Makamanda wa CHADEMA ndani ya Songea mda huu

wanafundisha kwani wao ni walimu?basi wafungue shule kabisa tujue moja.

Una akili timamu kweli??au unafikiria kwa kutumia masaburi??nimekujibu ila watu kama wewe huwa siwajibu,maana unaonekana hata unachoongea hujui nini unaongea....
 
Wakuu hii mutu ya kawe ni kichwa aise yani inaichambua hii sheria ya katiba mpaka basi.
Wananchi ni wengi na wamekua watulivu ingawa joto balaa nadhani mda si mrefu tutaingia katika maswali
 
Katibu wa kawe
Propaganda za Ikulu
Waandishi wababaishaji walitumika ili kupiga picha wakati cdm wako ikulu wakinywa juice na rais kisha wende kusema chadema imenunuliwa na ndio maana kesho yake walipo enda cdm wakawa wameto taadhari juu ya ilo na jamaa wakajua wameshastukiwa ikabidi wapotezee
 
R.mtema
1.Mandela aliwekwa gerezani ila alitoka na nchi yake ikawa huru kwaiyo atakama watazuia na iyo sheria yao cdm wao watajadili na wako tayari ata kufungwa ila awatokaa kimya katika hili.naametoa kidogo issue ya Lema kukaandani
 
R.mtema
Lema alipokua ndani kakutana na kijana aliye fungwa kwakua alikua na mahusiano na mtoto wa waziri fulani kijana yupo ndani akiwa hana haitia.lema kuwa ndani kajifunza na kuona mengi
 
Maswali
1.watu wengi wanatoa ushauri semina hizi zifike wilaya zote na kata zake ikiwezekana
2.wananchi wanasema sasa wemeelew kwa nini cdm walitoka bungeni na ivyo wanawapongeza kwa ilo
3.wananchi wanapendekeza cdm wajipange maana ccm wameanza kutumia vyombo vya habari kupotosha wananchi wenye uelewa mdogo
 
Maswali
1.mjumbe anapendekeza kila mkoa uunde kamati ndogo ili kuendesha semina kama hizi kwa kila kata na vitongoji vyake
2.cdm mmejipanga vp kuwapunguzia woga wananchi?
3.cdm mmejipanga vp kwa wananchi watakao tiwa gerezani katika harakati hizi?
 
Maswali
1.cdm kama ccm wakatumia wingi wao bungeni kupitisha hii kitu ni atua gani zitafuata?
2.wengi wanapongeza na kuomba cdm ijikite kwenye kuwajaza watu ujusiri
 
Maswali
1.Katiba ya sasa inatoa uhuru watu kutoa mawazo yao sasa hii sheria inayosema watakaokutwa wakijadili watachukuliwa atua ili inakuaje?
 
Cdm inapaswa kuunda serikali maana imezingatia taaluma za watu katika kuwapa uwaziri vivuli wakati ccm imezingatia uswaiba katika kuteuwa mawaziri wake
 
.maswali
Cdm ikatokea mmepewa nchi na msipo iongoza katika haki mmejiwekea utaratibu kani kujiwajibisha?
 
Maswali
1.kweli huu ni mda wa ukombozi kuna bibi umri umeenda vibaya mno anasema songea mjini cdm mnajulikana sasa nendeni vijijini
 
Maswali
1.kwanini cdm msishirikiane na vyama vingine vya kijamii vinavyoonesha kutaka mabadiliko ili kuongeza nguvu?
 
Maswali.
1.kuna mzee anasema cdm walipotoka bungeni na yeye aliamua kutoka pale alipokua akitizama bunge
 
Safi sana, naona mambo yanaenda kama ilivyopangwa!! hatuna haja hata kusherehekea miaka 50 ya uhuru wakati bado hatuna cha kujivunia! Kila kona ukifika unaulizwa, Tanzania mnajulikana kwa lipi? Unaanza Ooooh, do you mount Kilimanjaro, serengeti? Ukitaja hivyo ambavyo ni natural, kwisha unabaki kusema unaijua kenya! tunapakana nayo.
 
Majibu
1.kama watayapitisha hayo basi cdm tutaandamana kwiyo kwa sasa tunatumia diplomasia ila ikishindikana tutaandamana
R.mtema
Mimi ni mkatoriki ila kusema maandamano sio suluhisho la haya kwaili siungani kabisa na viongozi wangu wa dini walioanza kutumiwa na ccm
 
R.mtema
Majibu
1.kuhusu kuzunguka na kuunda kamati ndogo zizunguke kata,wilaya ilo watapeleka makao makuu lijadiliwe maana kwa sasa wameambiwa wasitoe tamko lolote
 
R.mtema
Majibu
1.kuhusu muungano Cdm msimamo wao ni kuunda serikali tatu
 
Majibu
1.kama watayapitisha hayo basi cdm tutaandamana kwiyo kwa sasa tunatumia diplomasia ila ikishindikana tutaandamana
R.mtema
Mimi ni mkatoriki ila kusema maandamano sio suluhisho la haya kwaili siungani kabisa na viongozi wangu wa dini walioanza kutumiwa na ccm



Aisee, huko siko kwa kwenda. Hawa Maaskofu wana nguvu mno, Chadema isipotoke na kufikiri inaweza ikapambana nao. Kama CCM inawatumia, basi nao pia wawatumie.
 
R.mtema
Majibu
1.kama cdm kwa sasa tunaendelea kutoa elimu juu ya mswada huu wa sherilia ila apo badae watajitahidi kuakikisha kila mwananchi awe na katiba ata kama ni copy
 
Back
Top Bottom