Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,583
pia katika wasukuma haoa hao tunetofautiana kunawasukuma wa shinyanga (wanyatunzu),
Mimi ni Mnyantuzu na kwetu ni Bariadi ambayo zamani ilikuwa ni moja wa wilaya za mkoa wa Shinyanga na sasa ndiyo makao makuu ya mkoa wa Simiyu.
Kwa hiyo Wanyantuzu si Wasukuma wa Shinyanga peke yao. Wasukuma wa Kahama au hata Shinyanga mjini na maeneo ya jirani kama Ibinzamata, Ibadakuli, Maganzo, n.k. wana lahaja tofauti na Wasukuma watokeao Ntuzu.
Wanyantuzu ni Wasukuma watokeao Ntuzu ambayo ndiyo present day Bariadi.
Ili kuweza kuzibaini tofauti hizo ni lazima uwe unajua vizuri mojawapo ya lahaja za Kisukuma la sivyo unaweza usijue tofauti.