Makamanda wa CHADEMA ndani ya Songea mda huu

Daa Sugu amefunika watu 1020 Mara mbili ya idadi iliyopendekezwa.Safi sana


big up
vipi mahudhurio ya watu huko hapa Mby tumemaliza kwa swaga la nguvu

  • watu waliojioresha ni 1020 kwa mjibu wa Sugu
  • Tumechangia ujenzi wa ofisi /ununuzi wa gari la matanangazo
  • vipi huko mbali na elimu nini cha ziada kilichofanyika ??
 
Wakuu ilikuwa leo makamanda wa CDM (R.mtema na katibu wa cdm jimbo la kawe) wafanye mkutano mkubwa hapa Songea mjini ila Mvua kubwa imenyesha na ndio imeacha mda huu sasa bado atujajua kama mkutano utaendelea ama la!ila watu wameanza kurudi tena hapa viwanjani baada ya mvua kukata.Nitawajulisha kile kinachoendelea.
 
Atimae mkutano unafanyika watu wengi utafikili akukua na mvua kwa sasa anaongea katibu wa kawe
 
Katibu wa kawe
1.kikwete hana msimamo
2.wananchi mngejua umuhimu wa kura msingekua mnachagua viongozi wa bovu
3.Ruvuma mnalima mahindi ila mpaka leo serikali imechukua mahindi yenu na amjalipwa mpaka sasa
4.kina mama muwe makini huyu jamaa anaweza saini ucamerun na mjue hali za wame zenu ziko atalini
 
Katibu kawe
1.Mmechagua jembe na nyundo sasa jembe limewashinda na nyundo inawapiga kichwani
2.malikia alikuja kutoa mahali sasa mngoje kameruni aje kuanza kazi maana mahali ishalipwa
3.mkisimama kiukweli mahindi yenu yatalipwa,meya ambae kawekwa na mchimbi nae mtamuondoa
4.kipyenga cha maandamano kikipigwa jitokezeni msiogope
Sasa anapanda R.mtema
 
R.mtema
1.nashukuru cdm pamoja na ulemavu wangu ila hawajanitenga na sasa tunakwenda pamoja
2.nguvu ya umma ikiamua amna kinachoshindikana
 
R.mtema
1.tunakwenda kushangilia miaka 50 uku walimu,polisi mishahara duni na ailipwi kwa wakati
2.katibu wa bunge wabunge posho hazijaongezeka spika kweli zimeongezeka
3.hamjalipwa fedha za mahindi yenu ila pesa za sherehe za miaka 50 zipo
4.elimu vijana wa sasa waulize kuhusu man u watakupa story vzuri waulize mambo ya maana hamna kitu tatizo ni mfumo wa elimu ila bado tunasema tumethubutu na tumeweza
 
R.mtema
1.serikali imefilisika kifikra na ndio maana ata camerun akaona atuingie na walijua sisi rahisi kama amuamini mpaka leo rais ajatoa kauli
 
R.mtema
1.issue ya katiba mpya haikuwepo kwenye sela za ccm
Wakuu picha nitawatumia badae kwa sasa najaribu kuandika yale yanayo ongelewa hapa
 
R.mtema
1.mswada wa sheria kua na lugha mbili ni kuwachanganya wananchi
2.mpaka mswada unapitishwa wananchi amna wanachokielewa maana waliobaki buungeni waliacha kujadili mswada na badala yake wakawa wanajadili cdm
3.ni eli kufa tukiwa tunatetea haki kuliko kufa kwa udhalimu
4.ata mkitufunga wote bado watatokea kina Slaa,Lema na mbowe wengine
5.Rais aliomba wapige picha kabla ya kikao cha ikulu alafu akawachekesha makusudi ili wapate picha ya namna hiyo kisha baada ya masaa machache issue ikawa hewani cdm wafurahia ikulu
 
Makamanda wetu CHADEMA, waache hao wengine huko waendelee 'KUDHARAU MWIBA' juu ya sheria ya uundwaji wa Katiba ya nchi kwa njia ya kumhodhisha Rais Kikwete madaraka sio yake, mambo kujipa kabla ya hawa watemi wa dharau na mzaha kushtukia 'miguu yao kuota matende' juu ya mpango mzima wanaokimbizana nao kwenye vikorido vya kule Magogoni hivi sasa.

Maslahi ya Umma mbeeele kama tai ili MAFISADI wote nchini waje wausikie vema utamu wa KUDIRIKI KUMPOKONYA MWANANCHI MADARAKA YAKE HALALI KI-KATIBA KUJITUNGIA KATIBA AKIWA USHUKANI.
 
R.mtema
1.katiba ikiwa mbovu mnakuwa na mahakama mbovu,bunge bovu na ndio maana leo hii viongozi wa serikali wamekua miungu watu.
2.leo hii mnamchagua mbunge ila kesho anapita kwenye gari vioo juu
3.mbunge anaenda bungeni mpaka bunge linaisha mbunge hajawai kuongea chochote wakati magari yetu na vitu vingine tunavipata kwa kodi zenu
4.kenya katiba yao mbunge ukichaguliwa ukazingua wananchi wanakung'oa sio mpaka umalize mda wako
5.watu wanang'ang'ania R.mtema aendelee kuhutubia ata kama mda umeisha.
Ya amekubali kuongeza mda kidogo ingawa kibali nadhani kilikua kimeisha mda ni kutokana na kucheleweshwa na mvua
 
R.mtema
Bunge la katiba muundo wake ccm na mkewe cuf watakua na nguvu maana wajumbe wao watakua wengi ndio maana cdm tunataka wananchi ndio waamue
 
Wakuu mkutano umeisha kwa R.mtema kuwaambia polisi nao wakunje ngumi kusema pipoz pawa.kisha akasema najua kazi inawabana ila mioyoni mwenu mmekunja ngumi kubwa kuliko ata izi zetu maana sisi wote tumepigika
 
CHADEMA Mi nimesaini kufa kwa ajili yenu, njia ninayoiona kukomboa nchi ndo hiyo, CHADEMA endelea si tuko bega kwa bega nanyi wala hatuko nyuma yenu kama wa mombasa! Tufike mahali tuanze kwenda kwa kasi make nchi imeporwa yote. Si mlimuona Bushi naye anakuja kumalizia kabisa kilicho baki?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom