Yo Yo
JF-Expert Member
- May 31, 2008
- 11,217
- 1,702
kama umenisoma vema ni kwamba namuoan mengi kama msanii tu.....kila mwenye akili ya kawaida anajua kabisa hao aliowataja sio mapapa kama alivyosema papa ni JK mwenyewe na yeye anampa shavu JK kuwa yu msafi...si wajitokeze kina Rostam na Manji na wenyewe walaani yaliyotokea Benki Kuu angalau tujue wanakerwa? Mbona hadi leo Lowassa na kina Patel na kina Don Ande hawajajitokeza kusema hata jambo moja dhidi ya EPA, na wizi wa mamilioni yetu Benki Kuu?
Wote hawa wana matatizo yao, lakini kumuweka Mengi kwenye kundi la wezi wa Benki Kuu ni kukosa kuwa wakweli.
Leo hii Mkapa aliyekuwa Rais wakati wizi mkubwa unatokea nchini hadi leo hajajitokeza kulaani yaliyotokea na badala yake amejikunyata kimya! Kina Makamba badala ya kulaani yaliyotokea wanataka kina Mengi wanyamaze! Kina Kaboyonga badala ya kulaani wizi wa fedha zetu wanataka kina Slaa wanyamazishwe! tukisema tumelaaniwa au tumerogwa watu wanasema tunajitukana!
Sasa hapa wanajitokeza wengine kujaribu kuneutralize alichosema Mengi ili tusipime madai dhidi ya wezi wa utajiri wetu! Kama kina Manji, Patel, Rostam na wenzao wanaona wameonewa na kuwa wanasingiziwa waende mahakamani! Kama wanashindwa basi na wao angalau wajitokeze na kulaani ufisadi nchini! Hawawezi; ufalme hauwezi ukajipinga wenyewe halafu ukasimama!
Kama na wenyewe wanajua Mengi ana mambo yake ya kifisadi wajitokeze basi wayaseme na kuonekana ni watetezi wa taifa basi..