Makamba asafishwa mgogoro wa Maswa

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
Makamba asafishwa mgogoro wa Maswa

*Yadaiwa alikaririwa vibaya dhidi ya Shibuda

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa kimetoa tamko rasmi kuhusiana na mgogoro uliotokea hivi karibuni wilayani Maswa kwa madiwani wa wilaya hiyo kutuhumiwa kususia kikao cha Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wa Mkoa, Bw. Fano Mwendapole, madai ya Bw. Makamba kumtuhumu mbunge wa Maswa, Bw. John Shibuda hayakuwa ya kweli.

Bw. Mwendapole alisema Bw. Makamba alinukuliwa vibaya kumtuhumu Bw. Shibuda, kuwa alishawishi madiwani wasusie kikao cha Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, bali alichokisema na kutoa ushauri kwa viongozi wa mkoa, ni kuchukua hatua za haraka kuondoa tofauti za wana CCM zilizojionesha kuwapo Maswa.

“Ndugu wanahabari vipo vyombo vya habari ambavyo vimeripoti sakata la Maswa vikimhusisha Katibu Mkuu, kuwa anapambana na Bw. Shibuda, huo si ukweli, si rahisi apambane na mbunge anayetokana na chama chake,” alieleza Bw. Mwendapole.

Alisema, “alichokisisitiza Bw. Makamba, ni kuwataka viongozi wa Maswa kumaliza tofauti zao, mfano halisi ni pale alipotoa nafasi kwa Bw. Shibuda kama ana neno la kusema na akasema Maswa iko safi, walipoulizwa Mwenyekiti na Katibu wake wakasema Maswa kuna tatizo.”

Kutokana na majibu hayo, ndipo Bw. Makamba alipowataka viongozi wa mkoa kuhamia Maswa, jambo ambalo Halmashauri Kuu ya Mkoa pia ililiunga mkono.

Alisema CCM inaendeshwa na vikao halali kwa kutumia Katiba, kanuni na taratibu na ndilo ambalo Katibu Mkuu alikuwa akiwakumbusha katika ziara yake mkoani hapa.

“Sisi katika ngazi ya mkoa, tunasubiri uchunguzi wa umakini unaofanywa na viongozi wa wilaya, ili hatimaye walete mkoani kwa hatua zingine,” alieleza Bw. Mwendapole.

Kwa upande mwingine, alisema chama mkoa kinaamini kuwa viongozi wote wa CCM wilayani Maswa, akiwamo mbunge na madiwani, ni safi mbali na tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza.

Akizungumzia suala la kutishiwa kufukuzwa ndani ya chama kwa madiwani ambao wanatuhumiwa kutohudhuria kikao hicho, Bw. Mwendapole alisema hakuna kitu kama hicho.

“Unajua kikao chenye mamlaka ya kumvua uanachama ni mkutano mkuu wa mkoa pekee yake, hakuna kikao kingine chenye uwezo huo, hili la watu kupewa fomu kujieleza ni jambo la kawaida, na si madiwani peke yao waliopewa fomu hizo hata wajumbe wa kawaida wamepewa,” alieleza.

Alisema lengo ni kutaka kuviwezesha vikao vya kuchunguza suala hili ni nani aliyehusika ama kusababisha kikao kile kukwama, kama ambavyo taratibu za chama zinavyoelekeza.

“Koramu ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ni watu 120, waliofika ni wajumbe 40, madiwani ambao hawakufika ni 14, mtaona wazi kuna wajumbe wengine wapatao 66 ambao si madiwani, hivyo inamgusa kila mjumbe si madiwani tu,” alieleza Bw. Mwendapole.

Mgogoro huo ulitokana na Bw. Makamba kushindwa kuzungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Maswa, baada ya kutotimia kwa idadi ya wajumbe wa kikao hicho wakiwamo madiwani.

Hali hiyo ilidaiwa kusababishwa na Bw. Shibuda ambapo Bw. Makamba alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kumtuhumu mbunge huyo kuwa ndiye anayewagawa wanachama wa CCM wilayani humo.

Mbali ya tuhuma hizo dhidi ya Bw. Shibuda, madiwani waliodaiwa kutohudhuria kikao hicho, walipewa fomu na kutakiwa kujieleza kwa nini wasipewe adhabu kutokana na kitendo hicho.

Source: Majira
 
Kunukuliwa vibaya ndiyo justification za kumsafisha Katibu Mkuu ... kila siku tunawaambia huyo Katibu Mkuu ni bomu! Hayuko makini kwenye kauli zake, bado anafanya yale mambo ya ki-RC RC utadhani bado ni Rais wa Dar, yaani amri amri tu utadhani anatoa amri kwa watendaji wa kata!
 
Kunukuliwa vibaya ndiyo justification za kumsafisha Katibu Mkuu ... kila siku tunawaambia huyo Katibu Mkuu ni bomu! Hayuko makini kwenye kauli zake, bado anafanya yale mambo ya ki-RC RC utadhani bado ni Rais wa Dar, yaani amri amri tu utadhani anatoa amri kwa watendaji wa kata!

Jamani umesahau kwamba ni Luteni kanari? mambo yote ni JAMBO AFANDEEEEE Mgosi anahisi bado amevaa yale magwanda kwi kwi kwi kwi
 
Huyu hana uwezo wa kuwa hata mwenyekiti wa kijiji changu, kwani busara kwake ni sifuri.

Heri mwenye busara maana anaweza kulioka taifa ,ila ******** ataliangamiza taifa.
 
Hakunukuliwa vibaya bali ndicho alichomaanisha, kwa nini asiseme yeye kuwa amenukuliwa vibaya hadi amsemee mwendajipole? Busara hapo ni 0, Mmesahau kuhusu muafaka alitaka kuufanya nini na kauli zake. Any way wote wamebebana wasanii toka sirikalini hadi kenye SISIEM.
 
nani anafahamu CV ya makamba,nimejitahidi kuangalia katika tovuti ya bunge ila sijaipata?aukama kuna mtu amesoma naye,huyu ni mtu wa hovyo sana na naamini alikuwa kilaza sana wakati wa kusoma kwake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom