Majirani...

Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,220
4,056
Nimekuwa nikijaribu kufikiria maisha ya nyuma niliyoyaishi na ya sasa na naona kama kwa sasa nipo kwenye ulimwengu tofauti kabisa. Nimezaliwa na kukulia katika mazingira ya kawaida, ambapo nilikuwa na interactions sana na majirani. Nilikuwa nikicheza, kula na hata siku nyingine kulala kwa majirani.

Miaka hii nashangaa hii hali siioni kabisa. Nimekaa mtaa huu kwa zaidi ya miaka 5, Jirani zangu sifahamiani nao zaidi ya kuona magar yakiingia tu ndani na kutoka. Watoto nao wamekuwa busy na shule na wakitoka ni computer na TV tu, na hawana interactions na wenzao kama ilivyokuwa miaka yetu.

nyie kwenu vp jaman, ni mtaa wetu tu au na hii hali kwenu ipo?

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Yeah, kuna mabadiriko makubwa zama hizi; in short tunaiga 'uzungu' na kuacha tamaduni zetu za Ki Afrika. Mambo ya utandawazi yametuathiri sana!
 
duh,mie huwa nakutana na majiran kwenye matukio. naifahamu familia iliyo kulia kwangu na kushoto. nyumba ya 2 na 3 hata siwahafamu kwa majina zaidi ya sura. . . zamani tulipokuwa watoto tulikuwa tunacheza kwa kushindana mtaa huu na mtaa wa pîli. afu pia karibu mji mzima tulikuwa tunafahamiana, lakin siku hizi weng tumehamia mji ambayo hatukuzaliwa kwa hiyo hatufahamiani na hata wanetu hawafahamian wapo busy na shule.
 
Nashangaa hata kwenye matukia kama misiba, sherehe hata hatuambiani!! uanasikia tu kwa jirani wanasherekea au wanalia, but you are not given any information...halafu tena ukizingatia miaka hii kujipendekeza nayo shidaa!!
 
Ujamaa ulikuwa na raha zake na mojawapo ilikuwa ni hii ya undugu,tofauti na sasa tumefikia mpaka kupeana kadi kwenye misiba...
 
Yeah, kuna mabadiriko makubwa zama hizi; in short tunaiga 'uzungu' na kuacha tamaduni zetu za Ki Afrika. Mambo ya utandawazi yametuathiri sana!
Huu utandawazi umetuharibia sana!!! Ukifulia unamkosa hata jirani wa kumpiga mzinga..dah!
 
Mimi naona huku kuna mshikamano sana hasa kwa kuwa nimeishi na watu primitive hasa. Huwezi kumsalimia ama hata kupiga story na mweupe. Ukienda mitaa ya weusi kama philedalphia au brooklyn na maeneo ya boston pia na pennyslavania ni utata kwa white
 
Ujamaa ulikuwa na raha zake na mojawapo ilikuwa ni hii ya undugu,tofauti na sasa tumefikia mpaka kupeana kadi kwenye misiba...
Dah! Na kukodi watu wa kulia misibani! Unapatwa na janga, huna jirani wa kukusaidia na kukufariji. Inabidi uingie tu garama za kuwakodi watu!!
 
maisha yamebadilika ni mchakamchaka na kukimbizana na shilingi..... Hapa mtaani majirani ninao wafahamu ni wachache wanaonizunguka na wengine ninaosali nao jumuia maana Kwa sisi wakatoliki angalau jumuia zimesaidia kujuana kutokana na kusali kila jumamosi.......

Ila kwa majirani waliobakia ilinichukua muda kuwajua majina, na kuonana ni mara chache sana..... Hivyo usimlaumu jirani yako asipokualika sherehe, ila msiba hauna mwaliko.....
 
Mbona sisi uswazi kwetu mambo ya ujirani yapo sana tu...
Mambo ya kuombana chumvi, moto wa kukolezea mkaa, ungo wa kupepeta mchele, sometimes majirani huwa wanakuja kuchuma matembele home...huku kwetu michezo kama ukuti, kombolela n.k bado ipo kwa sana
 
Maisha uliyoishi mtoamada it's same with me .
Tukubali tu global ndiyo imekuja kutofautisha life ile na hii .
Mf. Sisi tulikua tunatumwa kupeleka mahindi kusaga unga mashineni !
Leo hii watoto wetu hawajui kama unga husagwa wapi .
Zamani Mwl alikua ni mtu mwenye kuheshimika kuliko polisi ! Now days kinyume chake.
Bt ukiniambia niseme maisha yale na haya , yepi mazuri ?
Nitasema YALE na si HAYA .
 
BADILI TABIA, kwani miaka hiyo watu walikuwa hawazitafuti shilingi? Bora wewe una kitu cha kuwakutanisha angalau mara moja kwa wiki!!
 
Last edited by a moderator:
Mbona sisi uswazi kwetu mambo ya ujirani yapo sana tu...
Mambo ya kuombana chumvi, moto wa kukolezea mkaa, ungo wa kupepeta mchele, sometimes majirani huwa wanakuja kuchuma matembele home...huku kwetu michezo kama ukuti, kombolela n.k bado ipo kwa sana
Hahahahaha....umenifurahisha sana watu8, haya ndio maisha nayotamani kuyaishi!!!
 
Last edited by a moderator:
Maisha uliyoishi mtoamada it's same with me .
Tukubali tu global ndiyo imekuja kutofautisha life ile na hii .
Mf. Sisi tulikua tunatumwa kupeleka mahindi kusaga unga mashineni !
Leo hii watoto wetu hawajui kama unga husagwa wapi .
Zamani Mwl alikua ni mtu mwenye kuheshimika kuliko polisi ! Now days kinyume chake.
Bt ukiniambia niseme maisha yale na haya , yepi mazuri ?
Nitasema YALE na si HAYA .
Siku hizi hata mtoto hatumwi dukani, achilia mbali mashine!! Wazazi + hg ndio mnafanya shopping ya kila kitu. Nakubaliana na wewe, maisha yale yalikuwa mazuri kuliko haya!!
 
Zamani giza likikukuta ukiwa mbali na kwako unaenda kwa mjumbe unajitambulisha na utapewa chakula na pa kulala lakini si siku hizi. Zamani vichekesho tulikuwa tunapeana wenyewe bure kabisa lakini leo lazima ulipie ili Evansi Bukuku akuchekeshe. Siku hizi TV/GAME oriented families families utajuwa tu, hawana stori na wanaongea kwa step. Kifupi social life kwao ni kumbi za starehe tu na kushindana bila kuambiana kama kuna mashindano ya kumiliki kila kitu ghari...
 
Siku ambayo nilipishana na jeneza linaingizwa nyumbani kwa jirani yangu ndio nikagundua kweli naishi mjini! Nikajiuliza nisimame, niingie na kujikalisha ama vipi? Mwenye nyumba sijawahi kukutana nae hata sura yake simjui na gari yake siijui. Si ndio mwanzo wa kuitwa mchawi, kutokea msibani kama radi?
Hatua niliyochukua ni kuhakikisha niko karibu na ndugu zangu. Najua hapa nikipata tatizo ni simu tu! Sio utaratibu mzuri kiukweli!
Ujamaa ulikuwa na raha zake na mojawapo ilikuwa ni hii ya undugu,tofauti na sasa tumefikia mpaka kupeana kadi kwenye misiba...
 
Siku ambayo nilipishana na jeneza linaingizwa nyumbani kwa jirani yangu ndio nikagundua kweli naishi mjini! Nikajiuliza nisimame, niingie na kujikalisha ama vipi? Mwenye nyumba sijawahi kukutana nae hata sura yake simjui na gari yake siijui. Si ndio mwanzo wa kuitwa mchawi, kutokea msibani kama radi?
Hatua niliyochukua ni kuhakikisha niko karibu na ndugu zangu. Najua hapa nikipata tatizo ni simu tu! Sio utaratibu mzuri kiukweli!
Ndugu wenyewe nao siku hizi wanashikika? Bora hata uanze kujikomba kwa majirani...lol!
 
ni hatari na aibu huwa naona pia! simjui hata wa pembeni yangu kulia na kushoto maana ni nyumba za kupanga, wanakuja leo baada ya miezi 6 wameondoka wamekuja wengine! jirani mpangaji alijifungua twins last month, nimetoka job twins wangu nao wananitaarifu kuwa wameona barbies, lakini barbies wao wanalia na kunyonya, nikawauliza wapi, wakanijibu dukani! hiyo familia ina kaduka kwa mbele japo wamepanga. nikatafuta vizawadi same evening tukaenda, cha ajabu waliniambia wako hapo wana mwaka wa 3 wamepanga! na wao hawanijui, basi ukawa ni mwanzo wa kujuliana. ila kwa kweli tunakokwenda, sio kabisaaaaaaaaa! watoto wetu watakuja oana ndugu wallah!
 
Maisha yamekuwa ya dot.com tu kwa wote mie hata jirani simjui anafananaje........

Zamani mnakwenda kucheza chakula kinapikwa kwa jirani mnakula, mnaoga, mnalala huko siku hizi thubutu utaanzia wapi ukienda kwa jirani watoto wako busy na computer hata kukusalimu mgeni ni issue lakini ndo hivyo maendeleo
 
Back
Top Bottom