Makala za Mohamed Said Katika Mwananchi: Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika

ukereketwa kazi kweli

umeandika " Nijuavyo tuko mbioni kusherehekea miaka 50 ya nchi ya Tanzania ambayo ndio iko kwenye ramani ya dunia"

HII SENTENSI YAKO INA MATATA

HESABU VIZURI,

TANZANIA ILIANZA 26 APRIL1964 ,

ukihesabu 1964 mpaka 1981 ni miaka mingapi???? 50?????
tukihesabu kuanzia 1964 mpaka 1981, basi ni miaka 17
 
Jaman pamoja na majigambo yote ya serikali ikiwemo slogan yao ya TUMEJARIBU,TUMETHUBUTU NA TUNASONGA MBELE bado tanzania/tanganyika ntunahitaji "second indepence" ndsani yetu ili tuweze kuondokana na lindi la umaskini,ujinga,woga na manyanyaso kutoka kwa serikali ya kifisadi iliyopo madarakani.
 
Ili nisome kitabu chako nihakikishie kwanza kuwa wewe unajua pia upande mwingine wa shilingi jinsi watu wa maeneo ya bara walivyopigania uhuru ili niondokane kwanza na mtazamo kuwa wewe unafahamu mambo ya pale gerezani tu. Halafu ktk uandishi wako usitumie reference ambazo zina mlengo wa kidini i.e Tumaini letu, nyakati, Al huda, An nuur. Tumia neutral sources. Kwangu mie naziamini zaidi habari za Aljazeera, PressTV kuliko taarifa za Al huda na An nuur maana naamini kuwa waandishi ktk magazeti hayo sio waandishi makini.
Ndugu yangu uamuzi unao mwenyewe.Ukipenda soma la hupendi acha.Hatutagombana kwa hilo.Mohamed
 
Wanaukumbi,

Kuanzia leo Jumatano, 28 Septemba
Mwananchi limeanza "series" zangu na
za waandishi wengine kuhusu Miaka
50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Tusomeni kwa furaha.

Mohamed Said

========================
UPDATE 29/09/2011
========================

Unapoteza muda, find some business to do upate japo pesa ya kula, umetumwa na BAKWATA, waislamu wa ukweli they aint enslaved like what you're thinking, kaa hivyo hivyo , huchoki tu kuwa-victimize, wamestuka tayari huoni haya!
 
Ahsante kwa mchango wako.

Katika gazeti la Mwananchi la leo kuna makala zangu mbili
na kila moja nimeandika kwa staili yake.

Moja nimezungumzia Tanganyika chini ya Udhamini wa Umoja
wa Mataifa.

Makala ya pili nimejieleza mimi mwenyewe kama mtoto mdogo
wakati wa kupigani uhuru.

Nimeanza kwa kuhadithia nyumba kwa nyumba mitaa ya Gerezani
nilikozaliwa na kukulia nikieleza historia za wazee wangu walivyochangia
katika kupigania uhuru.

Sijui hili la Uislam liko sehemu gani. Tafadhali nifahamishe wapi umeliona.
Nimepitia upya makala hizo sikuona popote neno Uislam.

Mohamed
Unashukuru nini sasa, it seems hata wewe huelewi unachoambiwa! Moderator can you block guys like this! kwanza anachafua hali ya hewa tu!
 
Unashukuru nini sasa, it seems hata wewe huelewi unachoambiwa! Moderator can you block guys like this! kwanza anachafua hali ya hewa tu!

Ndugu yangu mbona una kuwa mkali bila sababu.

Huu ni mnakasha tu. Majadiliano.
Hapana haja ya kutoleana ufedhuli.

Ikiwa lipo nililokosea ustaarabu ni kunifahamisha
sio kutoa jeuri.

Huu si ukumbi wa watu wenye fikra pana?

Mohamed
 
Unapoteza muda, find some business to do upate japo pesa ya kula, umetumwa na BAKWATA, waislamu wa ukweli they aint enslaved like what you're thinking, kaa hivyo hivyo , huchoki tu kuwa-victimize, wamestuka tayari huoni haya!

Pole sana ndugu yangu.

Jifunze utulivu katika kuongea.

Kuna mengi utafaidika.

Mohamed
 
Mohamed Said,

Bandika vitu mwanzo mpaka mwisho, maswali na majibu mwisho wa bandiko. Achana na hawa wanaosutwa na historia, wanakuta ukweli uliopo ni tofauti na wanavyofundishwa kwenye shule zao za kanisa.
 
Faiza Foxy,

Asante sana kwa hilo ila suala la kanisa ungelipunguza kwani hata sisi tuliosoma shule miaka 1970-1980 tulikuwa tukimeza misumu ya vitabu vya wakoloni. Nilikujaga kusoma historia ya zanzibar nilipokuwa kikazi Zanzibar kutoka kwa wazanzibar wenyewe na baadhi ya wazee waliokuwa wakiishi huko nilitokwa na machozi jinsi wakoloni na serikali ya JKN walivyopindisha mambo mengi. Moja wapo kukataa kuwa utawala wa Sultani ulikuwa ukinufaisha wazanzibar na dhana ya mapinduzi ilikuwa slogan ya kibaguzi na chuki dhidi ya wasiokuwa na asili ya kiarabu. Watu wakati wa Sultani Khalifa mfano walikuwa wakipewa maziwa bure kisiwa kizima, shule bure kisiwa kizima, wanafunzi wanapewa uniform, vitabu na madaftari bure sasa nikajiuliza ubaya wa Sultani uko wapi??? Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. Sheikh Mohammed Said endelea kumwaga vitu nimefanya research ya unayosema kuhusu majimaji kwa jamaa zangu wa huko Kilwa na kuconfirm kumbe wale walikuwa watu wa tariqa bwana na wakati mie nilisoma historia ya vita vya majimaji vitabu vikasema ati mganga alikuwa akisoma maji halafu risasi ya mkoloni itageuka kuwa maji (huu ni uongo na nadhani walioandika historia wanatakiwa kuwa sued for intellectual infringment (wamedanganya na kuhadaa)). Maji yalikuwa sio ya mganga bali hawa walikuwa waislamu na walikuwa wakitawadha na kutia udhu na kwenda kupigana vita kama uislamu unavyosema ili wakifa wafe mashahidi. Hiyo dondoo moja Sheikh Mohammad Said ya jitihada zangu binafsi kuufahamu ukweli wa historia ya linchi letu.

Narudia Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Wakuu, hii mada ukiisoma vizuri, ina mafundisho na inatia kiu zaidi kuijua historia ya kweli ya nchi yetu iliyotukuka, nchi ya Tanganyika. Najuwa kuna wanao ujuwa ukweli na hawataki ukweli ujulikane, lakini kupitia hii thread nadhani ni mahala mwafaka kabisa kwa kila Mtanganyika anayejuwa historia ya wapigania uhuru, basi hii ndio fursa kuwaweka hapa, ili kila mtu ajuwe michango yao... Na hao mashujaa wa uhuru si wale wa mikoa ya pwani tu kwa maana ya wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake, la hasha... Watoke mikoa mbali yote ya Tanganyika.

Natarajia wapo wanaojuwa mashujaa kutoka mikoa mingine, kama vile Mwanza, shinyanga, Kigoma, Tabora, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mara, Kagera, Dodoma, na mikoa mingine ya Tanganyika (Tanzania Bara).

Tuichukulie hii topic katika hali chanya, na tuijazilie kwa kile tukijuwacho. Wapo wapigania uhuru waliokuwa Waislam, Wakristo na waliokuwa wakiabudu dini za jadi, basi tuwaweke hapa na kila mtu awasome. Mimi nina uhakika kabisa uko mikoani wapo waliojitolea kwa hali na mali katika kadhia hii ya kugombania uhuru, basi tuwape heshima yao japo kwa kuwataja tu majina yao.

Miaka ishirini (20) mpaka therathini (30) nyuma, hatukuweza kupata nafasi kama hii, ya kujimwaga na kujifaragua, sasa ndio wakati mwafaka wa kuelezea kile kilichokuwa kikifichwa hapo zamani...! Chuki zisitawale huu mjadala, kama ndugu yetu Mohamed Saidi yeye anaelezea historia, inayo wagusa Waislam wa mitaa ya Kariakoo na Gerezani, basi aje mwingine aelezee, wapigania uhuru wa mikoa mingine, aidha Wakristo waliojitolea kumtoa mkoloni au walio amini dini za jadi. Maana wote hao ni Watanganyika na wana haki ya kuelezwa hapa na mahala pengine...!

Tusiukatae ukweli, maana ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi, leo ukiukataa, kesho ukweli utakuja julikana, basi nyuso zetu tutaziweka wapi? Au mpaka mkoloni arudi tena na kutufundisha historia ya nchi yetu wenyewe?

Jamani shime shime! Wakati ndio huu.
 
Mohamed Said aweke ukweli
ila akileta udini mimi nitamletea udini mara mbili
Dawa ya mdini ni kuwa mdini zaidi yake
 
Ahsante ndugu yangu.

Mimi nawaonea huruma sana hawa ndugu zetu kwa kuwa kwa hakika
kwao wao hii historia ya wazee wetu imewashtua sana si kitu ambacho
walitegemea kipo.

Sasa baya zaidi akili zao zimefungika hawataki kusikia kitu kipya wakisoma
kitu kipya hasira zinapanda na kwa ajili hii wanapoteza hata ule utulivu wa
kufanya tafakuri.

Tusichoke kusomesha na kuelimisha.
Atakae atajifunza asiyetaka basi.

Mohamed
 
Mohamed Said aweke ukweli
ila akileta udini mimi nitamletea udini mara mbili
Dawa ya mdini ni kuwa mdini zaidi yake

Bi Maria,
Ahsante.

Lakini mbona unaanza kwa vitisho?

Hayo hayo ulosema ungeweza ukayasema
katika hali ya utulivu na uungwana zaidi kiasi
cha hata kumpedezesha unaejadiliananae.

Ukianza kwa hamaki unanipa mimi ushindi
kwa kukutambua kuwa ni mtu wa hasira kwa
hiyo kukushinda ni kama kumsukuma mlevi.

Nisome katika Mwananchi na The Citizen kila
siku zinatoka series zangu hadi kilele cha uhuru
9 Desemba Insha Allah.

Mohamed

Wakuu, hii mada ukiisoma vizuri, ina mafundisho na inatia kiu zaidi kuijua historia ya kweli ya nchi yetu iliyotukuka, nchi ya Tanganyika. Najuwa kuna wanao ujuwa ukweli na hawataki ukweli ujulikane, lakini kupitia hii thread nadhani ni mahala mwafaka kabisa kwa kila Mtanganyika anayejuwa historia ya wapigania uhuru, basi hii ndio fursa kuwaweka hapa, ili kila mtu ajuwe michango yao... Na hao mashujaa wa uhuru si wale wa mikoa ya pwani tu kwa maana ya wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake, la hasha... Watoke mikoa mbali yote ya Tanganyika.

Natarajia wapo wanaojuwa mashujaa kutoka mikoa mingine, kama vile Mwanza, shinyanga, Kigoma, Tabora, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mara, Kagera, Dodoma, na mikoa mingine ya Tanganyika (Tanzania Bara).

Tuichukulie hii topic katika hali chanya, na tuijazilie kwa kile tukijuwacho. Wapo wapigania uhuru waliokuwa Waislam, Wakristo na waliokuwa wakiabudu dini za jadi, basi tuwaweke hapa na kila mtu awasome. Mimi nina uhakika kabisa uko mikoani wapo waliojitolea kwa hali na mali katika kadhia hii ya kugombania uhuru, basi tuwape heshima yao japo kwa kuwataja tu majina yao.

Miaka ishirini (20) mpaka therathini (30) nyuma, hatukuweza kupata nafasi kama hii, ya kujimwaga na kujifaragua, sasa ndio wakati mwafaka wa kuelezea kile kilichokuwa kikifichwa hapo zamani...! Chuki zisitawale huu mjadala, kama ndugu yetu Mohamed Saidi yeye anaelezea historia, inayo wagusa Waislam wa mitaa ya Kariakoo na Gerezani, basi aje mwingine aelezee, wapigania uhuru wa mikoa mingine, aidha Wakristo waliojitolea kumtoa mkoloni au walio amini dini za jadi. Maana wote hao ni Watanganyika na wana haki ya kuelezwa hapa na mahala pengine...!

Tusiukatae ukweli, maana ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi, leo ukiukataa, kesho ukweli utakuja julikana, basi nyuso zetu tutaziweka wapi? Au mpaka mkoloni arudi tena na kutufundisha historia ya nchi yetu wenyewe?

Jamani shime shime! Wakati ndio huu.
Nasaha nzuri sana.

Kwa hakika wapo wengi walifanya mengi sana lakini hawatajwi.

Tuna dhima ya kuwatafuta mashujaa hawa na kama wametangulia
mbele ya haki na tufanye utafiti juu ya maisha yao na tuandike.

Mohamed
 
'Ukweli unatabia ya kulipa kisasi,leo ukiukataa kesho tutaweka nyuso zetu wapi'? Nami nauliza ukweli ni upi kati ya wanaojadiliana kwa jambo walilosimuliwa au kuhadithiwa? Ukweli unapitakanaje kama haukidhi haja ya majadiliano au malumbano?.Je,ukweli unatokana na kumeza au kutafakari!
Mohamed Said:Kuanzia leo Jumatano, 28 SeptembaMwananchi limeanza "series" zangu na za waandishi wengine kuhusu Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika
X-PastersWakuu, hii mada ukiisoma vizuri, ina mafundisho na inatia kiu zaidi kuijua historia ya kweli ya nchi yetu iliyotukuka, nchi ya Tanganyika
Hadi hapa tunaona mada nzima inajadili miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Fair enough!
X-Paster: Mohamed Saidi yeye anaelezea historia, inayo wagusa Waislam wa mitaa ya Kariakoo na Gerezani, basi aje mwingine aelezee, wapigania uhuru wa mikoa mingine, aidha Wakristo waliojitolea kumtoa mkoloni au walio amini dini za jadi. Maana wote hao ni Watanganyika na wana haki ya kuelezwa hapa na mahala pengine
Uhuru wa Tanganyika halafu historia ya Kariakoo!! Nadhani tuwe wakweli ili tusiwafanye wana jamvi majuha.Kinachoongelewa hapa ni uhuru wa Tanganyika hili la Kariakoo ni kujaribu kuepusha 'bias'. Tuweni wakweli ni sehemu ya uungwana na uumini.

Mohamed Said ameleta mada hapa (ingawa si mpya) baada ya kuitoa magazetini. Nadhani nia ni kuamsha mjadala wa fikra utakaotusaidia kwenda mbele au vinginevyo kama hajaweka wazi. Taratibu zetu ni kuwa mada inapowekwa inapewa heshima ya kuchangiwa labda kama mwandishi atakuwa amekataa hilo kufanyika, na hiyo itakuwa ajabu kwasababu basi angeiacha huko magazetini wanaomeza wameze tu!

Midhali ameiweka hapa itapata changamoto zinazolingana na kwa viwango kama ilivyowahi kutokea huko nyuma. Katika tafakuri kutakuwa na mitazamo hasi na chanya, na ni wajibu wa mtoa mada kutoa uelekeo. Inapotokea kuwa 'criticized' na kuonekana kama ni 'uasi' au ukorofi ina leta maana kuwa mada imewekwa isomwe tu! na kama hilo ndilo lengo basi litoke tamko na litaheshimiwa.

Vinginevyo hatuna sababu ya kutuhumiana kwa kauli zisizo na ukweli au zenye kuamsha hisia chafu kama zile za 'kusoma makanisani' n.k. Wasomaji na wachangiaji wana mila, kabila na imani zao ikiwa ni pamoja na vyanzo vyao vya elimu, kazi n.k na si vema kuanza kupotosha mada kwa kuchomeka mambo kama hayo yanayojenga hisia za kibaguzi au udini. Lau kama hilo ndilo lengo ahlan wahsalan.

