Dk. Slaa ni moto wa mabua ambao huzimika baada ya dakika tano kama alivyozimika Mrema. Mtu ambaye tunamuogopa tunayeweza kusema kuwa ni tishio ni Lipumba, maana yeye alikuwa wa pili katika uchaguzi uliopita, alisema Makamba.
Makamba siyo mtu wa kumnukuu kwa vile amejaa wivu na chuki,yeye tangu azaliwe hajawahi kupata nafasi yoyote kwa kuchaguliwa na watu , yeye siku zote amekuwa akipata nafasi za kuteuliwa na wakubwa kwa vile ni bingwa wa kuwalamba miguu wakubwa, hivyo akiona mtu anayependwa na watu roho inamuuma sana. Hivi kumlinganisha Makamba na Dr Slaa ni sawa na kulinganisha panya buku na tembo,YM yuko chini saaaana, ndiyo maana matamshi yake ni ya kijiweni tu.
Huyo mzee hana strategy zozote, mmesahau wakati wa uchaguzi mdogo tarime? Aligaragazwa kisiasa.
Ningependa Dr Slaa mwenyewe ndiyo angemjibu Makamba namna hii. Lakini naamini kabisa kama kuna mdahalo kati ya Dr Slaa na YM, basi YM atapata tumbo la kuharisha kabla ya kuanza. YM ni mwanasiasa uchwara tu, anakweza kwa kujikombakomba tu kwa walio juu yake -- hana lolote!!!!!!!!!!!
Makamba kazungumza haya makusudi akijua anakianzisha baina ya CUF na Chadema kwa kuwaweka ulingoni Dr.Slaa na Lipumba. This is stage one ya CCM siku zote ni kugombanisha Upinzani..Dk. Slaa ni moto wa mabua ambao huzimika baada ya dakika tano kama alivyozimika Mrema. Mtu ambaye tunamuogopa tunayeweza kusema kuwa ni tishio ni Lipumba, maana yeye alikuwa wa pili katika uchaguzi uliopita, alisema Makamba.
Huyo mtu binafsi anayetishiwa na Slaa ni nani?
MAKAMBA = CHEMICAL ALI a.k.a vuvuzela
"Dk. Slaa si tishio kwa CCM ila ni tishio kwa mtu binafsi…hawezi kuwa tishio kwa chama. Nani alikuwa maarufu kama Mrema. "Santuri mpya ikitoka itachezwa katika nyumba mbalimbali lakini baada ya muda watarudia ya zamani," alisema Makamba.
Dk. Slaa ni moto wa mabua ambao huzimika baada ya dakika tano kama alivyozimika Mrema. Mtu ambaye tunamuogopa…tunayeweza kusema kuwa ni tishio ni Lipumba, maana yeye alikuwa wa pili katika uchaguzi uliopita," alisema Makamba.
Wadadisi wa mambo wanaelezea hatua ya Makamba kulazimika kumuweka Lipumba juu ya Dk. Slaa, hasa wakati huu ambapo mgombea huyo wa CHADEMA anaonyesha dalili za kuungwa mkono, ni jitihada tu za chama hicho kujaribu kumshambulia yule wanayemhofia kuwa na nguvu zaidi katika kipindi hiki.