Major General Mkisi Hatunaye Tena

Kichuguu,

Nakubaliana na wewe. Ila ifike wakati tuwe tunawasema hawa wapuuzi na tumalize hasira zetu na baada ya hapo, tunamuachia Mungu sasa amhukumu. Ndiyo maana nimeweka kilio changu tu na hukumu namuachia mwenyewe.

Asante kwa cheti cha JKT. Mie nafikiri nilikuwa enzi za Makame. Makame alikuja Msange JKT na kukuta hali ya ovyo na akalazimisha kila COY iwe na taa na redio. Akaagiza tuchome Mkaa na kweli within mwezi mmoja, tukawa na redio na taa za chemli.

Alipoenda Msoma sijui kambi inaitwa vipi ile, nasikia alishangaa kukuta RAIA wamezagaa kikosini. Akauliza sasa wanajeshi wako wapi wakamjibu ndiyo hao. Nasikia alikataa kuondoka hadi maroli yaje kutoka makao makuu Dar. Yakaleta nguo, magodoro, vitanda, viatu, kaptura, sox na bila kuzisahau GREEN VEST ZA KIJANI.
 
kichunguu!

Umenikuna kwa hicho cheti. Angalau ungeonyesha operesheni yako ili tujue ulikuwa zama zipi.

Nikiwa Itende kama service man (miaka ishirini ya azimio la Arusha) niliwahi kufika mpaka kijijini kwa Mkisi (igamba) 'kwa shughuli maalum'.

Watu wanabadilika. kama yapo mapungufu yaliyokuwepo enzi zake za kazi, haimaanishi kaondoka nayo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom