Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

Unawasema hawa ni Wanyatunzu,ambao wao ni pesa tu.Kina Cheyo,Vijisenti na hawa akina Rehema ya Mungu ni watu wa Bariadi.
Jamaa wana msimamo sana..ukiwa chapa wanapokea lakini jibu wanalo kwenye vijisanduku...walifanya hivyo 1995 nilishuhudia walivyo kuwa wanapokea pesa ya CCM na kuvaa vit-shirt, kanga za na kofia za CCM lakini mwisho wa siku CCM miguu juu...
 
Ya Ukabila Yameanza????, Ukabila unanafasi gani katika Uongozi!, hili lisizungumzwe hadharani.
Ndilo swali nililotaka kuuliza!!!!!!!!!!!!!!!!ukubwa wa kabila na uongozi vinahusiana nini?au ni mimi sijaelewa vizuri?
 
"Ni heri uwe na dini lakini usiaathiriwe na virusi vya udini, na ni afadhali mara elfu uwe na kabila lako ili kujua namna ya kufanya matambiko yenu na kujua watani wako ni makabila gani kuliko kuwa na hisia na kuwa mkabila" alisema Mwalimu Julius Nyerere katika maisha yake.
well said
 
Mwisho watasema kabila lenye 10% ya population lipewe nafasi 10% za uongozi. Hatari.
 
Zenji,Tanga,Kilwa Dar kuna resources gani?Mshukuru watu wa bara kuja kujenga huko.
Mdigo ana maendeleo gani.

Si ndio njama zilifanywa na CCM ya kipindi hicho.. kumaliza mkonge, rei ya tanga!, bandari!! nashukuru saana viongozi wa sasa wa CCM ya sasa wana AKILI... pwani tuna resources zote! .. tunaringa na bahari yetu!... unauoiza mdigo ana maendeleo gani? kwani wewe mmakonde una maendeleo gani! Watu wa bara wamevamia miji ya pwani including TANGA! nakupoteza ustaaarabu wetu! mfano mzuri tanga yetu wachaga walivyoiharibu!.

mnasema naleta ukabila! huyu aliyenzisha hii thread nilimuuliza swali hilihili!..

watu wa tanga wenzangu tunahitaji michango yenu hapa http://www.usagara.org/ tukishikiana na mbunge wetu mtarajiwa muheshimiwa omar nundu tutafika tu
 
Ukiwa na kesi polisi, moja ya maelezo wanayochukua katika utambulisho wako ni kabila. Ukienda katika nyumba za kulala wageni, moja ya sehemu ya kujaza baada ya jina lako ni kabila. Na Mwalimu alisema tunaulizana makabila tunapotaka kutaniana tu! Ni kweli?
 
Ukiwa na kesi polisi, moja ya maelezo wanayochukua katika utambulisho wako ni kabila. Ukienda katika nyumba za kulala wageni, moja ya sehemu ya kujaza baada ya jina lako ni kabila. Na Mwalimu alisema tunaulizana makabila tunapotaka kutaniana tu! Ni kweli?

kwani wewe kabila gani?....
 
Ukiwa na kesi polisi, moja ya maelezo wanayochukua katika utambulisho wako ni kabila. Ukienda katika nyumba za kulala wageni, moja ya sehemu ya kujaza baada ya jina lako ni kabila. Na Mwalimu alisema tunaulizana makabila tunapotaka kutaniana tu! Ni kweli?

Kimsingi ukabila (with a negative tone) bado upo Tz ingawa sio kwa kiwango unachoweza kukilinganisha na nchi nyingine za jirani.

Lakini kutokuwa na 'ukabila' au 'udini' haina maana kwamba orientations za kikabila au kidini hazipo relevant tena katika maisha ya kila siku ya wanajamii. Hivyo kwa polisi kuchukua hiyo information sidhani kama ni kwa nia mbaya hasa zaidi ya kusaidia katika identity ya mtu.

Bado kuna situations ambazo inabidi tuulizane dini au kabila. Angalia katika harusi, maziko/mazishi nk utaona bado vitu hivi vinachukua nafasi kubwa tu.
 
Nilisomeshwa na kusoma katika vitabu kuwa TZ kuna makabila zaidi ya 120. Nani anajua idadi yake hasa?
Nimejaribu kuweka baadhi ya makabila hayo (kama nimekosea kuandika jina sahihi nisahihishwe na samahani). Naomba wale wanaokumbuka kabila lolote, endeleza orodha:
1. Wahehe 2. Wambungu 3. Waimao 4. Wachaga 5. Wapare 6. Wanyakyusa 7. Wanyamwezi 8. Wasukuma 9. Wahaya 10. Wafipa 11. Wamasai 12. Wandali 13. Wangoni 14. Wadigo 15. Wasambaa 16. Wahagaza 17 Wakurya 18. Wajita 19. Wazigua 20. Wadigo 21. Wadoe 22. Wameru 23. Wairaqw. 24. Warangi 25. Wakinga 26. Wasumbwa 27. Wapangwa 28. Wandamba 29. Wanyika 30. Waruguru 31. Warangi.................................
 
Source plz??? I have never heard some of the tribes mentioned, like those in red. Some of the mentioned tribes are not tribes as such but clans within a tribe. Some of the mentioned are "extinct", i.e. they have integrated themselves into bigger ones.

WaAlagwa, kabila ili linapatikana wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma, ila wengi kwa sasa wameingiliana na Sandawe

WaAkiek au WaOgiek, wanaishi kati ya Tanzania na Kenya, na Lugha yao ni moribund. Ila wengi wao kwa sasa wanaongea Kimaasai

WaAssa wamemezwa na Wamaasai waishio kaskazini ya Tanzania. Kwa sasa wapo wachache sana na wamemezwa na kabila la Kimaasai, ukiwaona wanataka kufanana na kabila la Wadorobo (Wandorobo).

WaDatooga
, kwa jina lingine wanajulikana kama Wamang'ati. Wanapatikana kusini mwa bonde la Ngorongoro. Kuna makabila ambayo wanafanana nayo, au matawi yenye kushabihiana.
Wabajuta
Wagisamjanga (Kisamajeng, Gisamjang)
Wabarabayiiga (Barabaig, Barabayga, Barabaik, Barbaig)
Watsimajeega (Isimijeega)
Warootigaanga (Rotigenga, Rotigeenga)
Waburaadiiga (Buradiga, Bureadiga), ndio hao Watindiga.
Wabianjiida (Biyanjiida, Utatu)

WaDhaiso, au WaDaiso, ni kabila lililoko kwenye Milima ya Usambara katika Wilaya ya Muheza wa Mkoa wa Tanga katika kaskazini mashariki mwa Tanzania. WaDhaiso wana mahusiano ya karibu sana na WaSegeju.

WaGorowa
, wanapatikana Dodoma na Mkoa wa Manyara. (Cushitic language )

WaJiji, kabila linalopatika Ujiji Kigoma. Ila wanawekwa kundi moja na WaHa.

Wakisankasa, wanapatikana Kaskazini mwa Tanzania. Wakati mwingine wanafananishwa au kuwekwa kundi moja na Wandorobo.

NB:
Hayo yote ni makabila mkuu, haijalishi ukubwa au udogo wao, kila kabila lina haki ya kutambuliwa uwepo wake, hata kama wamemezwa na makabila makubwa.

Kila kabila hapo juu, kuna link ambayo inaweza kukusaidia kupata maelezo zaidi.
 
Mkuu umesahau kabila la Wambugu (not Mbugwe who are found in Babati). Hawa wanapatikana West Usambara Mountains eneo la kijiji kinaitwa Lukozi (ilipo ikulu ya raisi Lushoto). Kwa wale waliosoma shule ya sekondari Magamba watakuwa wanawaelewa hawa watu vyema maana iliyokuwa Magamba Secondary (sasa ni University College ya chuo cha Tumaini kwa jina la SEKUCO) ipo katika eneo wanaloishi. Wanazungumza lugha ya asili ya Cushic (kama ki-iraqw/mbulu). Ila ni wachache sana na as of now wako katika hatari ya kumezwa na makabila ya Wasambaa na Wapare. Wakiwa hadharani hupenda kuzungumza Kipare zaidi na sababu kubwa ni kwamba kabla hawahamia milima ya Usambara walishawahi kuweka makao katika milima ya South Pare na ndipo walipojifunza kipare hapo na kwenda nacho Usambara.
Source plz??? I have never heard some of the tribes mentioned, like those in red. Some of the mentioned tribes are not tribes as such but clans within a tribe. Some of the mentioned are "extinct", i.e. they have integrated themselves into bigger ones.
 
Ninawashukuruni nyote ambao mmechangia. Ni habari ambayo Watanzania tulipaswa kuijua na watoto wetu kusomeshwa historia na sociolojia ya Watanzania.
Hilo lo kabila moja kumezwa na kabila jengine pengine ni kutokana na ukaribu wao kiutamaduni na kiisimu. Linalonipa hofu ni kwa baadhi ya makabila kufa au kuwa katika hatari ya kupotea kabisa. Jamii ya Watanzania tunalielewa hili? Inashangaza "wasomi wetu" na wataalamu wengine wanashughulikia utafiti wa viumbe wengine kama vile vyura wa Kihansi lakini tunasau umuhimu wa makabila, lugha na utamaduni wetu, wa watu wetu.
 
Kuna kabila moja baya sana linaitwa hili lilianzisha 1977 linaitwa MAGAMBA hili hatulitaki TZ , linatumia UDINI kutugawa
 
Back
Top Bottom