Makamba afiwa na mtoto

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,009
Makamba afiwa na mtoto
Mwandishi Wetu
Daily News; Sunday,October 26, 2008 @00:03

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, amefiwa na mtoto wake wa kiume, Kimweri Yussuf Makamba. Taarifa ya Ofisi ya Makao Makuu ya CCM Dodoma jana kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa kutokana na msiba huo, Makamba aliondoka Dodoma jana mchana kwenda kijijini Mahezangulu wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga kwa ajili ya taratibu za maziko.

“Kwa mujibu wa maelezo ya Mheshimiwa Makamba, mtoto wake huyo amefariki ghafla jana asubuhi huko kijijini kwake Mahezangulu Lushoto mkoani Tanga,” ilisema taarifa ya CCM. Kuhusu mazishi, taarifa hiyo ilisema yanatarajiwa kufanyika leo alasiri Bumbuli, Tamota, Lushoto.
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN na pia awape nguvu na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao.
 
Mungu amlaze mahali pema peponi , tunakuomba pia uwafariji wafiwa,kwa kuwa wewe bwana ulitoa na umetwaa, jina lako lihimidiwe amina
 
poleni sana wazazi wa marehemu pamoja na ndugu na jamaa wa marehemu. nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape nguvu na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu na aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
Poleni sana familia nzima ya Mzee Makamba kwa msiba huu; Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi amina.
 
Poleni kwa msiba huu mkubwa familia na Bwana Makamba, ni kazi ya wbana na awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki
 
Pole Mzee Makamba pole January Makamba, Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi marehemu
 
Poleni sana familia ya mzee Makamba,kazi ya bwana haina makosa.Nawaombeeni mpate faraja ya Mungu.
 
Poleni sana wanafamilia na watanzania wote kwa ujumla kwa kupoteza nguvu kazi.
 
Mungu amlaze mahali pema peponi Amen.
Pole kwa Katibu mkuu wa ccm na wana ccm kwa ujumla bila kusahahu ndugu, Jamaa na marafiki popote pale walipo.
 
Poleni sana Mzee Makamba na familia yako
Poleni sasa wana CCM popote pale mlipo
RIP Kimweri
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiewe. Amen
 
Back
Top Bottom