Andiko lolote hapa kwa mujibu wa forum hii lina haki ya kujadiliwa na kuhojiwa, nami nikiwa napenda kusimamia ukweli, kuhoji ili kuelewa na kukemea chembe zozote zinazolenga kuigawa jamii yetu nitahoji bila kuomba radhi au ruhusu kwa kufuata kanuni za forum. Nitakemea ikibidi na kama kufanya hivyo sitampendeza mtu siombi radhi. Nitakachokikwepa ni kejeli,kashfa, tashtiti, munkari,jwazba na ubaradhuli wa namna hiyo.

Mohamed Said,
Ni nini mchango wa AMNUT katika harakati za ukombozi wa Kariakoo, Gerezani au Tanganyika?
Ni kwanini Waislam wa Kariakoo,Gerezani/Tanganyika hawakuiunga mkono?

Ni lini utaratibu wa kutumia namba katika mitihani ulianza kutumika?

Nisaidieni hapa nimekwama na nashindwa kuunganisha dot za mada kwasababu nimekwama. Tafadhali nifahamishe.

Ahsante.
 
Faiza Foxy,

Asante sana kwa hilo ila suala la kanisa ungelipunguza kwani hata sisi tuliosoma shule miaka 1970-1980 tulikuwa tukimeza misumu ya vitabu vya wakoloni. Nilikujaga kusoma historia ya zanzibar nilipokuwa kikazi Zanzibar kutoka kwa wazanzibar wenyewe na baadhi ya wazee waliokuwa wakiishi huko nilitokwa na machozi jinsi wakoloni na serikali ya JKN walivyopindisha mambo mengi. Moja wapo kukataa kuwa utawala wa Sultani ulikuwa ukinufaisha wazanzibar na dhana ya mapinduzi ilikuwa slogan ya kibaguzi na chuki dhidi ya wasiokuwa na asili ya kiarabu. Watu wakati wa Sultani Khalifa mfano walikuwa wakipewa maziwa bure kisiwa kizima, shule bure kisiwa kizima, wanafunzi wanapewa uniform, vitabu na madaftari bure sasa nikajiuliza ubaya wa Sultani uko wapi??? Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. Sheikh Mohammed Said endelea kumwaga vitu nimefanya research ya unayosema kuhusu majimaji kwa jamaa zangu wa huko Kilwa na kuconfirm kumbe wale walikuwa watu wa tariqa bwana na wakati mie nilisoma historia ya vita vya majimaji vitabu vikasema ati mganga alikuwa akisoma maji halafu risasi ya mkoloni itageuka kuwa maji (huu ni uongo na nadhani walioandika historia wanatakiwa kuwa sued for intellectual infringment (wamedanganya na kuhadaa)). Maji yalikuwa sio ya mganga bali hawa walikuwa waislamu na walikuwa wakitawadha na kutia udhu na kwenda kupigana vita kama uislamu unavyosema ili wakifa wafe mashahidi. Hiyo dondoo moja Sheikh Mohammad Said ya jitihada zangu binafsi kuufahamu ukweli wa historia ya linchi letu.

Narudia Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.

Bi Faiza,

Mungu akujaze kheri.
Napata faraja ninaposoma fikra kama hizo zako.

Historia ya Majimaji na makumbusho yake Mahenge, Songea
yapo katika mtihani mkubwa.

Hata yale majina ya askari wa Majimaji hayatakiwi kuwapo kwa
kuwa tu jeshi zima lina majina ya Waislam.

Majina ya mashujaa wale yanayoashiria Uislam wao yameondolewa.

Songea Mbano aliyekuwa amiri jeshi dhidi ya Wajerumani jina lake
ni Ali Songea Mbano.

Jina la Ali halitakiwi na ni hivyo hivyo kwa kila askari majina yalowekwa
ni ya Kikristo ati walibatizwa kabla ya kunyongwa.

Hii ni dhulma na upotoshaji mkubwa.

Soma hii kutoka "Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania Mainland":
[1]Maji Maji Museum in Songea which has been greatlydesecrated removing all signs of Muslim symbols during the Maji Maji War withGermans. The Maji Maji Museum at Peramiho under the Catholic Church has closedits doors to young inqusitive Muslims for fear of criticism for distorting history. AllMuslim symbols in Maji Maji War against Germans have been obliterated in theMaji Maji Museum.
[1] In all historical references to Maji Maji War hero and Chief of WangoniAli Songea Mbano, his Muslim name "Ali" would be omitted and he would bereferred to as Songea Mbano.

