Elections 2010 Makamba akiri Dr Slaa ni tishio kwa Kikwete na CCM

CCM sasa inapumua kwa nguvu ya vyombo vya dola tu -- pasipo hivyo ni kwishnei. Itafika mahala hata hivyo vyombo vya dola vitashindwa kukisanifu chama hicho. Mfano wa huyo DC ni onyesho tosha la kushindwa kwa Takukuru kuisanifu CCM.

Hawakuwa wajinga kuweka usalama wa taifa, jeshi, polisi na takukuru mikononi mwao, hizo ndio last line of defence. Wamefikia hapo ndio wako hapo, sasa itafikia siku wananchi watasema tunataka vyombo vyetu vya usalama. That will be it.
 
Mfamaji haachi kutapatapa hivyo ccm mwisho umekaribia haitaacha kusema hii na lile kujifariji,wanajua kabisa CHADEMAni tishio kwani hata Mrema enzi zake alishinda kwa rekodi nzuri kuliko Kikwete ila kwa wizi na mbinu za CCM ikiwemo rushwa wakabatilisha matokeo.
 
"Dk. Slaa si tishio kwa CCM ila ni tishio kwa mtu binafsi…hawezi kuwa tishio kwa chama. Nani alikuwa maarufu kama Mrema. "Santuri mpya ikitoka itachezwa katika nyumba mbalimbali lakini baada ya muda watarudia ya zamani," alisema Makamba.

Dk. Slaa ni moto wa mabua ambao huzimika baada ya dakika tano kama alivyozimika Mrema. Mtu ambaye tunamuogopa…tunayeweza kusema kuwa ni tishio ni Lipumba, maana yeye alikuwa wa pili katika uchaguzi uliopita," alisema Makamba.

Wadadisi wa mambo wanaelezea hatua ya Makamba kulazimika kumuweka Lipumba juu ya Dk. Slaa, hasa wakati huu ambapo mgombea huyo wa CHADEMA anaonyesha dalili za kuungwa mkono, ni jitihada tu za chama hicho kujaribu kumshambulia yule wanayemhofia kuwa na nguvu zaidi katika kipindi hiki.

Kitakachokuja kumpiga miti Slaa na wana-Chadema ni poor timing ya kumtangaza. Sasa hivi makundi yote yanayokwenda kwenye hizo mihadhara hawana hata kadi za kupigia kura. Iwapo angejitangza mapema, wakati ule wa ku-renew/re-register watu kibao wangechangamkia. Lakini kwa kuwa wengi walijua wimbo ni ule ule, kama ilivyo kawaida ya miaka ya nyuma, hawakusumbuka kujiandikisha.

Makamba is right. Yale makundi ya Mrema miaka ile, hakuna aliyetegemea matokeo yake October ile. I won't be surprised, and, in fact I am expecting,, a massive win for CCM this October.
 
Kitakachokuja kumpiga miti Slaa na wana-Chadema ni poor timing ya kumtangaza. Sasa hivi makundi yote yanayokwenda kwenye hizo mihadhara hawana hata kadi za kupigia kura. Iwapo angejitangza mapema, wakati ule wa ku-renew/re-register watu kibao wangechangamkia. Lakini kwa kuwa wengi walijua wimbo ni ule ule, kama ilivyo kawaida ya miaka ya nyuma, hawakusumbuka kujiandikisha.

Makamba is right. Yale makundi ya Mrema miaka ile, hakuna aliyetegemea matokeo yake October ile. I won't be surprised, and, in fact I am expecting,, a massive win for CCM this October.
Tumia lugha za heshima kwa watu wazima kanyaboya mkubwa we kwenu hakuna wazee nyambafu. Usirudie tena uozo kama huo nitakula na wewe sambamba kama MS nyani kasoro.
 
Ningependa Dr Slaa mwenyewe ndiyo angemjibu Makamba namna hii. Lakini naamini kabisa kama kuna mdahalo kati ya Dr Slaa na YM, basi YM atapata tumbo la kuharisha kabla ya kuanza. YM ni mwanasiasa uchwara tu, anakweza kwa kujikombakomba tu kwa walio juu yake -- hana lolote!!!!!!!!!!!

Sio busara Dr. Slaa kumjibu Makamba kwa sababu hakuna jambo la kujibu hapo. Pia kwa kumjibu Makamba, Dr Slaa atakuwa amemkweza sana huyu mzee wa watu ambaye hana jipya zaidi ya kuwa mpiga debe wa viongozi wenzake wa CCM.
 
Lumbe umenena, mwenye CV ya makamba atujuze jama, huyu mtu keshaanza kuongea sana. Na huyo mtangazaji wa TBC pia atujuze kuhusu hyo mtu kwani TBC is a public facility not for CCM.
 
Muungeni mkono Dkt. Slaa-Marando


PostDateIcon.png
Tuesday, 03 August 2010 05:52

Na Tumaini Makene
marando%20kuhutubia.jpg

MMOJA wa wanasiasa maarufu na waanzilishi wa siasa za mageuzi za vyama vingi nchini, Bw. Mabere Marando amewataka wanasiasa waandamizi wa vyama vingine kuwa wazalendo na kumuunga mkono mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa.
Bw. Marando aliyasema hayo jana Mjini Dodoma katika Viwanja vya Barafu ukiwa ni mfululizo wa mikutano ya mgombea huyo kutafuta sahihi za Watanzania nchini kote kumdhamini ili aweze kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano.

Bw. Marando ambaye kabla ya kujiunga na CHADEMA hivi karibuni aliwahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi na mmoja wa wabunge wa mwanzo katika Bunge la Nchi za Afrika Mashariki, alisema kuwa wanasiasa hao wanapaswa kuunganisha nguvu zao na kutumia ushawishi wao kumuunga mkono Dkt. Slaa.
"Wengi wa wanasiasa hao wengi wao wamekwisha kugombea urais mara kadhaa, wamegombea wakati wa Mkapa wakashindwa, wamegombea wakati wa Kikwete wameshindwa.
"Namwomba Profesa Lipumba...nawaomba akina Cheyo na wengine wote ambao ni maarufu waunganishe nguvu zao kumuunga mkono Dkt. Slaa, mimi kwa dhati kabisa baada ya kuona, Dkt. Slaa ameteuliwa kuwania urais niliamua kujiunga na CHADEMA ili nitumie uzoefu wangu na nguvu zangu kumnadi kwa Watanzania," alisema Bw. Marando.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA , Bw. Freeman Mbowe alisema kuwa viongozi wa serikali na CCM wameshindwa kutambua vipaumbele vya Watanzania, badala ya kuwaondolea umaskini, wanatanguliza mbele masuala yasiyokuwa ya msingi wala faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
"Kwa akili za viongozi wa serikali na CCM, kwa akili ya Rais Kikwete, akina Makamba, Chiligati wameona kuwa kuweka picha za Rais Kikwete kila baada ya hatua tano ndiyo kipaumbele kwa wakazi wa Dodoma na ninyi mmekubali.
"Kuna mambo yanafanyika nchi hii, wanafanyiwa Watanzania ingekuwa katika nchi nyingine ambako wanaume na wanawake sio waoga, wamejaa ujasiri, watu wangeshinda na kukesha wakiandama barabarani," alisema Bw. Mbowe.
Mapema akizungumza na wananchi wa Singida katika Uwanja wa Ipembe, waliofika kumdhamini, kabla ya kwenda Dodoma, Dkt. Slaa aliwaambia wafanyabishara wa mji huo kutotishwa na baadhi ya wakuu wa wilaya wanaowalazimisha kuchangia kampeni
ya mgombea wa CCM Rais Jakaya Kikwete.
"Tunazo taarifa za Mkuu wa Wilaya Paschal Mabiti kuwaita wafanyabiashara na kuwatisha akitaka mchangie kampeni za Kikwete tena mnatajiwa na viwango vya kutoa, bahati mbaya mkutano huo ulivunjika baada ya kuingia Tundu Lissu," alisema Dkt. Slaa.
Leo Dkt. Slaa ataendelea kusaka sahihi za Watanzania kudhamini fomu yake ya kugombea urais kupitia CHADEMA katika Mikoa ya Iringa na Mbeya.

 
Dk. Slaa ni moto wa mabua ambao huzimika baada ya dakika tano kama alivyozimika Mrema. Mtu ambaye tunamuogopa…tunayeweza kusema kuwa ni tishio ni Lipumba, maana yeye alikuwa wa pili katika uchaguzi uliopita," alisema Makamba.

everything that u contribute has a religious bias in it....! i feel sorry for u..! gud enuf pipo knw u nw..!

kuwa wa pili last time does not guarantee u anything..!
 
kanyafu nkanwa huna akili kabisa wewe unamtukana mtu mzima kama dr slaa. Ambaye ni sawa na baba yako huna adabu kabisa wewe ushindwe!
 
Back
Top Bottom