Makalio na Mapaja Makubwa ni Bora Kwa Afya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
<table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;"></td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
3917698.jpg

</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top">
Wanawake wenye makalio makubwa na mapaja makubwa kama vile Beyonce na Jeniffer Lopez wana uwezekano mdogo sana wa kupata magonjwa ya moyo na kisukari kulinganisha na wanawake wenye makalio madogo, matokeo ya utafiti wa wanasayansi nchini Uingereza umeonyesha.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Wanasayansi wa nchini Uingereza waliofanya utafiti wao katika chuo kikuu cha Oxford University wamegundua kuwa makalio makubwa yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko matumbo makubwa (vitambi).

Utafiti umeonyesha kuwa makalio na mapaja makubwa huhifadhi mafuta ambayo husaidia mwili kujilinda na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.

"Mafuta ya kwenye makalio na mapaja ni bora kwa afya lakini mafuta mengi ya kwenye tumbo si mazuri kiafya", alisema Dr Konstantinos Manolopoulos, mmoja wa watafiti watatu walioshiriki kwenye utafiti huo ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la International Journal of Obesity.

Watafiti hao walisema kwamba mafuta ya kwenye tumbo hutoa tindikali nyingi za mafuta zenye madhara kwa mwili wakati mafuta ya kwenye makalio na mapaja huzuia tindikali za mafuta zenye madhara kuingia kwenye misuli na maini na hivyo kuuepusha mwili na magonjwa ya kisukari na magonjwa ya moyo.

Ingawa mafuta ya kwenye makalio na mapaja huyeyuka taratibu sana lakini mafuta hayo hutoa homoni zenye faida zijulikanazo kama adiponectin ambazo huilinda mishipa ya damu na kusimamia kiwango cha sukari mwilini.

Wanasayansi hao walisema kuwa wanaendelea na utafiti ili kutengeneza dawa za kuufanya mwili uhifadhi mafuta yake kwenye makalio na mapaja ili kupunguza matatizo ya kiafya yanayosababishwa mafuta kujazana kwenye tumbo.

Utafiti huo ulimalizia kwa kusema kuwa wanawake wenye mapaja au makalio madogo sana wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo kadhaa ya kiafya kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;">
</td></tr></tbody></table>
 
Ndo maana napenda mwanamke wa kiafrika yaani VAS(Value Added Services) kwa kwenda mbele.
 
Ni waingereza hao hao wanaopenda ukimbaumbau hata wanajienzi kwa kujisemea "English figure" Kama wameanza kusema hayo maneno wanakumbukia enzi zao za ukoloni walipokuwa wanagegeda dada zetu. Nimewashitukia hao.
 
Kwa jina la msemaji inaonyesha ni mgiriki sio mwingereza! japo utafiti umefanyika UK
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom