndugu Kinen*#...ooops sorry KINANA, maana kila chaguzi zinapokwisha naye anapotea, ina maana yeye huwa ni mtaalam wa kuchakachua akishamaliza anapotea.

Yuko Somali anaendelea na harakati. Consultancies za uharamia
 
Edward Lowasa alitoa tamko la kuwaomba CCM na CHADEMA Arusha wakae kwenye meza ya mazungumzo wamalize mgogoro. Siku iliyofuata Makamba alitoa tamko kama katibu wa CCM akiongea kwa kejeli na dharau kuwa CCM haitafanya maongezi na Chadema kamwe kuhusiana na mgogoro wa Arusha. Makamba huyuhuyu leo hii anajibaraguza kulaani maanandamano ya kudai haki walioipokonya wao CCM?. Kwa kutumia akili yangu ya darasa la kwanza kutathimini mwanzo wa uchakachuaji wa uchaguzi wa nafasi ya Umeya Arusha mpaka kufikia maandamano yaliyovamiwa na dola iliyopata amri ya uonevu nakupelekea vurugu na mauaji Arusha, MAKAMBA ni chanzo cha matatizo kwa kugoma kufanya maelewano baina ya CCM na CHADEMA kutatua tatizo mapema.
MY TAKE; Huyo Makamba anaweweseka usiku wakati akiwa usingizini kutokana na roho zilizotoka na damu iliyomwagika Arusha kutokana na kauli yake na msimamo wake wa kukataa kufanya makubaliano baina ya CCM na CHADEMA. Pia huyu Makamba sidhani kama maneno anayoongea anatumia mdomo au mlango mwingine wa fahamu kwa sababu watu wamekufa, wengine wamejeruliwa sana na wengine wamepoteza mali zao ila Makamba yeye anasikitikia mali za CCM zilizoharibika. DOES HE HAS REAL TWO BALLS????
 
MAKAMBA SASA YATOSHA

Nimekuwa nikimsikiliza Mheshimiwa Yusuph Makamba katika mikutano yake mingi na waandishi au vyombo vya habari juu ya mambo mbalimbali yanayoihusu Serikali, Chama Cha Mapinduzi ambacho yeye ni Katibu wake ama Wananchi kwa ujumla. Yapo mambo mengi ambayo kimsingi sikubaliane nae; lakini kwa leo lililonikwaza na hata kunipelekea kuandika makala hii. Ni hili suala la Mheshimiwa Makamba kuichafua Biblia Takatifu, ambayo sisi wahumini wa dini ya Kikristo tunaamini kwayo.


Hivi karibuni kumetokea mtafaruku kati ya wafuasi na waamini wa chama cha CHADEMA na Jeshi la Polisi Mjini Arusha. Mtafaruku ambao umewaacha watu katika hali mbaya na wengine kupoteza maisha yao. Jambo la kushangaza Mheshimiwa Makamba kama kawaida kaanza nukuu zake kutoka katika kitabu kitakatifu "Biblia". Amenukuu Warumi 13 akasema;


"Itiini Mamlaka inayowazidi nguvu; hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu"


Kiukweli hii nukuu ndio iliyonifanya nione kuna kila sababu ya kumwambia Mheshimiwa kwamba sasa yatosha; lengo ni kuonyesha kuchoshwa kwangu na kejeli, dharau na mabezo kuhusu imani za watu wengine.

Tumekuwa tukifundishwa "Amani na Upendo" katika imani yetu siku zote. Pengine hii ndiyo iliyompa jeuri na kiburi cha kukashifu imani ya Kikristo. Kwakuwa, siku zote amekuwa akitumia Biblia vibaya na kwamba hajawahi kutokea Mkristo aliyeonyesha kuwa tabia yake inatukera sana. Labda ndiyo maana amekuwa akiendelea siku hadi siku na sasa imegeuka tabia.


Napenda kutumia nafasi hii kumwambia Mheshimiwa Makamba kwamba tabia yake ya kudharau, kuukashifu na kuubeza Ukristo sasa YATOSHA. Ninavyofahamu mimi yeye ni muumini wa dini ya Uislamu. Vilele naamini yeye kama muumini safi, asingependa kuona mtu mwingine asiye mwamini wa Uislamu anajifanya anaijua Kuruani Tukufu wakati kiukweli haijui kabisa.


Nadhani ni vyema kwa Mheshimiwa Makamba kuwaachia Wakristo Biblia yao na yeye abakie na imani yake ambayo naamini wana vitabu vyao vinavyoelezea imani yao. Mheshimiwa umeshavisoma vyote na kuvielewa vizuri?. Je! Humo hujaona nukuu za kutolea mifano ya wanasiasa? Huoni huo ni uchokozi wa imani za watu?. Nijuavyo mimi imani yako inaheshim sana vitabu vitakatifu na kwamba mtu huwezi kukurupuka na kamstari kamoja na kuwa ndio mfano wako. Soma kwa makini na roho wa Mungu akuongoze ili uelewe vizuri. Kwamaana Biblia sio sawa na vitabu vya Kifizikia, Kemia, Jiografia, Lugha nk ambavyo unaweza kuvisoma hata kama umelewa chakali. Biblia ni kitabu cha kuogopwa na kwamba unaposoma kwanza unatakiwa umwombe Mungu akuongoze usome neno gani na pengine akufungulie maana ambayo Mungu amekusudia iwafikie Wanadamu.


Jambo la kushangaza Mheshimiwa anakariri kamstari kamoja bila hata kujua maana na nini makusudio ya Mungu kuhusu maandiko hayo na kuondoka nacho kwenda kwa waandishi wa habari na kukatumia kama mfano wa malengo yake ya kisiasa. Huwezi kusema;


"Itiini mamlaka inayowazidi nguvu; hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu".


Hiyo nukuu haipo kwenye Biblia. Labda kwenye kitabu cha imani yake anayoijua yeye mwenyewe. Warumi 13:1; Maandiko Matakatifu yanasema;


"Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imeamriwa na Mungu".


Mheshimiwa, naomba nikuambie kuwa; nukuu yako na iliyopo kwenye kitabu Kitakatifu ina tofauti kubwa sana wala hazifanani kimaana. Isitoshe hukoma vizuri mpaka mwisho ili ulewe vizuri nini lilikuwa kusudio la andiko hilo. Maandiko Matakatifu yanatufundisha kuwa;


"Si kila mamlaka zinatoka kwa Mungu" zipo mamlaka zinazotoka kwa Shetani. Tofauti ya hizo mamlaka mbili ni matendo yake, "Mtazipima hizo mamlaka kama zinatoka kwa Mungu ama kwa Shetani kutokana na MATENDO YAKE".


Wana wa Israeli walipokuwa Misri kwa Mfalme Farao wakiongozwa na Musa akisaidiana na Haruni; waliupinga Utawala wa Mfalme Farao. Je! walifanya makosa kuupinga? Mbona Mungu aliwaongoza na hata kuwapigania dhidi ya udhalimu wa Mafirauni?. Kama kila mamlaka inatoka kwa Mungu iweje Musa ambaye hata imani unayoitambua na kuiamini pia inamtambua, aliupinga!. Ukisoma Luka 19; 45-46, Marko 11; 15-18.


"Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa; wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu. Akawafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala kwa Mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya pango la wanyang'anyi"


Hapo Yesu aliipinga mamlaka; Je! Alifanya makosa kufanya hivyo?. Ni sahihi kwako wezi na wanyang'anyi kuvamia na kuua lakini wasiulizwe au kuhojiwa kwa kuwa kila mamlaka inatoka kwa Mungu?.


Nakumbuka mwaka 1979; Tanzania iliingia katika vita kati yake na Taifa la Uganda wakati huo Iddi Amini Dada ni Rais wa nchi hiyo. Uganda ni mamlaka kamili; kwanini TPDF (Tanzania Peoples Defense Force) waliivamia nchi ya Uganda ambayo ni mamlaka kamili? Huoni kuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliamuru majeshi yaingie vitani?. Na wakati huo wewe mwenyewe ukiwa jeshini kwanini hukumwambia Mwl Nyerere asiipinge ile mamlaka kwa kuwa mamlaka zote zinatoka kwa Mungu?. Utawala wa Iddi Amini Dada nao ulitoka kwa Mungu?. Kagera ilivamiwa na hata kusababisha mauaji ya kutisha kwa Watanzania na mali zao; Je alitumwa na Mungu?.


Utawala wa Dikteta Adolf Hitler ambaye alisababisha mauwaji ya watu wa Jamuhuri ya Kisovieti yapata 20,000,000 na Wayahudi yapata 6,000,000. Alianzisha makambi ya kuua Wayahudi huko Sobibo na kungineko Duniani; na hata kusababisha mabomu kupigwa katika miji ya Nagasaki na Hiloshima. Utaniambia naye mamlaka yake ilitoka kwa Mungu? Ni Mungu yupi huyo anayeamuru hayo yatokee kwa wanadamu aliyowaumba yeye mwenyewe?.


Jamani naomba ya "Kaisari tumwachie Kaisari na ya Mungu; tumwachie Mungu. Wewe ni mwanasiasa ya Biblia waachie Wachungaji na wewe bakia na siasa. "Waswahili wanasema mshika mawili hukosa yote" mwisho wa siku utajikuta hufai kwenye siasa wala kwenye dini.


Mwaka 2001, Zanzibar kulitokea maandamano yaliyoongozwa na CUF, mbona hukutoa huo mfano? Au hukuwa na mfano kutoka kwenye kitabu cha imani yako. Unataka Watanzania tuelewe nini unapounganisha au kutoa mfano wa Kibiblia na Maandamano ya CHADEMA. Unaweza kuyalinganisha maandamano yaliyotokea mwaka 2001 huko Zanzibar na haya ya Arusha?. Mimi nadhani ni kampeni yako ya udini unataka watu waondoke kwenye ukweli wahamie kwenye mawazo kuwa maandamano ya Arusha yanamwelekeo wa kidini?.


Unapokuwa kiongozi ni vizuri sana kutafakari kabla hujasema; jambo ambalo naona linakosekana kwa huyu mzee wangu. Mara nyingi husema kwanza na suala la kufikiria kwake huja baadae. Kuna ushahidi wa kutosha juu ya jambo hili. Wakati umefika sasa kwa Mheshimiwa kuwa na mshauri wa karibu ambaye atakuwa anahariri kila sentensi anayotaka kusema mbele ya waandishi au vyombo vya habari.


Wakati sasa umefika kwa Wakristo kutokukaa kimya kwa mtu yeyote mwenye nia au dalili ya kuukashifu Ukristo. Anachofanya Mheshimiwa Makamba ni dharau dhidi ya Biblia Takatifu. Kama amesoma na kwamba ameona anahitaji kuwa Mkristo, ni vyema kwake akaongozwa sala ya toba ili ampokee roho mtakatifu akoke. Lakini anachofanya sasa ni uchokozi dhidi ya Ukristo. Huwezi kuisoma Biblia kwa nia ya kupata tu vifungu vya kuongelea mambo ya kisiasa na sio kujifunza neno la Mungu linataka nini. Wakristo hatuwezi kukusomea FATWA wala kuwaomba Wakristo duniani kote waandamane kupinga hilo. Ninachokuomba Mheshimiwa acha mara moja hiyo tabia. Inanikwaza sana pia naamini wengi hawaipendi isipokuwa ni usistaarabu tu tuliojaliwa na Mungu ndo maana unaona tuko kimya.


Nidhahiri kwamba Mheshimiwa umenielewa vizuri sana na kwamba hutarudia tena kusoma Biblia kwa nia ya kutafutaa kamstari kakwenda kuongelea na waandishi wa habari. Unavyoiheshimu Koruani; vivyo hivyo iheshimu Biblia Takatifu kwani nasi ndicho kitabu tunachokiamini na kufuata mafundisho yake.
 
kaaaa..... mkuu...... font size.., font type.... justify..edit ..italic..which is which....tafuta secretary,..... habari ni nzuri lakini kichwa kinaniuma... nimevaa miwani tatu kwa pamoja..... pamoja na kioo cha monitor hakuna ninachoelewa
 
Mimi nimesoma kama nusu hivi ya thread. Points zipo japo editorial errors zipo kibao. Hata hivyo, mkuu hoja nimeipata. Najua 'mzee mfyatukaji' atapata ujumbe kama siyo yeye mwenyewe moja kwa moja basi atapelekewa na mwanawe januari manake naye ni mwanaJF.
 
Back
Top Bottom