Yussuf Makamba amwinda Reginald Mengi, yeye awataja mafisadi Papa rasmi!

Huyu Mengi naye huyu....kweli idadi ya mafisadi wanaofilisi nchi haifiki 10? Halafu kwa nini kawa single out wale wenye asili ya Kihindi pamoja na Rostam? Vipi Mkapa? Vipi Chenge? Vipi Mahalu? Na wengineo wengi tu? Hivi tatizo Tanzania ni mafisadi tu? Vipi kuhusu uongozi?
 
Tupo pamoja mkuu, if anything kwa issue hii nadhani mengi yupo vitani na mwamko wa mtanzania na sio hawa so called mafisadi....hawa wakina manji, rostam na patels sio mafia kama most of us like to think..mali zao dubai, london, geneva hazijafichika kihivyo..serikali ya tanzania ni uamuzi tuu na msimamo...watanzania tuache uoga na njaa jamani..recession hii nchi nyingi zimekuwa patriotic..mwingereza hadi taxes kwa matajiri kaongeza ili kulinda uchumi..mafisadi wa kirusi wataanza kupungua sasa..sisi tupo busy kusifia watu walioshikilia uchumi wa nchi mkononi mwao...list ya kitine former usalama na aliyosema mengi hamna tofauti..ni watu hao hao.

UCHAGUZI MWAKANI TUFANYE MABADILIKO.

Unajua huyu mzee naye siyo perfect, lakini amejitoa kwa ajili ya mapenzi ya nchi yake, he didn't have to do this. Ana mahela yake, biashara zake, ana uhakika wa kula na kusaza. Sisi anaotutetea ni nani hata tusiungane naye kupambana? Unajua hata mapapa hawa wanafurahi sana, wanajua tutaongea,tutalala, kesho tukiamka kutakuwa na habari mpya nyingine. Mapovu yatatutoka kujadili habari hiyo mpya kwa jazba, nayo itapita,na wao wanaendelea kupeta. TUONYESHE MFANO. Jeeeez people !!!!!Enough already !! Don't we have those Ambulance chasing lawyers in TZ ?
 
Sadly we dont have those ambulance chasing lawyers! lawyers ambao walikuwa upinzani sasa ndo pro-ccm, wao ndo wanaofungua haya makampuni hewa tanzania na mauritius and pretending to be investors.. tusipoamka sasa tusahau kujikomboa hapa tulipo. Simjui mengi lakini i respect him more now..in my eyes it seems serikali haihusiki katika kumpatia kipato...wengi wetu kwa namna moja au nyingine kipato kinahusisha serikali..its hard to criticise those that secure ur well being..ndo maana wabunge wengi wa ccm kimya tangu mambo ya bot yaibuke.
 
Unajua huyu mzee naye siyo perfect, lakini amejitoa kwa ajili ya mapenzi ya nchi yake, he didn't have to do this. Ana mahela yake, biashara zake, ana uhakika wa kula na kusaza. Sisi anaotutetea ni nani hata tusiungane naye kupambana? Unajua hata mapapa hawa wanafurahi sana, wanajua tutaongea,tutalala, kesho tukiamka kutakuwa na habari mpya nyingine. Mapovu yatatutoka kujadili habari hiyo mpya kwa jazba, nayo itapita,na wao wanaendelea kupeta. TUONYESHE MFANO. Jeeeez people !!!!!Enough already !! Don't we have those Ambulance chasing lawyers in TZ ?

Naam, angeweza kabisa kuamua kukaa kimya huku akitafuna Utajiri wake lakini umaskini wa kukithiri anauona katika jitihada zake za kusaidia Watanzania mbali mbali wanaoishi maisha ya dhiki kubwa huku kukiwa hakuna dalili kwamba ipo siku nao watafaidi maisha waliyoahidiwa ya "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Huyu ni jasiri na jasiri kama huyu katika nchi zetu za Kiafrika au hata duniani ni nadra sana kupatikana.
 
