majina ya kizungu hamtaki, mbona kizungu mmeiga?
wapo baadhi wanaongea hicho kiswahili. lkn sijawahi kuona shule au chuo cha kizungu wanafundisha masomo yao kwa lugha ya kiswahili. Tanzania sasa hivi shule zote ni english tu kuanzia chekechea hadi chuo. shule pekee zilizobaki kufundisha lugha ya kiswahili ni shule za primary za serikali tu.Kwani hamna wazungu wanao ongea Kiswahili dada?
Takauchi, Kayashika, Takahara
majina ya kizungu hamtaki, mbona kizungu mmeiga?
Mziwanda (maana yake mtoto wa mwisho, wengine huita kitinda mimba) hii imekaa vizuri sana, unanikumbusha wakati ninasoma kulikuwa na stori nilihadithiwa na jamaa yangu, aliniambia alikuwa na jamaa yake alienda Ulaya kusoma, jamaa alikuwa anaitwa Daudi Ndege, sasa kwa kupenda kwake uzungu aliporudi nyumbani alianza kujiita Dav Bird, sasa jamaa zake wakashindwa kulitamka hilo jinale jipya na kuishia kulibadili kabisa na kumuita Davibade! Unajua haya majina ya kizungu hasa ya kiingerza ambayo watu wengi hupenda kujipachika ukitafsiri maana yake kwa kiswahili hakuna ataye penda tena kujiita. Mfano mwingine kuna yule jamaa anetoa simulizi zake katika kipindi cha sinto sahau, anajiita ROGERS, nimeambiwa eti jina lake halisi ni RAJABU, sasa hebu tazama kapoteza kabisa maana ya jina! Kisa Uzungu