Karibuni masijala
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 409
- 135
Kuna kila sababu sasa ya kukipumzisha. Kimechoka na kinatuchosha tena Kimezeeka na kukiendekeza ni kufanya mzaha na Taifa hili. Kwani katika uzee wake kimekuwa legelege na hakina mikakati, iwe ni ya kukinusuru au kuinusuru nchi hii na matatizo yake. Kinajiendea kwa mazoea na sasa kuna dalili zote kinachapa mwendo kuelekea kaburi lake la kisiasa.
Kwa sasa hivi kimesambaratika mapande mapande. Mapande mengine yakishikiliwa na nguvu ya dola kwani bila vyombo vya mabavu haiwezi kufika hata kesho. Kwani kinabebwa ili kifanye siasa, lakini hakibebwi kutatua matatizo yetu ya kweli ya Taifa letu. Hivyo tunahitaji chama mbadala na ninaweza kusema hata kama ni kujaribu kingine wacha tujaribu tu. Liwalo na Liwe.
Hatuwezi kuendelea na watu wale wale waliotuangusha miaka nenda rudi, kimeshindwa kujipanga kujana mikakati ya kuikwamua nchi tunachokiona ni mikakati binafsi ya kuchukua madaraka. Na sasa mambo hayendi.
Nikupe nafasi nawe kuchangia kama nawe umechoshwa na chama hiki au hujachoshwa maana kuna wachache wananufaika nao ni huru kuchangia kwa hoja ili nasi tuwaelewe. Makala