Mwanakijiji hakuna anayejitokeza kuneutralise alichosema, bali aliyeneutralise ni yeye mwenyewe. Yeye kamsifia JK ambaye ni zao la ufisadi na pia amesifia mahakama ambazo wananchi wanakerwa nazo bado (kumbuka ule mgomo wa mahabusu wakati wa kesi ya Dito). Sasa hilo linafanya wengine tujiulize lengo la Mengi ni nini kujipendekeza au kupambana na ufisadi. Anapofanya hivyo ndiyi anafanya tukumbuke historia yake mwaka 1995 alipotishia wananchi kuwa wakichagua upinzani watauana kama Rwanda, na alikuwa akionyesha kipindi maalum cha amani. Kwa hiyo unakuta Mengi ni mtu mwenye tabia ya kujikomba ili afanikishe biashara zake. Sasa wewe kuja kumtetea hapa na kudai wengine wayaseme ni kukwepesha tu hoja. Hapa tunajadili hoja za Mengi na hao nao wakija na hoja zao tutawajadili vile vile. Hawa watu jamii ya akina Mengi ni wapotoshaji tu, umefika wakati wa uchaguzi ambapo ingestahili watu wawashauri wananchi wa kawaida wachague viongozi wazuri wao huanza kuwasifia watu fulani na kudai eti ni viongozi wasafi na waadilifu. Usanii mtupu. Wakati dili la rada linakamilishwa JK alikuwa Waziri wa Fedha, wakati akina CHavda amekula fedha za Benki akishirikiana na Idris Rashid, Kikwete alikuwa waziri, wakati IPTL inaingia JK alikuwa waziri, wakati wanachukua mapesa BoT kwenye akaunti ya EPA kwa kushirikiana na Ballali, ni JK huyo huyo ambaye alisaidiwa ili aingie ikulu, wakati Richmond JK huyo huyo alikuwa Rais aliyeubariki huo mpango. Leo anajitokeza mtu anayejitapa ni kamanda wa kupambana na ufisadi na kuanza kumsifia kwa nini tusimuone msanii??

Mkodeleaji and the Like;
Mengi ametaja mafisadi anaowajua, na sisi wote tunawajua. That is fine, he is brave and then he played his part.
Sasa wewe Mkodoleaji (na the like); mnajua wazi kuwa Mengi anawaacha wengine pembeni, kama Muungwana JK, yes, mie naamini kabisa JK is a major culprit; (and I have stated this before); Sasa ni zamu yako kusimama na kusema JK ni fisadi mkuu, you have that freedom, lakini kumkandamiza Mengi kwa kazi nzuri aliyoifanya si vizuri. Kumbuka kuwa unavyoanza kum-discourage mtu kama huyu shujaa, then you demorlarise others also. It is then your next part to take on JK; let us go one step forward instead of backward!
 
bravo Mzee Mengi.At least you dared to mention their names.Taifa la waoga haliwezi kuondokana na ufisadi.
 
kawatajia kumi yawezekana wengine wote ni wasaidizi wa hawa kumi. Maana unaweza kukuta kila atakaetajwa kama ni EL au BMW at the end of the day unakuta amekuwa linked na RA au JP n.k.
 
Sema Mengi sema Mangi....ila angalia sana sana....hao wana nguvu kubwa...wasije wakakumaliza soon...nakuombea sana
 
Mengi anasumbuliwa na Maradhi ya UGOZI na ndio maana aliowataja wote ni WEUPE, Hii ni hatari sana kwa TANZANIA yetu hasa kwa wakati huu ambao CCM imeifikisha Nchi pahala pabaya kwa kuwaweka Watanzania katika Umasikini wa Kutupwa.Kauli yake inaweza kuchochea fujo kati ya Sisi Walalahoi na wale Weupe wote Wenye Kiapato kwa Dhana tu ya Kuwa Wote ni MAFISADI.

Ukitizama kwa umakini kauli yake imeficha jambo moja kubwa nalo ni lile alilolisema Makamba kuwa Mengi anaajenda ya SIRI ya Kuimaliza CCM pamoja na KIKWETE sio Kweli kama anampenda Kikwete hampendi hata kidogo na anampiga Vita kwani likitokea lolote baya kwa kauli ya Mengi litammaliza Kikwete Kisiasa.

Hivi Mengi anamficha nani kama nae sie FISADIIIII Hii inajulikana au alishindwa nini Kumtaja MKAPA, YONA , MRAMBA, CHENGE, MARANADA IDDI SIMBA, KARAMAGI nk au kwa kuwa hawa ni WEUSI na Wengi wa Dini yake Mengiii ? au Kwao ni Kumojaaaaaaaa.