Mohamed
 
'Ukweli unatabia ya kulipa kisasi,leo ukiukataa kesho tutaweka nyuso zetu wapi'? Nami nauliza ukweli ni upi kati ya wanaojadiliana kwa jambo walilosimuliwa au kuhadithiwa? Ukweli unapitakanaje kama haukidhi haja ya majadiliano au malumbano?.Je,ukweli unatokana na kumeza au kutafakari! Hadi hapa tunaona mada nzima inajadili miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Fair enough! Uhuru wa Tanganyika halafu historia ya Kariakoo!! Nadhani tuwe wakweli ili tusiwafanye wana jamvi majuha.Kinachoongelewa hapa ni uhuru wa Tanganyika hili la Kariakoo ni kujaribu kuepusha 'bias'. Tuweni wakweli ni sehemu ya uungwana na uumini.

Mohamed Said ameleta mada hapa (ingawa si mpya) baada ya kuitoa magazetini. Nadhani nia ni kuamsha mjadala wa fikra utakaotusaidia kwenda mbele au vinginevyo kama hajaweka wazi. Taratibu zetu ni kuwa mada inapowekwa inapewa heshima ya kuchangiwa labda kama mwandishi atakuwa amekataa hilo kufanyika, na hiyo itakuwa ajabu kwasababu basi angeiacha huko magazetini wanaomeza wameze tu!

Midhali ameiweka hapa itapata changamoto zinazolingana na kwa viwango kama ilivyowahi kutokea huko nyuma. Katika tafakuri kutakuwa na mitazamo hasi na chanya, na ni wajibu wa mtoa mada kutoa uelekeo. Inapotokea kuwa 'criticized' na kuonekana kama ni 'uasi' au ukorofi ina leta maana kuwa mada imewekwa isomwe tu! na kama hilo ndilo lengo basi litoke tamko na litaheshimiwa.

Vinginevyo hatuna sababu ya kutuhumiana kwa kauli zisizo na ukweli au zenye kuamsha hisia chafu kama zile za 'kusoma makanisani' n.k. Wasomaji na wachangiaji wana mila, kabila na imani zao ikiwa ni pamoja na vyanzo vyao vya elimu, kazi n.k na si vema kuanza kupotosha mada kwa kuchomeka mambo kama hayo yanayojenga hisia za kibaguzi au udini. Lau kama hilo ndilo lengo ahlan wahsalan.

Andiko lolote hapa kwa mujibu wa forum hii lina haki ya kujadiliwa na kuhojiwa, nami nikiwa napenda kusimamia ukweli, kuhoji ili kuelewa na kukemea chembe zozote zinazolenga kuigawa jamii yetu nitahoji bila kuomba radhi au ruhusu kwa kufuata kanuni za forum. Nitakemea ikibidi na kama kufanya hivyo sitampendeza mtu siombi radhi. Nitakachokikwepa ni kejeli,kashfa, tashtiti, munkari,jwazba na ubaradhuli wa namna hiyo.

Mohamed Said,
Ni nini mchango wa AMNUT katika harakati za ukombozi wa Kariakoo, Gerezani au Tanganyika?
Ni kwanini Waislam wa Kariakoo,Gerezani/Tanganyika hawakuiunga mkono?

Ni lini utaratibu wa kutumia namba katika mitihani ulianza kutumika?

Nisaidieni hapa nimekwama na nashindwa kuunganisha dot za mada kwasababu nimekwama. Tafadhali nifahamishe.

Ahsante.

Ahsante kwa mchango wenye nasaa nzuri za kuelimisha.

Tusianze na AMNUT. Tutapunjika.

Tuanze mwanzo wa mwanzo wake.

Hisia za kutaka kuleta ubaguzi wa dini zilianza mwaka 1953
mara tu Abdulwahid Sykes alipomleta Nyerere katika TAA na
kumpa uongozi.

TAA siku zile pale New Street na kwa hakika siasa Dar es Salaam
zilikuwa zimetawaliwa na wenyeji na takriban wote walikuwa
Waislam.

TAA ikaanza kudidimia chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere. Sababu
ni kuwa hawakuwa na imani na Wakristo kuwa wangeweza kupambana
kumng'oa Muingereza kwa kuwa wao walikuwa wananufaika na mfumo ule.
Huu ndiyo ulikuwa mtazamo ndani ya TAA.

Sasa nini kifanyike ili TAA isife?

Ndipo hapo Abdulwahid na Dossa na vijana wengine wakawaendea wazee wa mji
kuwaeleza kile kilichokusudiwa. Nacho ni kuwaunganisha Watanganyika wote
kusaidia harakati za kupigania uhuru.

Mtu aliyafanikisha hili kwa vizuri kabisa alikuwa Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa Mufti wa
Tanganyika na Zanzibar. Yeye alikuwa mtu wa ndani katika wale waliokuwa wamepanga
kuunda TANU toka 1950 TAA ilipotengeneza Kamati Ndogo ya Siasa ndani ya TAA.

Sheikh Hassan Bin Amir alimuunga mkono Nyerere moja kwa moja. Sasa hapa Sheikh Hassan bin
Amir akajaungwa mkono na Sheikh Suleiman Takadir aliyekuja kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Wazee wa TANU, akaungwa mkono na Mohamed Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate, Mwinjuma
Mwinyikambi, Sheikh Mohamed Ramia kutaja wachache. Hawa watu walikuwa na nguvu sana k
atika jamii na ndiyo waliomfikisha Nyerere kileleni mwa uongozi wa Tanganyika. Hawa ndiyo walikuja
kuunda Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe 170 na wote Waislam.

Hili ndilo baraza lililofanikisha safari ya kwanza ya Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa, New York mwaka
1955.

Sasa AMNUT ilipokuja viongozi hawa wa Kiislam walikiona chama kile kama nuksi inayotaka kuwabagua watu
kwa misingi ya dini na hivyo kuleta vita na kuwapa Waingereza sababu ya kutotoa uhuru.

AMNUT ikapigwa vita na haikuweza kufanikiwa.

Kisa hiki nimekieleza kwa kirefu katika "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes" kitabu
kipo Tanzania Publishing House (TPH) kwa atakae kupata habari zaidi.

Kuhusu matumizi ya namba na majina katika mitihani. Ingekuwa na maana zaidi iwapo
Wizara ya Elimu ingetupa taarifa hiyo.

Mohamed
 
Una mfahamu Mohammed Said au una msikia tu?
Jamaa anatetea msimamo wake wa kidini kama nini vile.
Utabishana naye page na page kwa vile kwake uhuru ni uhuru wa uislamu dhidi ya dini nyingine na si vinginevyo.
Kama humjui mPM.

Nafahamu fika tumetofautiana sana kwa uwezo wa kuchambua mambo kutokana na tofauti ya uzoefu na hata ya elimu iliyopo baina yetu, lakini nakumbuka vizuri sana maelekezo ya mwalimu wangu mmoja nilipokuwa shule ya msingi aliponiambia usimbishie mtu kitu aemacho kwa vile tu unamchukia au kwa vile tu una tofauti nae kabla, msikilize asemacho wakati huo na ukijibu kutokana na anachokiongea muda huo na si kutokana na tofauti zenu mlizonazo au ulizozizoea kwani binadamu si jiwe, binadamu anabadilika anaweza ikiwa siku hiyo ameamua kuanzisha mazungumzo ambayo yanaweza kuelekeza mwanzo wa tofauti zenu kumbe ukakuta hakuna mnachotofautiana ila mmeshindwa tu kupeana muda wa kusikilizana. Msikilize mtu kwanza amalize, kama kuna hoja ambazo huzielewi muulize taratibu, na kama kuna hoja ambazo zinapinganamuombe atoe ufafanuzi na kama kuna hoja ambayo hukubaliani nae ipinge kwa hoja nyingine kwa kutumia maelezo mazuri kabisa. Waweza fikiri kuwa hajui kitu kumbe wewe ndiye usiyejua kitu. Kila kwenye hoja tusizozipenda kuna kitu ambacho aidha hatukijui au hatutaki kukifahamu kwa vile tunaogopa na kuhisi kwamba ukweli wake unaweza ukawa tofauti na matarajio yetu. Tusiogope kwani uzoefu mpya hata kama ni mgumu na wa kuumiza namna gani ndio maarifa yanayomtofautisha mwenye busara na yule asiyekuwa nazo
 
Bi Faiza,

Mungu akujaze kheri.
Napata faraja ninaposoma fikra kama hizo zako.

Historia ya Majimaji na makumbusho yake Mahenge, Songea
yapo katika mtihani mkubwa.

Hata yale majina ya askari wa Majimaji hayatakiwi kuwapo kwa
kuwa tu jeshi zima lina majina ya Waislam.

Majina ya mashujaa wale yanayoashiria Uislam wao yameondolewa.

Songea Mbano aliyekuwa amiri jeshi dhidi ya Wajerumani jina lake
ni Ali Songea Mbano.

Jina la Ali halitakiwi na ni hivyo hivyo kwa kila askari majina yalowekwa
ni ya Kikristo ati walibatizwa kabla ya kunyongwa.

Hii ni dhulma na upotoshaji mkubwa.

Soma hii kutoka "Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania Mainland":
[1]Maji Maji Museum in Songea which has been greatlydesecrated removing all signs of Muslim symbols during the Maji Maji War withGermans. The Maji Maji Museum at Peramiho under the Catholic Church has closedits doors to young inqusitive Muslims for fear of criticism for distorting history. AllMuslim symbols in Maji Maji War against Germans have been obliterated in theMaji Maji Museum.
[1]In all historical references to Maji Maji War hero and Chief of WangoniAli Songea Mbano, his Muslim name "Ali" would be omitted and he would bereferred to as Songea Mbano.

Mohamed

Mohamed,

Nilifanya utafiti huo kule Kilwa nikaambiwa waliopigana majimaji hawakuwa wapagani bali walikuwa waislamu. Tena walinambia Uislamu uliingia Kilwa mwaka 2 baada ya Mtume Muhammad (SAW) kupewa utume kuna familia ya moja wapo ya ahlul sahaba au sijui ahlul bayt walisafiri kuja habasha wakahama na kuhamia Kilwa. Kilwa huko mwaka 2 Hijra Calendar. Maeneo ya Kilwa yalikuwa na maendeleo makubwa ya civilization kuliko eneo lengine Africa including sehemu ya kwanza kuwa sarafu yake. Inakuwaje sasa maeneo hayo yalikuwa na ustaarabu na uislamu ulienea kwa kiwango kikubwa Kilwa, Lindi, Mtwara halafu tusome historia inayosema kuwa ati walikuwa ni jeshi la savages walioaminishwa na mganga wao Kinjekitile Ngwale. This to me does not make any sense at all!!!! Ni sawa na kusema England tunayoijua Anglican Church is dominant faith tuambiwe na historia kuwa walikuwa mijitu isifuata dini wakati wanapigana vita. Either kuna uongo umefichwa au aliyefanya utafiti amendisha mambo mengine au pengine tunavyofahamu sivyo. Labda tuwaulize walioandika historia ya Tanzania information zao wamezitoa wapi? Na tufanye DNA test kutrace origin ya waliofariki vita vya maji maji nadhani tunaokelekea kuna watakaoumbuka vibaya sana.
 
To imply that the struggle for Uhuru wa Tanganyika was solely initiated or even spear-headed by those mentioned by Mohamed Said is a distortion of history.

Tanganyika being a Trust Territory of the British, the United Nations Organization received Tanganyika representatives as early as 1945. The Trusteeship Council was addressed by Tanganyika personalities like Japhet Kirillo on the Meru Corridor dispute in the late 1940s triggering the fight for freedom and the right to own our land. Personalities like John Rupia, Cliest Sykes and Dossa Aziz and those who initiated TAA (Tanganyika African Association), stressing the inclusion of country-wide leaders like Adam Sapi Mkwawa, Abdallah Fundikira, Humbi Ziota, Kidaha Makwaiya of Shinyanga, Elias Sarwatt of Mbulu and Chief Patrick Kunambi of Morogoro.

What I am trying to say is that the struggle for Uhuru was not purely a Dar es Salaam Kisutu affair. There were many players.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom