Majina yetu jamani

Hodi!! naingia ilikuungana nanyie kweli tunaenda wapi? . majina tunayo mazuri na yanamaana nzuri .kwani jina hujiiti ?unaitwa na wazazi,wako. na ukikua unlibadilisha kwamatakwa yako je.?yule aliekuita anajisikiaje?. inamaana wewe unaona alikosea?. kwa kukuita jina hilo? pia majina mengine nikumbukumbu ya wazazi wetu. leo unalifuta je?.unawapenda wazazi wako? hilo tulitazame .vinginevyo tutapoteza utamaduni wetu bila kujua.wewe unaona jambo dogo kumbe kidogo huzaliwa na kikubwa.

We baba yako alikuita Kamjingijingi?
 
Napenda kutolea mifano humu jamvini. Nyani ngabu, Mziwanda, Mzee Mwanakijiji, Kibunango, Kichuguu, Bubu…, Mzizi mkavu, Mbu, Visenti, MwanaFA, Masanilo, Kuntakinte, Kizimkazimkuu, Msanii, Dingiswayo, (sitawamaliza)
Dah,

Najiona mwenye hatia. Sijui nitumie jina gani?
 
Kweli ni aibu kubwa sana kwa Mwafrika kutokuwa na jina hata moja la kiafrika, ila na dhani mmeangalia upande mmoja wa kwenye majina ya majina ya kizungu. Vipi kwnye majina ya kiarabu!!?? utakuta mtu anaitwa Haroub Othman, Ali Hasan, Fatma Salim, Aubakar Sadik, hii ni fedheha kubwa kwetu!!
 
Asante KAKAJAMBAZI.ukweli nihuo sijabadili jina langu tena nalipenda sana. sijui kama itatokea nibadilike .sababu binaadam hatujui tuendako. KAKAJAMBAZI je?hili lako umelipataje?!!!!!!!!!
 
Pole sana "mziwanda" - kwanza kabisa naona nikusahihishe, hayo sio majina ya kizungu, ukiangalia kwa undani sana haya majina ni ya kidini yaani "christian names" na udini hauna mzungu wala mwafrika - we belong to same Jesus. Sioni ubaya mtu kujifananisha na watu mashuhuri kama vile Paul, John, Samwel, Job, Elia, Sarah, Ibrahim n.k.

Sisi watanzania ndio bora zaidi ya wa-kongo maana tuna mchanyato wa majina yooote. Mfano: John Cigweyemis Malecela, Jakaya Mrisho Kikwete, Peter Kayanza Pinda, John Pombe Magufuli, Edward Ngoyaiye Lowasa, Julius Kambarage Nyerere (RIP), John Bamsifile Mwakajumba, etc. sasa wewe unataka nini tena zaidi ya haya majina mazuri namna hii. I am sure we are better than Kongo's.

Kuhusu haya majina ya JF, usihofu maana yote haya ni a.k.a (also-known-as), kila mtu hapa ana jina lake alililopewa. Ukiyataka waulize watakupa na utayafurahia.
 
..........
'''''''''''' idadi kubwa ya watanzania tuwe na majina ya asili yetu. ............. Ukarimu huanzia nyumbani.

MZIWANDA,
Cha msingi katika jina ni maana iliyokusudiwa na siyo asili.
Unaweza kusikia majina ya asili ya kitanzania kama SHASHATA, ITEITEI, NGOSHA, FISWANU, lakini maana zake zaweza zisipendeze sana kwa wahusika.
 
Kuna mambo ambayo ukitayatazama kijuujuu utaona kuwa ni madogo sana hasa katika kipindi hiki cha utandawazi. Hayo madogo kwa wingi wake ndio yanayofanya vitu vikubwa. Napenda kuzungumzia majina watu wanayopewa kutokana na jamii wanazotoka.

Ukitazama au kusikiliza majina mengi ya raia wa kikongo, mengi ni ya asili. Sina sababu ya kuyataja kwani kila mtu anayajua. Sijajua kama bado wanawapa wanao majina ya asili. Ni kitu cha kujivunia. Hii ilikuwa ni kampeni ya kitaifa huko Congo. Hapa ninachoshangaa ni kwamba, Mobutu aliwezaje kuyakataa majina ya kizungu na akakubali kuwa kibaraka.

