Wakati mwingine nikisoma baadhi ya mabandiko humu nacheeeka hadi gego la mwisho. Kwa nini:Nakushukuru sana kwa kutuwekea wazi jinsi ulivyo mdini. Hapana shaka unamsifia Nyerere kwa jinsi alivyotumiwa vizuri na Kanisa katika kuwasaliti na kuwahadaa wale wazee wa kiislam na kisha kuwavunjia kwa nguvu ule umoja wao wa EAMWS na kuwawekea BAKWATA kwa lazima. Kwa nguvu hizo hizo za Kanisa kumtumia vizuri Nyerere, leo Waislam wameachwa kama mayatima ktk. Nchi yao. Kwa hali hiyo sasa Mwita kwake kicheeko, kuwa 'Nyerere kafanya mazuri sana' na atayatetea kwa nguvu zote na kubeza kila jitihada zitakazofanywa na Waislam kujikwamua. Bado tena Mwita anatufundisha 'udini' kuwa eti Waislam bado wamelala, wanatakiwa kuamka na kuwatumia vizuri Mwinyi kwa wakati ule na sasa Kikwete kupata Mou toka kwa Muislam mwenzao kwa vile wao kina Mwita (Wakristo) walimtumia vizuri Nyerere Mkristo mwenzao. Kwa msemo mwingine ni kusema hivi: Nyie Waislam amkeni mumtumie Kikwete kupata Mou yenu, akiingia Rais Mkristo hampati kitu! Huu ni 'udini' wa wazi wazi. Kazi kwenu Waslam.
-Nguvu za ziada za Mwalimu alizokuwa nazo. EAMWS anavunja. Anatafuta WAislamu "feki" anawaundia BAKWATA!
-Serikalini anakuwa na WAISLAMU wengi tu "feki" kuanzia makamu wake.
-Ndani ya CCM nako anajizungushia WAISLAMU "feki" wengi tu.
-Anaunda MUUNGANO na nchi ya WAISLAMU 99%!
-Anafungua balozi nchi nyingi tu za Kiislamu ikiwemo Palestina isiyo na hadhi ya "State".
Nimesoma gazeti la Jambo Leo. WAISLAMU wanataka MoU ya serikali na makanisa ivunjwe. Sio wao waingie ya kwao na serikali sijui kwa huduma zipi! Ulevi wa UDINI tu.