CCM Yote imejaaa uchafu uliokithiri akiwemo na yeye Mengi kama mwanachama wa CCM Hivi karibuni Mengi huyu huyu MNAFIKI alimwaga MIlioni Mia moja Kwa Umoja wa WANAWAKE CCM Kule mkowani Mbeya akijuwa kuwa ni Umoja wa Chama Cha Mafisadi sasa aeleweke nini Mzee Huyu kama sio Ndumila Kuwili wa Ufisadiiiiiiiiiiiii.
 
Mzee Mengi ana lake jambo!. Simpongezi kwa kuwataja, bado najiuliza 'the motive behind', sitaki kureach the simple conclusion kuwa kweli kuna element ya wivu, chuki na husda dhidi ya hawa jamaa yenye ubaguzi wa rangi, bali naamini its not that simple, there is something big he is up to.

Kitu ambacho namkubali Mzee Mengi ni power ya uthubutu mpaka kutaja majina. Wakati wa issue ya waziri kijana, alijiumauma tuu.

Pia siku za hivi karibuni, yeye na familia ya vyombo vyake vya habari, amejiweka karibu na wabunge machachari wa CCM Bungeni kwa kuzuru majimbo yao na kuyapa covarage kubwa ITV.
Lets wait and see as more things unfold.
 
Makamba na kiherehere chake eti cha kuwanyamazisha wazalendo in favor ya wadosi ambao anaishi kujikomba kwao...atashangaa mambo yakimgeuka maana hakuna yasiyo na mwisho...uzalendo wa watendaji wakuu uko wapi??
 
Mengi anasumbuliwa na Maradhi ya UGOZI na ndio maana aliowataja wote ni WEUPE, Hii ni hatari sana kwa TANZANIA yetu hasa kwa wakati huu ambao CCM imeifikisha Nchi pahala pabaya kwa kuwaweka Watanzania katika Umasikini wa Kutupwa.Kauli yake inaweza kuchochea fujo kati ya Sisi Walalahoi na wale Weupe wote Wenye Kiapato kwa Dhana tu ya Kuwa Wote ni MAFISADI.

Ukitizama kwa umakini kauli yake imeficha jambo moja kubwa nalo ni lile alilolisema Makamba kuwa Mengi anaajenda ya SIRI ya Kuimaliza CCM pamoja na KIKWETE sio Kweli kama anampenda Kikwete hampendi hata kidogo na anampiga Vita kwani likitokea lolote baya kwa kauli ya Mengi litammaliza Kikwete Kisiasa.

Hivi Mengi anamficha nani kama nae sie FISADIIIII Hii inajulikana au alishindwa nini Kumtaja MKAPA, YONA , MRAMBA, CHENGE, MARANADA IDDI SIMBA, KARAMAGI nk au kwa kuwa hawa ni WEUSI na Wengi wa Dini yake Mengiii ? au Kwao ni Kumojaaaaaaaa.

CCM Yote imejaaa uchafu uliokithiri akiwemo na yeye Mengi kama mwanachama wa CCM Hivi karibuni Mengi huyu huyu MNAFIKI alimwaga MIlioni Mia moja Kwa Umoja wa WANAWAKE CCM Kule mkowani Mbeya akijuwa kuwa ni Umoja wa Chama Cha Mafisadi sasa aeleweke nini Mzee Huyu kama sio Ndumila Kuwili wa Ufisadiiiiiiiiiiiii.

Labda wewe ndiyo une-clarify wazi hivi hao jamaa waliotajwa hapo ni weupi, kwa standard yako! Mie sioni hata kidogo lipo suala la rangi; hapa ni ufisadi tu; mweusi au mweupi ufisadi ni ule ule; nyie ndiyo ndumila kuwili. Hapo chini umetaja dini; lo; hapo ndipo tunachoshana kabisa. Kwa nusubongo yako umeongelea vitu ambavyo vinakutawala wewe katika hizi discussions na maamuzi, Dini na Rangi ya mtu; hapa hamna vyote viwili; bali ni Utaifa; hata hao wewe uliowataja ni WaTanzania kwa hiyo punguza hiyo jazba. Mengi kafanya hatua moja mbele labda ungeendeleza jingine hapo huwezi kum-demoralise mtu!
 
Mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi ajitoa mhanga kwa mafisadi

Boniface Meena na Mkinga Mkinga

....................................
Kati ya wafanyabiashara hao watano ambao Mengi alidai ni mapapa wa ufisadi, wamo Rostam Aziz, Yusuf Manji na Jayantkumar Chandubhai Patel (Jeetu Patel), ambao Mwananchi ilipata nafasi ya kuzungumza nao kuhusu tuhuma hizo za Mengi.

Nasubiri kuona mwanzo wa drama hii maana kweli Mengi alikuwa akizungumza kwa uhuru kabisa! Namuunga mkono.

Binafsi nimekuwa nikishindwa kuwa na imani na wafanyabiashara wa Kihindi. Imani niliyoijenga naamini niko sahihi kwamba Biashara za Wahindi nchini zimejaa ufisadi. Wana makundi ya kifisadi na kwa kiasi kikubwa wanasiasa wema wanashindwa kulisema ili wasiitwe wabaguzi.

Ninachokiona ni kwamba Wahindi wanastawi sana ki-biashara wanapokuwa ktk nchi ambazo zina viongozi laini na wenye njaa kama hii yetu na nchi zenye mifumo ya rushwa za wazi wazi. Nchi ambayo Waziri anapigiwa simu na kijana wa ki-hindi na kufunga safari kwenda kuchukuwa chochote. Aibu Tupu!!
 
Mengi anasumbuliwa na Maradhi ya UGOZI na ndio maana aliowataja wote ni WEUPE, Hii ni hatari sana kwa TANZANIA yetu hasa kwa wakati huu ambao CCM imeifikisha Nchi pahala pabaya kwa kuwaweka Watanzania katika Umasikini wa Kutupwa.Kauli yake inaweza kuchochea fujo kati ya Sisi Walalahoi na wale Weupe wote Wenye Kiapato kwa Dhana tu ya Kuwa Wote ni MAFISADI.

Ukitizama kwa umakini kauli yake imeficha jambo moja kubwa nalo ni lile alilolisema Makamba kuwa Mengi anaajenda ya SIRI ya Kuimaliza CCM pamoja na KIKWETE sio Kweli kama anampenda Kikwete hampendi hata kidogo na anampiga Vita kwani likitokea lolote baya kwa kauli ya Mengi litammaliza Kikwete Kisiasa.

Hivi Mengi anamficha nani kama nae sie FISADIIIII Hii inajulikana au alishindwa nini Kumtaja MKAPA, YONA , MRAMBA, CHENGE, MARANADA IDDI SIMBA, KARAMAGI nk au kwa kuwa hawa ni WEUSI na Wengi wa Dini yake Mengiii ? au Kwao ni Kumojaaaaaaaa.

CCM Yote imejaaa uchafu uliokithiri akiwemo na yeye Mengi kama mwanachama wa CCM Hivi karibuni Mengi huyu huyu MNAFIKI alimwaga MIlioni Mia moja Kwa Umoja wa WANAWAKE CCM Kule mkowani Mbeya akijuwa kuwa ni Umoja wa Chama Cha Mafisadi sasa aeleweke nini Mzee Huyu kama sio Ndumila Kuwili wa Ufisadiiiiiiiiiiiii.
Na Chadema walisema anaekumbatia mafisadi na yeye ni fisadi ,kutokuwataja akina Mkapa na wenziwe ambae ndio chanzo cha chemchem ya mafisadi ni woga au tunaweza kusema yupo katika kambi ya akina Mkapa na anamsifu Kikwete kwani ukitaka kumuua jibwa mpe jina zuri ndivyo wasemavyo wazungu,ukiangalia aliowataja Mengi wote ni wasaidizi wa kambi ya Kikwete na aliowaacha ni kambi ya Mkapa ,tunafahamu kuwa Kikwete si chaguo la Mkapa liliopo ni kulindana tu ,huo msaada wa feza alioutoa kwa umoja wa wanawake wa CCM inaonyesha wazi ni jinsi gani anavyoukumbatia ufisadi ,kama Mengi ameamua kuwasakama na kuwataja mafisadi basi afahamu kuwa huwezi kuwataja bila ya kumkaba Sultani mwenyewe ,kuwabana na kuwagandamiza wafuasi wachache wa Sultani CCM na kuwawacha wengine huo utakuwa ni unafiki mkubwa ambao utawalaghai wengi kama tunavyoona hapa ,baazi yetu wakionekana kuunga mkono ,kama Mengi ni mkweli katika hili basi anapaswa kuikandandia CCM nzima na serikali yake hapo tutajua yupo na wanyonge othrwise atakuwa mnafiki mkubwa kama kilivyo chama cha CCM kusema na kudai kuwa ufisadi ni private matter wakati wamewakumbatia mafisadi wanaojulikana kwa ushahidi ulio wazi ,hawajamfukuza mtu ubunge wala uanachama ,Mengi awabwekee CCM na serikali yake na sio mtu mmoja mmoja tena wa mrengo fulani tu ,kama upinzani ni lazima Chama kilichopo madarakani ndicho cha kuvutwa shati na kuzuiwa kuendelea kutawala ,kumvuta mmoja mmoja ni kuwasaliti wananchi katika kupambana na ufisadi

Huwezi kuzuia bidhaa wakati kiwanda kinachozalisha bidhaa hizo kinaendelea kufanya kazi ni lazima makelele yaendelezwe katika kukifunga kiwanda kizima na kukiweka kando kwa kuwa bidhaa zake (aka wafuasi wakuu wa Sultani CCM) ni sumu inayowamaliza WaTanzania. Mengi anaimarisha kiwanda kwa kuwajalizia mtaji wa kuendeleza utotoaji.

Nawashangaa wapinzani wanaomshangilia Mengi bila ya shaka yeyote wamekosa uyakinifu wa siasa za Mengi.
 
Kawataja kama mafisadi papa. Anasema watu wanaolisunbua taifa hili wako kumi lakini mapapa kabisa wako watano wakiwemo Rostam, Jeetu, Manji, Subash na mwingine mmoja.
Aliulizwa kama haogopi kushitakiwa? Akajibu kuwa waende mahakamani kwani mahakama zipo kutoa haki kwa watu. Akasema waende ili yote yakafichuke huko.
Amezungumzia kashfa nzito wanazohusika nazo ni pamoja na
Richmond
EPA
Dowans
Ndege ya Rais
Helkopta za jeshi
Magari ya jeshi.
 
Mengi aanika mafisadi papa

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi ameibuka na kudai nchi inahujumiwa kundi dogo la watu aliowaita 'mafisadi papa' na wamejiandaa kutoa roho za wanaowapinga kwa gharama yoyote.

Bw. Mengi alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza kuwa mafisadi hao wameifikisha nchi pabaya kwani hawataki kuguswa.

Aliwataja watu hao wakiwemo wafanyabiashara na wanasiasa (majina tunayo) na kueleza kuwa wameivuruga nchi kwa kiasi kikubwa.

"Nia njema ya Rais Jakaya Kikwete ya kupambana na mafisadi na aina zote za uovu zimewashtua mafisadi na sasa wamecharuka wanapambana na watu wote wanaomsaidia Rais kupambana nao kuwazuia wasiendelee kuitafuna nchi,"alisema Bw. Mengi.

Bw. Mengi alisema mafisadi hao wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya fedha za wananchi, na baya zaidi, yamehamisha pesa hizo nje ya nchi.

Alisema wanaotuhumiwa wanahusishwa na karibu ya kila kashfa kubwa iliyoibuka hapa nchini.

"Jitihada kubwa za Rais Kikwete kuleta maendeleo na Maisha Bora kwa kila Mtanzania zinadhoofishwa na wizi mkubwa wa rasilimali za Taifa,"alisema Bw. Mengi na kuongeza;

"Bado Watanzania wengi wanaandamwa na umasikini mkubwa, hawajui hata mlo mmoja kwa siku utatoka wapi"

Bw. Mengi ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini, alisema cha kusikitisha ni kwamba pale Mtanzania mwema mwenye uwezo anaposaidia jamii kuondokana na umaskini, mafisadi wamekuwa wakipiga kelele kuwa misaada ya aina hiyo ina agenda na kupinga kwa kutaka Watanzania wafe njaa na matatizo mengine.

"Inavyoonekana nia ya mafisadi hao sasa ni kuvuruga nchi na si ajabu wakaunga mkono matatizo yanayotokana na kampuni ya Kuvuna na Kupanda mbegu, DECI na Watanzania wakabaki wakifukuzana na wachungaji bila kujiuliza ni kina nani hasa wanachochea vurugu hizo,"alisema.

Bw. Mengi alisema DECI imeleta matatizo makubwa katika nchi mbalimbali duniani, ambapo iliiangusha Serikali ya Albania na kwamba hatma yake ikiendelea kuchochewa na watu wapenda vurugu, italeta matatizo makubwa hapa nchini.

Alisema kuwa mafisadi papa hao hawaibi rasilimali tu, bali wanaiba pia muda, badala ya wananchi kutumia muda katika shughuli za maendeleo, wanajikuta wakiutumia kupambana nao.

Bw. Mengi alidai mafisadi hao wanatumia fedha walizoiba kuanzisha magazeti ya kujenga kiburi cha kudharau Watanzania, kuwatukana na kuwanyanyasa.

"Inakuwa ni kesi ya mwizi kumkimbiza na kumpiga aliyeibiwa. Hata sasa hivi mafisadi hao wanaendelea kutumia uwezo wao wa kiuchumi uliotokana na wizi wa rasilimali za nchi kuwashawishi na kupata miradi mikubwa mikubwa kwa kutumia majina tofauti tofauti huku wakipuuza kabisa kelele za wananchi kuhusu ufisadi wao,"alisema.

Alisema Watanzania wanaolia na ufisadi ni mamilioni wakiongozwa na Rais Kikwete, lakini wachache waliojitokeza na wanajulikana kwa majina.

Alieleza kuwa hata hivyo kuna tetesi kwamba mafisadi papa wamedhamiria kuwatokomeza kabisa wapinga ufisadi wanaojulikana kwa majina.

Alisema mafisadi hao ni lazima wajue kwamba iwapo wapambanaji hao wa ufisadi watadhuriwa kwa njia yoyote, ndani au nje ya nchi, watawajibishwa na Watanzania.

Alisema mafisadi hao wanafanya kila wawezalo kuhakikisha Watanzania wanaopiga vita ufisadi, wanaangamia kwa njia mbalimbali zikwemo sumu, ajali au kwa kupigwa risasi ili kuondoa ushahidi.

"Watanzania mtasikia tu kwamba fulani amefia nje ya nchi na mtachukulia kama kitu cha kawaida kumbe mafisadi ndio waliotekeleza azma yao, ni lazima muwe macho kwani wanataka kuisambaratisha nchi,"alisema.

Aliwataka Watanzania kujiuliza mafisadi wanapata wapi ujasiri, majigambo, dharau, nguvu za kuwatukana na kuwanyanyasa ?

Alisema mafisadi wote hususani wale wanaotuhumiwa kuwa mafisadi papa ni lazima washughulikiwe, la sivyo wataiyumbisha na kuitikisa nchi na kwamba ni lazima Watanzania waone kwamba sasa nchi imefika mahali pa kusema imetosha.

Bw. Mengi alisema amejitoa muhanga kupigana vita dhidi ya mafisadi na kubainisha kuwa yeyote atakayekerwa na hatua ya kuitwa 'fisadi papa 'aende mahakamani ili wakapambane kisheria.

SOURCE; MAJIRA
 
Mpaka sasa naweza kusema mambo matatu

1.Mzee ni Mbaguzi

2.Familia imemshinda

3.Ana wivu,fitina na chuki na watu anaoshindana nao kibiashara

Haiingii akilini leo kusema mafisadi ni watu watano tu,ambao tena wamehusishwa na kesi za hivi karibuni za kifisadi.

Anogopa kuwataja watu ambao wanafahamika
kabisa kuwa wamertufiksha hapa.

Hataki kuigusa CCM na watu wake kwa kuwa anawaogopa watamaliza.

Ameweza kujenga hoja kuwa mafisadi ni wahindi tu,na tuwabague wakati hao hao wahindi wanatumia na mafisadi mama ambao wapo serikalini,wakubwa ambo mengi anawaogopa kuwasema
 
Back
Top Bottom