Ukiangalia kwa undani zaidi na kuvuka mipaka ya Congo na Afrika, utafika Marekani. Wengi wa wamarekani weusi wana majina ya kizungu. Ukisikia jina tu bila ya kumwona mhusika hutajua asili yake. Niliposoma kitabu cha Booker T Washington- Up from slavery (uk. 24), niligundua kuwa wamarekani wengi walijipa majina wenyewe ama kupewa na ‘mabwana' wao. Booker alijulikana kwa jina hilo tu ila alipoanza shule alikuta wenzake wana majina zaii ya moja, hivyo mwalimu alipomuuliza anaitwa nani alijropokea tu-Booker Washington. Na ndio yakawa majina yake. Halafu alikuja gundua kuwa mama yake alimpa jina la Taliaferro alipokuwa mdogo, akaliongeza na kujiita Booker Taliaferro Washington (Booker T Washington)

Ikanikumbusha pia Kuntakinte. Kwamba, wazungu hawakuyapenda majina ya kibantu. Ni pale Kuntakinte alipokuwa akipigwa mijeledi ili akubali jina la kizungu (silikumbuki). Mwisho wa siku alilikubali baada ya kichapo kikali! Kuna wasaa ulinifanya nifadhaike sana. Nashukuru nilikuwa peke yangu wakati natazama hiyo filamu. Pale yule mzee alipomwambia pale chini alipolala kwa maumivu, naye akitokwa machozi, "No matter what they call you. You will remain Kuntakinte". Nilifadhaika.

Sasa najiuliza, hii kasumba ya majina ya kizungu ni ya nini? Mbona wao hawajiiti majina yetu ya kibantu? Watanzania wengi hubadilisha majina yao angalau yafanane na ya kizungu. Japo si katika maandishi, basi matamshi. Heko kwa wale walio na majina ya asili, au hata kama si ya asili basi yanayotamkika Kiswahili kama Joni, Samweli, Daudi, Yohana, Mariki n.k. nadhani majina ya kiitaliano huwa mnayasikia. Heko pia kwa wale wenye majina ya bandia ya kiasili. Napenda kutolea mifano humu jamvini. Nyani ngabu, Mziwanda, Mzee Mwanakijiji, Kibunango, Kichuguu, Bubu…, Mzizi mkavu, Mbu, Visenti, MwanaFA, Masanilo, Kuntakinte, Kizimkazimkuu, Msanii, Dingiswayo, (sitawamaliza)

Changamoto kwa akina Invisible, Field Marshall, Wos, Next level, Pretty, Fidel, Allien, Sasha Fierce, Lazy dog, Game theory, na wengine wengi.

Ningetamani kusikia wale wamarekani weusi wanajiita majina ya asili yao (Afrika). Na idadi kubwa ya watanzania tuwe na majina ya asili yetu. Tusijidanganye na majina ya magharibi nay a watakatifu na ya Mashariki ya kati. Ukarimu huanzia nyumbani.

Kuna vitu vingi vinanavyoweza kumtambulisha mwafrika.
Mkuu wewe umeona majina tu?? mambo mengine je? umeisha jiuliza enzi zile wazee wetu walikuwa na utaratibu gani wakati wa kula? uvaaji wanguo?? malezi kwa watoto? kutafuta mchumba mpaka ndoa? ndoa zilikuwa zinafungwaje?? kuabudu?? majirani walikuwa wanaishi vipi?? kulinganisha na sasa??
Nafikiri majina ni sehemu ndogo,tubadilishe kila kitu kiwe cha kiafrika kama tunataka kurudi kule kitu ambacho ni ndoto.
 
Pole sana "mziwanda" - kwanza kabisa naona nikusahihishe, hayo sio majina ya kizungu, ukiangalia kwa undani sana haya majina ni ya kidini yaani "christian names" na udini hauna mzungu wala mwafrika - we belong to same Jesus. Sioni ubaya mtu kujifananisha na watu mashuhuri kama vile Paul, John, Samwel, Job, Elia, Sarah, Ibrahim n.k.

Sisi watanzania ndio bora zaidi ya wa-kongo maana tuna mchanyato wa majina yooote. Mfano: John Cigweyemis Malecela, Jakaya Mrisho Kikwete, Peter Kayanza Pinda, John Pombe Magufuli, Edward Ngoyaiye Lowasa, Julius Kambarage Nyerere (RIP), John Bamsifile Mwakajumba, etc. sasa wewe unataka nini tena zaidi ya haya majina mazuri namna hii. I am sure we are better than Kongo's.

Kuhusu haya majina ya JF, usihofu maana yote haya ni a.k.a (also-known-as), kila mtu hapa ana jina lake alililopewa. Ukiyataka waulize watakupa na utayafurahia.

Suala sio mchanyato wa majina mkuu. ni uwiano au ulinganifu. ndio maana Sembene Ousmane aliandika kitabu chake na kukiita 'God's bits of woods'. Yaani sisi ni mabaki mabaki tu, mchanganyiko usio rasmi. muislam huko huko, mkristu huko huko, mweupe, mweusi, mzuri, mbaya, chotara, na kila zagazaga. sasa kwa vile sie ni mchanyato, basi unataka kuhalalisha huu mchanyato?
 
MZIWANDA,
Cha msingi katika jina ni maana iliyokusudiwa na siyo asili.
Unaweza kusikia majina ya asili ya kitanzania kama SHASHATA, ITEITEI, NGOSHA, FISWANU, lakini maana zake zaweza zisipendeze sana kwa wahusika.

sasa huko ndiko kujikataa. tunataka majina kama prince, freddy, woods, n.k nadhani ndicho unachomaanisha
 
Kuna vitu vingi vinanavyoweza kumtambulisha mwafrika.
Mkuu wewe umeona majina tu?? mambo mengine je? umeisha jiuliza enzi zile wazee wetu walikuwa na utaratibu gani wakati wa kula? uvaaji wanguo?? malezi kwa watoto? kutafuta mchumba mpaka ndoa? ndoa zilikuwa zinafungwaje?? kuabudu?? majirani walikuwa wanaishi vipi?? kulinganisha na sasa??
Nafikiri majina ni sehemu ndogo,tubadilishe kila kitu kiwe cha kiafrika kama tunataka kurudi kule kitu ambacho ni ndoto.

sivyo kama unavyofikiri. hujayachambua mambo kiundani ndugu. pia usikate tamaa kiivyo. ukiamini hivyo utaamini pia kuwa ukimwi hautaisha
 
Majina ya kigeni ni ishara ya kuwa bado tuna mawazo ya kitumwa.
Na jambo gumu kuliko yote ni kukubali kuwa bado tuna mawazo ya kitumwa.
Hadi leo hii wajapani, wachina, nk wanatumia majina yao ni kwa sababu wameondoa fikra za kitumwa.
Majina ya kiafrika ni bora zaidi.
 
Ndio maana nawakubali Wachina. Wazungu through history and different mechanisms, wameharibu kabisa thinking yetu waafrika.
 
...nashukuru hakuna wanaojiita majina ya "kijapani", mnh! :(
 
Tatizo tumeshindwa kuwathamini, mashujaa wetu na kukumbatia mashujaa wa wenzetu.

Historia ya Tanzania ina mambo mengi sana ya kujivunia, lakini leo hii ni wangapi wanaweza kuelezea historia ya Tanzania kabla ya kuja wageni.

Tuna makabila zaidi ya 120, je katika makabila hao hakuna hata watu wa kujivunia, watu ambao tungeweza kuwatungia Ngano, mashahiri ngonjera na michezo ya kuigiza?

Tunakumbatia majina ya kishujaa ya kigeni kwa kukosa kwetu ufahamu wa kutambua michango ya wale waliokuwa kabla yetu. Nakumbuka enzi zile za shule, kuna baadhi ya vijana walikuwa wanajinasibisha na majina ya kizulu, na hii ilitokana na usomaji wa vile vitabu maarufu vya H. Rider Haggard. Kuna walio jiita kina Umbopa, Nkomabakosi, Umslopogaas... nk. Hii yote ilitokana na msomaji kupatwa na msisimko wa hivyo vitabu vya mtunzi huyo mahiri Muingereza.

Sisi wasomi wetu hawakuliona hilo na wala hawakulizingatia. Baadhi tu ndio baada ya uhuru wakaja na simulizi chache ambazo walitumia majina ya kiasili ya Kitanzania. Nakumbuka simulizi ya kina Mzuri Kwao, kina Kibanga, na wengine wachache. Walisahau kuwa watu uvutiwa kuwaita vijana au watoto zao kutokana na kusikia ushujaa na busara za watu mbali mbali, hususani waloko kwenye jamii yao.

Suala la majina wakati mwingine uhathiriwa sana na imani tulizokuwa nazo. Watu wengi ujiona kuwa kuwaita watoto zao kwa majina yanayo tokana na imani zao ni kuonyesha utiifu au ukubalifu fulani wa imani hizo. Japokuwa Hizo dini hususani Uislam hauangalii jina, unaweza kuitwa vyovyote unavyotaka, as long as imani yako hipo hakuna tatizo.

Wakati mwingine huwa nafikiria hawa wakoloni walilazimisha tujiite kwa majina yanayo endana na imani zao ili tuonyeshe utiifu kwao au kututenganisha baina yetu.

Kwangu binasfi sioni tatizo mtu akiitwa Marunyarunya, Mpambalioto, Mwakenge, Ntalimbo, Nyirabu, na majina mengine ya kiasili. La kuzingatia tu kuwa majina hao tutakayo wapa watoto zetu hayataleta hathari mbaya za kutaniwa na kuwakosesha raha wanapokuwa uko nje wakicheza na wenzi wao.
 
Chifu umenena sana tu. Mtu anaona fahari kuitwa jina la kigeni. Mbaya zaidi watu wakishakuwa maarufu ndio kabisa huyazika majina yao ya nyumbani na kuyavaa ya kistaarabu ili kuenda na wakati. so sad. pia suala la kuamini kuwa kumwita mtoto jina la kidini kwa kuamini ni usahihi ni ufanatic huo. kaka yangu aliwahi kukataliwa mwanae kubatizwa kwa jina la Amani. Mapadre husoma falsafa na theolojia ila nadhani kuna kitu cha ziada wanatuficha
 
Back
Top Bottom