Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

........Kama unajua ni vema ungetujulisha asili ya hawa Wasokile.

Kwa upekuzi wangu nimeona wametokana na Malkia wa Kinubi aliyeitwa Nyanseba. Huyu malkia alikuwa Malawi, lakini je huko Malawi ndio kuna hawa wanyasa, na kama tujuavyo asili ya wanyasa ni kama wangoni. Ndio tutakapokuja sema asili ya nyakyusa ni africa kusini.
Doubtless to say, Malawi inayo mahusiano ya karibu sana na Wanyakyusa kama ilivyo kwa Wangoni na Wawemba kule Zambia, lakini kumbuka hata sasa wanyakyusa wa Kyela na wale wa Tukuyu wanayo tofauti kubwa tu, ikiashiria pia tofauti ya asili zao.

Wapo wanyakyusa wenye asili ya Ukinga, Usangu, Malawi kule Karonga (Kumbuka mkoa wa Karonga wanaongea Kinyakyusa na ndicho kinachoitwa Nyakyusa Ngonde). Lakini wengi sana wanaongelea asili kuwa Mahenge.

Inasemekana waliamua kuondoka pale kwa sababu ya vita ya kikabila. Lakini pia majanga ya asili ya mazingira yanawezekana. Ninachojiuliza, ikiwa wanajiita Waluguru kwa asili yao, Mahenge kuna Waluguru?

Naambiwa walianza kuchanja mbuga kupitia kwa Wahehe na Wasangu (ndio maana ni watani zao) kisha wakajichimbia kundi moja pale Suma (pana msitu mkubwa sana wa makaburi - isyeto) ambapo miili ya watu wazima na viongozi wao wengi imelala hata leo - japo hapajapewa tunu kihistoria. Wengine kwa mtawanyiko uliosababishwa na Melele wa Wasangu aliyetumiwa na waarabu kupata watumwa, walijikuta wanakimbilia uelekea wa Zambia na wakajificha milimani ndio Undali na baadaye wakateremkia Rungwe na kukutana na wenzao. Hata pale Suma walitawanyika sababu Melele aliendelea kuwasarandia, mke mkuwa wa kiongozi wao Kyusa akaendelea kusini hadi Masoko, wengine kama Ngosi na wanae wakaenda mashariki. Inadaiwa mpiganaji mmoja Kitunda Mjaba alijichimbia mlimani Livingston. Akaoa wake sita ambao uzao wake ndio kina Mwangosi, Mwakatobe, Mwakajila, Mwandumbya, Mwakipesile (?). Hao waliitwa kwa majina ya mama zao ambao pia kuepusha magonvi kati yao wenyewe kwa wenyewe mzee aliwatawanya akabakia na mke mkubwa Ngosi pale kilimani na wanae, ndio maana ya Mbanyangosi...........

Waliokwenda Masoko na Kyusa waliandamana na Nsasu ambaye alienda Mpata mlimani Kyejo karibuna machimbo ya sasa ya gesi, nao wakaongezeka kwenda Ipinda na Kyela kukutana na wengine waliotokea Malawi na wengine wakaenda Makwale na Matema wakakutana na Wakinga na kuchanganyika. Inasemwa ndi maana hata Kinyakyusa cha Matema, Mwakaleli, Masoko, Kiwira ni tofauti sana, wenyewe wanajuana wanapoongea.

Kuna haja ya kujua zaidi, historia ya watu hawa kwa faida ya vizazi vijavy. Mjerumani MONICA ndiye pekee aliyechimbachimba sana historia na utamaduni wa wanyakyusa, lakini hakutoa nakala nyingi, nadhani ilikuwa ni mfumo wa ripoti na sio kitabu cha kuuza. Hakuna bookshop iliyo na kitabu hicho maana hawakutoa chapa nyingine baada ya yeye kufariki. Alikuwa katika harakati za kutafuta namna ya kueneza Injili kati ya watu hawa.

Leka
 
Mnazungumzia historia ya karibuni yaani baada ya Wanyakyusa kufika maeneo ya ukanda wa juu; Historia ya namna hiii ndiyo inayowafanya watu wafikirie kuwa Zanzibar ina historia ya kale zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote katika mwambao wa Bahari ya HIndi au kwamba historia yetu imeanza miaka mia tatu hivi iliyopita. Wanyakyusa wana historia tofauti sana.. ukitaka kujua historia yenu.. someni historia ya Wanubi!!
 
Mnazungumzia historia ya karibuni yaani baada ya Wanyakyusa kufika maeneo ya ukanda wa juu; Historia ya namna hiii ndiyo inayowafanya watu wafikirie kuwa Zanzibar ina historia ya kale zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote katika mwambao wa Bahari ya HIndi au kwamba historia yetu imeanza miaka mia tatu hivi iliyopita. Wanyakyusa wana historia tofauti sana.. ukitaka kujua historia yenu.. someni historia ya Wanubi!!

Thanx. Wako wako wapi hao wanubi? Pretty naye kawasema hao, ndio leo kusikia maunganiko ya Wanyakyusa na Wanubi. Wanubi si ni Watanznia hao? Pretty anasema wako Malawi?

Leka
 
Au wangonde na wanyakyusa jaribu kutembbelea www.nyakyusa.com
Lol ngumbwike akapote,amapenenga,ikimpumu,ifwefwe,ehndingala,ikitumbwike,ubusipa,imbasa and imbagala,haa Kubinika kupata historia huenda unende vijijini wilaya za Rungwe na Kyela kama unabahati unaweza kuwakuta wazee wakakupa akasumo ingawa kwa kweli wengi wametangulia mbele ya haki,kwa kweli inasikitisha Wanyakyusa hatuna historia yoyote wala kumkumbu ya utamaduni wa Wanyakyusa.Nasikia chanzo chetu ni Mahenge sehemu za Mwaya pia inahisiwa kuwa tuna nasaba na Nguni a.k.a Ngonis

une ngumbwike i ndudndu i sya kulila i ngati.
Nasikia Wanyakyusa asili yao ni maeneo ya Mahenge Morogoro.
Sijui ukweli ni upi.
 
Mnazungumzia historia ya karibuni yaani baada ya Wanyakyusa kufika maeneo ya ukanda wa juu...... ukitaka kujua historia yenu.. someni historia ya Wanubi!!

Mkulu Mwanakijiji naomba utupe shule, au uni PM au hata uni-email (choveki@yahoo.co.uk) kwani hii kwangu ni hobby kubwa sana yaani historia na jiografia ya dunia, na si unajua wa Tz wengi huwa wahadharau sana historia?
 
Wanubi ni watu walioko Southern Sudan.. na zamani utawala wa himaya yao ulifika hadi Misri na hata kuwa na mafarao kule..
 
Thanx. Wako wako wapi hao wanubi? Pretty naye kawasema hao, ndio leo kusikia maunganiko ya Wanyakyusa na Wanubi. Wanubi si ni Watanznia hao? Pretty anasema wako Malawi?

Leka
Mwanakiji Wanyakyusa hawana uhusiano na Wanubi,hata Pretty naye anakosea Wanubi sio Wabantu,jamii ya Wanubi kwa hapa kwetu ni Wajaruo na Waacholi walioko Tanzania,Kenya na Uganda.Mimi najua Wanyakyusa ni jamii ya Wabantu na wana uhusiano na Ngoni. Kutoka kwa madiba
 
Hii mada ni muhimu sana maana naweza kuwa mwenyeji wa Wanyakyusa kwa kupata kitchen pale
 
Hii mada ni muhimu sana maana naweza kuwa mwenyeji wa Wanyakyusa kwa kupata kitchen pale



Oh karibu sana mkwe tukutayarishie nini Unyanfu (wali)au Imbalaga(ndizi)na usije shangaa mama mtu mzima akipiga magoti kukusalimia na akikukwepa kukaa nawe karibu hata siku moja hatakubali mle chakula meza moja ,yeye atakaa mbali au jikoni kwetu hiyo ndo culture ingawaje siku hizi kidogo hawa mama zetu wa mijini wameanza kusahau culture kwa kuukumbatia usasa
 
Oh karibu sana mkwe tukutayarishie nini Unyanfu (wali)au Imbalaga(ndizi)na usije shangaa mama mtu mzima akipiga magoti kukusalimia na akikukwepa kukaa nawe karibu hata siku moja hatakubali mle chakula meza moja ,yeye atakaa mbali au jikoni kwetu hiyo ndo culture ingawaje siku hizi kidogo hawa mama zetu wa mijini wameanza kusahau culture kwa kuukumbatia usasa
Mkuu mambo yakikaa kama ninavyopanga itakuwa haki kukujulisha, bado niko kwenye early stages but hope things to be good. Asante kwa misamiati hiyo hapo ya Unyafu na Imbalaga
 
MC...........`Haya haya lin`goma lya ndandalo liingie.(ngoma ya ndandalo iingie).
Lin`goma...`Badu kubaba.(bado inapashwa moto)
MC............`Mbona mnachelewa?
Lin`goma.....`Mwee kwani manyi mlitukwanyia?(we vipi kwani majani mlituchumia?)
 
