Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Ndani ya nyumba,mume na mke wote mmeajiriwa na kila mmoja ana kazi yake.Inawezekana mshahara wa mume ukawa mkubwa kuliko wa mke au vice versa.Nimekuwa nikisikia akina mama wengi wakisema,mshahara wa mume ndo kila kitu,kuanzia matumizi madogo madogo ndani ya house mpaka yale makubwa ya kimaendeleo,mshahara wa mke hauhusiki,ana uhuru wa kuutumia atakavyo tena bila kuhojiwa.Hili swala limekaaje au ndo utamaduni wetu wa Tanzania?