Makamba amshtaki Halima Mdee kwa Spika Sitta

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Katibu Mkuu wa CCM, Makamba ameshtaki Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Halima Mdee kwa kumtuhumu kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi. Bwana Makamba amewasilisha malalamiko hayo akirejea mchango wa Mbunge huyo alioutoa bungeni. Maelezo zaidi yatafuata

PM
 
Ndio hayo tu ndio uliyotaka tufahamu mzee? Mbona taarifa imekaa kama udaku maana hajibu maswali mengi. Mi umeniacha mzee, nadhani ulikuwa huna haraka ungesubiri taarifa hiyo ikamilike ndio ulete hapa tujadili. Sasa hapo tukianza kujadili tutaambiwa waosha vinywa kumbe taarifa yenyewe inatengeneza mazingira hayo.
 
- Hii kesi ni kweli ipo tena siku nyingi sana na nimeisema mapema sana kuhusu uwepo wake, nijuavyo ni kwamba Makamba alilalamika kwa Spika kwa kumuandikia kijibarua hivi, lakini Spika akaikataa hii kesi na kumpa mwenyekiti wa kamati ya maadili ya bunge, na imeanza rasmi tarehe 13, na jana pia ilifanyika na inaendelea, leo niliongea na mjumbe mmoja aliyeko ndani ya hii kesi akaniambia kuwa bado haijashika moto, ndio kwanza imeanza tu!

- Kwa hiyo tuko karibu nayo!
 
;)Tehe he!

Pole sana Makamba!;)

Na mie nakumbuka wakati namshitaki dogo moja hivi nikaambiwa "Wacha hizo, wivu gani huo"

Lakini wacha tuone jinsi hii itakavyogeuka!

Kwa Halima, mie niliambiwa nikaze buti humu--Kaza moyo Makamba naye anawajua watu kama hao:D
 
Katibu Mkuu wa CCM, Makamba ameshtaki Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Halima Mdee kwa kumtuhumu kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi. Bwana Makamba amewasilisha malalamiko hayo akirejea mchango wa Mbunge huyo alioutoa bungeni. Maelezo zaidi yatafuata

PM

Baba na mwana tunaimba nakucheza....
 
This is interesting!! Doesn't Makamba have better things to do?? Halima mdogo kaza buti, make sure una data za kutosha za kumtoa mzee mzima makamasi............. hivi Halima Mdee si alisoma na watoto wake Makamba UDSM? I think it was at around the same time. So his kids must know her well.

Nasikia kucheka kweli................
 
Katibu Mkuu wa CCM, Makamba ameshtaki Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Halima Mdee kwa kumtuhumu kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi. Bwana Makamba amewasilisha malalamiko hayo akirejea mchango wa Mbunge huyo alioutoa bungeni. Maelezo zaidi yatafuata

PM

Sijui mantiki ya kesi kama hiyo. Maana kikatiba, hairuhusiwi kufanya mashitaka kwa lolote litakalosemwa na Mbunge katika vikao vya Bunge. Labda kama Halima Mdee alitoa shutuma hizo nje ya Bunge
 
Hata ndani ya Bunge na Makamba na Londa ndio waliolalamika kama alivyolalamika Mengi kwamba Mdee kawasingizia, na baada ya Makamba na Londa kuandika maelezo yao na ushahidi yaliyofanana sana kwa kila kitu kasoro majina yao, Mdee akaitwa na akamwaga radhi kwa kutoa ushahidi wa ajabu ambao sasa umekuwa moto kwa kina Makamba na Londa na Muungwana amewaambia hilo ni lao walimalize wenyewe. Soon yatakuwa public
 
aisee! uovu unamwisho. Mtu afanye kosa halafu utake kujisafisha kwa kudhani hakuna ushahidi.
 
Hata ndani ya Bunge na Makamba na Londa ndio waliolalamika kama alivyolalamika Mengi kwamba Mdee kawasingizia, na baada ya Makamba na Londa kuandika maelezo yao na ushahidi yaliyofanana sana kwa kila kitu kasoro majina yao, Mdee akaitwa na akamwaga radhi kwa kutoa ushahidi wa ajabu ambao sasa umekuwa moto kwa kina Makamba na Londa na Muungwana amewaambia hilo ni lao walimalize wenyewe. Soon yatakuwa public

Safi sana Mdee kaza buti mwana mama...
Makamba huyo anataka kujiumbua mbona huwa anaropoka mara nyingi tuu kuwatetea mafisadi? tena hata vyombo vya habari hususani magazeti huwa wanaandika sana pumba zake? achilia mbali alipo kuwa anamponda Dr. Slaa alipo leta hoja za wizi wa EPA akiwa tetea mafisadi hao hao. Natamani kibao kiwageukie kwa nguvu zote na Mdee tumia sheria kuwafunza adabu hao watu wanao dhani vyeo ni rungu la kukandamiza waliopo chini yao!
 
Hata ndani ya Bunge na Makamba na Londa ndio waliolalamika kama alivyolalamika Mengi kwamba Mdee kawasingizia, na baada ya Makamba na Londa kuandika maelezo yao na ushahidi yaliyofanana sana kwa kila kitu kasoro majina yao, Mdee akaitwa na akamwaga radhi kwa kutoa ushahidi wa ajabu ambao sasa umekuwa moto kwa kina Makamba na Londa na Muungwana amewaambia hilo ni lao walimalize wenyewe. Soon yatakuwa public

Mkuu, kama unao huo ushahidi usiukawizem ebu tumwagie na sie
 
aliomba mjadala wa EPA ufungwe... huko si ndio kutetea mafisadi?
 
Nadhani Mdee alikosea kidogo, sio kweli kwamba Makamba anatetea mafisadi bali ni FISADI MKUU anayeongoza chama Chenye mafisadi kilichoingia madarakani kwa nguvu ya Mafisadi
 
LONDA ,baada ya Halima kuwasilisha ushahidi mpana na wenye vielelezo aliomba kutoka nje ila Mwenyekiti wa Kamati ambaye ni Mama Kilango alimzuia , ila nyaraka zilizopo ni nyingi sana na zitawekwa hapa JF soon kwa ajili ya wadau kuweza kujionea ufisadi wa kutisha manispaa ya kinondonoi na jinsi Makamba, Londa na Manji walivyohusika kwenye wizi wa kutisha.

Niwadokezee kidogo tuu ni kuwa Manji9 baada ya kumwaga noti za kutosha kwa Londa na zikaenda kuchukuliwa na Diwani mmoja wa viti maalumu ambaye aliambulia kiasi cha shilingi 2 milioni na kuamua kwenda Marekani .

Londa akishirikiana na Makamba ndio walimuuzia Manji CocoBeach..... na madudu mengine mengi ya kutisha .

Ntawawekea full nondo kwa kina .
 
Back
Top Bottom