Mwalimu...............Ambumbulwise kwa nini jana hukuja shule?
Ambumbulwise.......Nakaa kilasilo kibira alitapika mwalimu.
 
hawa wanyaki walitokea kusini mwa africa, wakijichanganya kabila la kingoni, kwa kuswagwa na wangoni katika maeneo yao ya kuishi, wakati huo wangoni wakibaki kusini mwa tanzania (songea) wanyakyusa walipanda hadi kuja kuweka makazi yao katika maeneo Mahenge mkoani Morogoro, na ndipo baadhi ya vitabu vya makabila na histiria zake vinaonesha kama wanyaki chimbuko lao ni wapogolo, kwa kuwa pogoloz ndiyo wenyeji wa Mahenge
Watu hao tangu asli hawakupenda kukaa bila ardhi ya kutosha kulima na ndipo walipo anza kutelemka taratibu kutafuta ardhi yenye rutuba kwa kilimo hata wakanza safari wakiteremka kuelekea kusini mwa Mahenge kupiti makete,mpaka mwakaleli wilayani Rungwe, wakatawala maeneo yote ya lugombo, kandete, kambasegela, isange, ruangwa, masoko, mpanda mbambo bujesi , lufilyo, mpata, mpuguso, bujonde, ntapisi, ipinda, na maeneo mengine mengi na baadhi ya maeneo yaanza kupewa majina ya machifu wa maeneo hayo kama banyangomo, e.tc
Hao wandali ni pijini wa wenyeji wa baadhi ya maeneo ya mbeya vijijini na baadhi ya wanyaki waliokuwa waki move tokea kusini mwa Mbeya na mashariki yaani Rungwe walikuwa wakitafuta maeneo mengine kwa ajili ya kilimo, ha kukatoke makabiri mengine kama wandari, wanyamanyafu anbao hawa hupatikana sana wilayani rungwe maeneo ya Kiwila na baadhi katumba
 
Mkuu mambo yakikaa kama ninavyopanga itakuwa haki kukujulisha, bado niko kwenye early stages but hope things to be good. Asante kwa misamiati hiyo hapo ya Unyafu na Imbalaga
naloli uli ghwa kukajha kabisaa ughwe usimenye ni ndaghilo sya ijholo eeeee
 
Wabantu wote asili yao Matebeleland kando ya Zambezi river. Hujui kwamba lugha ya makabila mengi ya Nigeria inayo maneno yanayofanana na ya Afrika Mashariki achilia mbali Afrika kusini? Unajitia aibu mwenyewe, wanakupatia shule hapo.Amanyisye na Amanyisye, Amunike na Amulike, Mandela na Mwandela

Lekaga

Wabantu hawakutokea Matabeleland, wametokea Nigeria kaskazini nyanda za Jos na Cameroon ya kusini

Hebu ona hapa

[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Bantu_expansion[/ame]

The Bantu expansion was a millennia-long series of migrations of speakers of the original proto-Bantu language group. This group is hypothesized to have originated from modern day Cameroon. A diffusion of language and knowledge spread among neighbouring populations, and a creation of new societal groups involving inter-marriage spread to new areas and communities. The expansion is taken to have begun after the introduction of agriculture, which would indicate a date of ca. 3000–2500 BC for the early expansion within West Africa, followed by first eastwards and southwards migrations beyond West Africa from about 1500 to 1000 BC.[2]
 
Kwa Wanyakyusa makala ya wikipedia ya Kiingereza ina habari nyingi:
[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Nyakyusa[/ame]

Ina nukuu kutoka vitabu vya kihistoria lakini si kazi ya kitaalamu.

Inataja mapokeo kwamba Wanyakyusa wanasimulia juu ya uhusiano na "Wanubii" lakini haieleweki.
Maana haijulikani ya kwamba watu wa Sudan walifika kusini hivi. Wanyakyusa jinsi ninavyoelewa lugha yao ni Kibantu kabisa - nani anajua zaidi?

Kwa bahati mbaya makala ya wikipedia ya Kiswahili juu ya Wanyakyusa bado ni fupi mno. Labda msomaji fulani anawezakusaidia hapa na kuipanusha.
[ame]http://sw.wikipedia.org/wiki/Wanyakyusa[/ame]
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom