Makala hii katika Tanzania Daima imenivutia mno

Halafu tunashangaa kwa nini madawa ya kulevya yamezagaa nchini? sasa sishangai kwa nini Wanajeshi wa Mali waliamua kuwachukulia hatua manyang'au wao ambao wahalifu wenzao waliosheheni "ECOWAS" na "AU" wanahaha kuwatetea!

Mkuu umeona jinci maelfu wa raia wa Mali walivyoingia mitaani kuandamana kulaani kauli ya ECOWAS na kulipongeza jeshi kwa kuchukua madaraka..? Niliona kwenye TV wananchi wakiwa na furaha sana.. How i wish yatokee na maeneo mengine ambako demokrasia inabakwa..!
 
Katika gazeti la jana la Tanzania Daima kulikuwa na makala hii ya Nkwazi Mhango iliyonisisimua na kunivutia sana. Mimi niko mbali na Dsm na husoma makala kwa njia ya mtandao. Kwa faida ya wengi ambao hawakubahatika kulipata gazeti hili jana naweka makala hii ili nao waisome na ikibidi wachangie hoja.

Ila ndugu zangu hapa ndipo tulipofika sasa hakika hali ni mbaya mno.ila huwa tunafarijiana eti tuna amani.Amani inasaidia nini watu wanachukua mali ya nchi serikali inaaagalia tu sheria haichukui mkondo wake ,kisha mnarudi kutusifia eti WaTanzania tunaamani mimi naona bora kuingia barabarani bora hata tukapoteza uhai kwa sasa ili wengine wapone hata kama siyo leo watakuja kufaida kama si watoto wetu basi wajukuu,potelea mbali hata kama sisi tutakuwa hatupo watakumbuka kuwa haya yalikuwa matunda ya wazee wetu,kuliko hali tuliyonayo ya kufarijiana pasipo maana.
 
Sosoliso una mawazo kama yangu sijui wale jamaa waliotoa siku 100 wamepotelea wapi?
Nchi iko ICU hii na kama ndege ni auto pilot!
Yaani kila mtu anafanya atakavyo na hakuna wa kumdiscipline mwenzie yaani mdogo kama mkubwa na mkubwa kama mdogo
 
Watanzania wenzangu makala hii naomba itufanye kuanza kuomba dua kwa muumba ili atusamehe dhambi inayolitafuna taifa letu kwa taifa levye watawala wanapenda kuona uovu ni kitu cha fahari ,kuhujumu mali ya umma na kujitarisha kwa njia chafu kwa ni haki yao.
Serikali yetu na watawala wake yote hayo wanayajua lakini kwakuwa hali hizo zina masilahi kwao ya kujitajirisha wala hawawezi kuchukua hatua yoyote.Umaskini wakujitakia kwetu unazidi kututafuna wakati sisi tu matajiri kwa natural resources.Mungu wangu onekana sasa na kutookoka kwa namna yoyote ile itakayokupendenza iwe kwa vote,au kama Mali au vyovyote yalivyo mapenzi yako.Mungu tuhurumie maana taifa letu mabaya yamezidi mazuri.Kila kukicha tunasikia na kujionea wenyewe namna watu wasio na huruma na mali za watanzania wanavyowaza kujineemesha wao wenyewe.Leta mapinduzi ya kweli na haki hata kabla ya 2015 tutapokea kwa moyo mmoja.
Makala hii imeumiza sana roho yangu lakini yote na mwachia Mungu aliyenauwezo wa kuwavunja na kuharibu kila falme zinazokumbatia uozo na ufisadi kama ilivyo serikali ya ccm.
 
BAdo tuna safari ndefu ndugu zangu,lakn jambo la msingi kila mmoja ahakikishe eneo alipo anatoa elimu ya Uraia hasa kwa vijana kama mimi na kundi ambao tupo kwenye elimu tufanyapo huku na kwa maana hii mpaka 2015 najua tutakua tumetengeneza vijana wengi kwa kweli na hakika Mungu atasaidia kwa haya tuyafanyayo
 
hivi mpayukaji wa msema hovyo ndio nkwazi?makala zake huwa hazina chembe ya woga.
 
Katika gazeti la jana la Tanzania Daima kulikuwa na makala hii ya Nkwazi Mhango iliyonisisimua na kunivutia sana. Mimi niko mbali na Dsm na husoma makala kwa njia ya mtandao. Kwa faida ya wengi ambao hawakubahatika kulipata gazeti hili jana naweka makala hii ili nao waisome na ikibidi wachangie hoja.

Mhariri alieleza kilio halisi cha taifa, nawe Umeeleza hali halisi ilivyo mbaya! Taifa limefikishwa mwisho na viongozi wezi, walafi...

Kadhalika, tusisahau hela ya Rada ambayo ufisadi wake uliwajaza mapesa viongozi wa juu wa Awamu iliyopita akiwepo na Mkaa-apa mwenyewe lakini wote tumesahau na serikali hiyo iyo inashangilia kuwa upande wa pili wa ufisadi umekubali kulipa hela na kiunafiki wanaipangia kununua vifaa vya mashule ili waonekane wanajali...Hao akina Mkapa na Chenge na maafisa wengine kwanini wasifilisiwe na hela waliojichumia ipelekwe kwa manunuzi ya vifaa vya mashule na mahospitali? Huo wizi serikali hii inayo majibu? Naamini hata Serikali ya Mali, wananachi wake wawajavumilia kwa kiasi walivyo watanzania! Mungu wetu ni Mungu wa kweli, ametuumba ili kwa haki zetu tuishi, na anayetumia haki na dhamana ya raia kama walivyofanya viongozi hawa kuhusu wizi na ufisadi katika RADA, RICHMOND/DOWANS, IPTL, MADINI, EPA, KIWIRA, RELI, WANYAMA MALI-ASILI, BIASHARA YA UNGA nk, Hukumu yao ni moja tu! Nayo itakuja! 'Hawastahili kuendelea kutembea mitaani' Siku inakuja na watahukumiwa, hakuna wa kuifuta siku hiyo! Watahukumiwa na Umma, au Jeshi (maana Mahakama zetu 'hazipo kwa ajili yao'). Au Mungu mwenyewe atatenda maajabu! Hakuna Mtanzania/raia aliyeumwa kuishi ktk mateso ya namna hii, ambayo mengi yanajengwa makusudi na viongozi na walafi kwa upofu wao na kukosa dhamira! Wezi hawa Hawastahili kuendelea kuonekana mtaani!
 
Bado tupo katika alama ya kujiuliza Kwanini? Rasilimali tulizobahatika kuwa nazo nchini ni maradufu ya idadi
yetu, kila raia kazidiwa mara mia moja na rasilimali tuliyonayo. Sasa swali la kujiuliza kwanini??? wanufaike
watu kumi badala ya Taifa zima, kitu ambacho kinawezekana kufanyika kwa maslahi ya wote na Taifa kwenda
juu zaidi kiuchumi. Imani ya kuishinda roho imekuwa ni ngumu kwa viongozi, ambayo ndio inayosababisha tamaa
kuelekea kwenye ufisadi, rushwa, kujilimbikizia mali, ukatili na kutolijali Taifa lao.
 
Mkuu umeona jinci maelfu wa raia wa Mali walivyoingia mitaani kuandamana kulaani kauli ya ECOWAS na kulipongeza jeshi kwa kuchukua madaraka..? Niliona kwenye TV wananchi wakiwa na furaha sana.. How i wish yatokee na maeneo mengine ambako demokrasia inabakwa..!

Hapo rekebisha kwa neno kulilaani.
 
Back
Top Bottom