Majogo: Baada ya kustaafu marafiki wengi wamenikimbia

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
KITAIFA
By Raymond Kaminyoge

Posted Monday, October 29 2012 at 12:18

IN SUMMARY

"Nawaasa viongozi wa serikali mkiwa madarakani huku mkitembelea magari yenye bendera za taifa, mtazungukwa na marafiki lakini baadhi yao ni wanafiki."

WAZIRI wa zamani, Edgar Maokola Majogo amejitokeza amesema baada ya kustaafu nusu ya marafiki walimkimbia kutokana na kutambua kuwa tena msaada kwao.

Majogo ambaye amekuwa waziri katika wizara mbalimbali, alisema akiwa madarakani alikuwa na marafiki wengi waliokuwa karibu naye.

Akizungumza kwenye kufunga maonyesho ya wajasiriamali Dar es Salaam juzi, Majogo alisema marafiki wanakuwa karibu pindi kiongozi anapokuwa madarakani, wakijua watapata msaada.

"Walipogundua sina cheo tena serikalini walinikimbia mmojammoja," alisema Majogo na kuongeza:

"Nawaasa viongozi wa serikali mkiwa madarakani huku mkitembelea magari yenye bendera za taifa, mtazungukwa na marafiki lakini baadhi yao ni wanafiki."

Alisema wengi wataonyesha unyenyekevu lakini baada ya kustaafu watashangaa hawaonekani.

Alisema jambo la msingi kwa viongozi na wananchi wanatakiwa wanapokaribia kustaafu wajiandae kuwa wajasiriamali.

"Watu wafahamu kwamba kuna muda wa kustaafu na wajiandae kwa hilo, kwa kuanza kuwa wajasiriamali," alisema Majogo.

Akitoa mfano wake, alisema baada ya kustaafu aliomba mkopo benki na kuanza ujasiriamali na hivi sasa ana kiwanda cha kubangua korosho.

"Niliweka dhamana nyumba yangu nisiporudisha mkopo kwa wakati, nyumba inaweza kuuzwa ili kulipia mkopo huo," alisema.

Majogo alisema kiwanda hicho kilichopo Dar es Salaam kimetoa ajira kwa zaidi watu 100, wengi wao wakiwa wanawake.

"Kwahiyo ukijiandaa mapema baada ya kustaafu utaishi maisha ya raha na starehe," alisema Majogo

Alishauri serikali kuandaa utaratibu wa kuvisaidia vikundi vya wajasiriamali ambavyo vimeonyesha uwezo wa kujiendeleza kupambana na umaskini.

Inamaanisha, ukistaafu ukiwa MWANACHAMA wa CCM ni kosa kubwa to MOVE on hata kama UNATAKA UBUNGE tena lazima Ugombee ndani ya CCM; Ukigombea NJE na USHINDWE ina Maana Marupurupu na pesa za peremende zote hata kama ni kidogo na hizikutoshelezi zinapotea... Kila UKIENDA ni kama UMEFUTIKA hawakujui... that's how CULT BUSINESS is doing it is DICTATORSHIP.

Sasa, Angalia THOMAS NYIMBO na yeye kajirudia CCM - Inaonyesha NGUVU zote za KIUCHUMI zinakukimbia pia

CCM inakuua vibaya hata kama wewe ni MZEE Inaonyesha ni BORA CCM ikuweke JELA kuliko wewe kufungasha virago na KUHAMIA UPINZANI...
 
Na hasa ukistaafu ukiwa huna kitu, lazima wakimbie wanajua itakuwa zamu yao kuombwa msaada.
 
Inategemea alikua na marafiki wa aina gani. Kama alichagua marafiki kwa misingi ya vyeo na pesa vikiondoka wengine wanaondoka navyo. Kama ukiwa mtu wa watu hata ukifa utaendelea kuwa miyoni mwao. Huyu Mzee nakumbuka alipewa wizara yenye jukumu la kupambana na umasikini wakati wa Mzee Mkapa, akawa busy kupambana na maskini wa Masaki, Ostabei,na mbezi beach. Wale maskini wa kwa mtogole, yombo, manzese na maeneo mengine kama hayo hakua na mda nao kabisa. Sasa wale waliomfuata kwa sababu ya cheo chake wamekimbia. Hili nadhani ni funzo kwa watu wanopata nafasi wakawasahau watu wa chini nao siku wakirudi chini watasahaulika hivyo hivyo.
 
ukistaafu uwe mjasiria mali??aisee!hii nchi kiboko,hivi inawezekana mtu anapostaafu awe mwalimu wa kujitolea shule iliyo kijijini kwake?au afanye kazi za umma za kujitolea
nilimwona mzee mmoja alikuwa meneja wa tanesco pale iringa alikuwa anaishi maisha mazuri lakini alipostaafu aliteseka sana
inabidi tujifunzie hapo
 
KITAIFA
By Raymond Kaminyoge

Posted Monday, October 29 2012 at 12:18

IN SUMMARY

"Nawaasa viongozi wa serikali mkiwa madarakani huku mkitembelea magari yenye bendera za taifa, mtazungukwa na marafiki lakini baadhi yao ni wanafiki."

WAZIRI wa zamani, Edgar Maokola Majogo amejitokeza amesema baada ya kustaafu nusu ya marafiki walimkimbia kutokana na kutambua kuwa tena msaada kwao.

Majogo ambaye amekuwa waziri katika wizara mbalimbali, alisema akiwa madarakani alikuwa na marafiki wengi waliokuwa karibu naye.

Akizungumza kwenye kufunga maonyesho ya wajasiriamali Dar es Salaam juzi, Majogo alisema marafiki wanakuwa karibu pindi kiongozi anapokuwa madarakani, wakijua watapata msaada.

"Walipogundua sina cheo tena serikalini walinikimbia mmojammoja," alisema Majogo na kuongeza:

"Nawaasa viongozi wa serikali mkiwa madarakani huku mkitembelea magari yenye bendera za taifa, mtazungukwa na marafiki lakini baadhi yao ni wanafiki."

Alisema wengi wataonyesha unyenyekevu lakini baada ya kustaafu watashangaa hawaonekani.

Alisema jambo la msingi kwa viongozi na wananchi wanatakiwa wanapokaribia kustaafu wajiandae kuwa wajasiriamali.

"Watu wafahamu kwamba kuna muda wa kustaafu na wajiandae kwa hilo, kwa kuanza kuwa wajasiriamali," alisema Majogo.

Akitoa mfano wake, alisema baada ya kustaafu aliomba mkopo benki na kuanza ujasiriamali na hivi sasa ana kiwanda cha kubangua korosho.

"Niliweka dhamana nyumba yangu nisiporudisha mkopo kwa wakati, nyumba inaweza kuuzwa ili kulipia mkopo huo," alisema.

Majogo alisema kiwanda hicho kilichopo Dar es Salaam kimetoa ajira kwa zaidi watu 100, wengi wao wakiwa wanawake.

"Kwahiyo ukijiandaa mapema baada ya kustaafu utaishi maisha ya raha na starehe," alisema Majogo

Alishauri serikali kuandaa utaratibu wa kuvisaidia vikundi vya wajasiriamali ambavyo vimeonyesha uwezo wa kujiendeleza kupambana na umaskini.

Mzee Majogo style za kustaafu ukiwa na hali kama uliyostaafu wewe ni enzi hizo, leo hii Mawaziri wenzio wanastaafu wakiwa na mabilioni ya pesa wanayaweka Uswisi.
 
Hii karne wastaafu wanakuwa mabilionea sio tena wajasiliamali ila niwatumiamali wakubwa na utajiri mkubwa wa kutisha!Ngeleja ana haja gani kuwa mjasiliamali?labda ajiite tu mjasiliamali akiwa anamiliki hotel za ghorofa 7 kila (Dar ,Mwanza na Arusha)...wamejilimbikizia vya kutosha
 
Mamkumbuka huyu mzee wa party,alisikia dodoso kutoka kwa hao marafiki wake ya kuwa anakuwa balozi france,mzee akaangusha bonge la pati,kilichofuata akapigwa chini,akaja chinga mwenzake akamuokota,nakumbuka ile nyumba yake alimpangisha mjasiriamali mmoja aitwaye abba Mwakitwange.
 
Inategemea alikua na marafiki wa aina gani. Kama alichagua marafiki kwa misingi ya vyeo na pesa vikiondoka wengine wanaondoka navyo. Kama ukiwa mtu wa watu hata ukifa utaendelea kuwa miyoni mwao. Huyu Mzee nakumbuka alipewa wizara yenye jukumu la kupambana na umasikini wakati wa Mzee Mkapa, akawa busy kupambana na maskini wa Masaki, Ostabei,na mbezi beach. Wale maskini wa kwa mtogole, yombo, manzese na maeneo mengine kama hayo hakua na mda nao kabisa. Sasa wale waliomfuata kwa sababu ya cheo chake wamekimbia. Hili nadhani ni funzo kwa watu wanopata nafasi wakawasahau watu wa chini nao siku wakirudi chini watasahaulika hivyo hivyo.

Haswaa, kama ulikuwa na marafiki waadilifu kama wewe sasa hivi wamekengeuka Azimio la Arusha.
Kama ulikuwa na marafiki wanapata kilaji sasa hivi wameokoka ni Mitume na Manabii.
Kama ulikuwa na marafiki mkiwa wote na Land Rover 109, sasa hivi wenzio wanamiliki HARMMER.
Kama ulikuwa na marafiki mkiishi Oysterbay sasa hivi wenzio wanamiliki Village Villas zao hapahapa Bongo.
Kama ulikuwa unamiliki shamba la urithi wenzio leo wanamiliki maelfu ya ekari sawa na wilaya yako ya Masasi tena bila aibu.
Na mengine mengi.
 
inategemea alikua na marafiki wa aina gani. Kama alichagua marafiki kwa misingi ya vyeo na pesa vikiondoka wengine wanaondoka navyo. Kama ukiwa mtu wa watu hata ukifa utaendelea kuwa miyoni mwao. Huyu mzee nakumbuka alipewa wizara yenye jukumu la kupambana na umasikini wakati wa mzee mkapa, akawa busy kupambana na maskini wa masaki, ostabei,na mbezi beach. Wale maskini wa kwa mtogole, yombo, manzese na maeneo mengine kama hayo hakua na mda nao kabisa. Sasa wale waliomfuata kwa sababu ya cheo chake wamekimbia. Hili nadhani ni funzo kwa watu wanopata nafasi wakawasahau watu wa chini nao siku wakirudi chini watasahaulika hivyo hivyo.

hata hivyo nafikiri anawalilia haohao maskini wa masaki, mikocheni,.......... Na sio wa manzese, buguruni, kwa mtogole.... Hawa hawana mvuto kwake.
 
ndo analijua leo?

Alikuwa hajui anapaswa kuwa makini na uchaguzi wake wa marafiki wakati akipanda na kuwa juu maana atawahitaji akiwa chini?

Imekula kwake
 
Inaelekea baada ya kupata vyeo aliona watu aliokuwa nao mwanzo si daraja lake na hilo tatizo tunalo wengi wetu baada ya kupata mafanikio tunasahau watu tuliokua nao tunaambatana na watu wengine ambao kiukweli wanakuangalia watafaidikaje kutokana na mafanikio au nafasi uliyokuwa nayo ndio maana alipoondoka madarakani wakamkimbia kwani hakuwa na msaada wowte kwao
 
Wapambe wamemkimbia...wapambe wanaenda kwa maslai sio hivihivi.!
 
Kuna mshua alinihadithia alienda kumtembelea rais Mwinyi (rais Mwinyi aliwahikumteua katika nafasi kubwa kwenye utawala wake). Basi alipofika kwa Mwinyi, Mwinyi akawa kama anamlalamikia watu wamemsahau, maisha ya urais na ya kustaafu tofauti. Mshua akamwambia sio wote tumekusahau, wengine tunakukumbuka Mzee.

Sasa kama watu wamemsahau Mwinyi, Majogo kusahauliwa siwezikushangaa.

Yeye apige hela kwenye korosho tu.

Na hivi Magufuli kasikia atatuma watu wafuatilie kama analipa kodi.
 
Back
Top Bottom