Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

Naona kama vile ni mkusanyiko wa wendawazimu vile! hivi inawezekana vipi "Mazungu ya unga" yakapewa hadhi kwa kesi zao kusikilizwa faraghani? Nafikiri kodi zetu tunazowalipa hawa 'waheshimiwa' zinatumika vibaya. Binafsi nadhani ni muhimu tukawa na sheria za kuwalinda mashaidi na waendesha mashtaka badala ya kutengeneza sheria za kuwalinda hawa 'makafiri'
 
Wanaogopa mengi kusiklika kwa kuwa wengi wao wana washirika serikalini na pia ndiyo wadhamini na wachangiaji wazuri wa CCM nyakati za kampeni . Sasa kwa nini wasilindwe ?
 
Kwa mambo yanayo fanyika Dodoma sitashangaa mwishowe wauza madawa na vigogo kesi zao zikawa zinasikilizwa chumbani itakuwa ni kinyume adhima ya Rais ya kutaka kupambana na uovu .
 
Ama Kweli Nchi Hii ina matatizo. Hivi Nyie Wabunge Mliopo Dodoma Mkipitisha Sheria Hii Tanzania Ndio Mwisho Wake. Tumewapa Kura Mjadili Bungeni Mambo Ya Maana Ya Kutuletea Maendeleo Siyo Mambo Ya Wauza Unga na Kuwakingia Kifua.

Mheshimiwa Kikwete, Tafadhali Weka Majina Ya Hawa Wauza Unga Nje. La Sivyo Tutahisi Serikali Yako Ina Jambo Pia. Ndugu Zangu Jambo Hili Linakera Sana. Ulimwengu Mzima Unapiga Vita Ya Madawa Kwa Kuwa Madhara Yake Ni Makubwa. Ndio Maana Nchi Imekuwa Kama Ya Walevi Walevi Tu. Hata Maamuzi Mengi Ya Nchi Yanatia Shaka Uwezo Wetu Wa Kufikiri Na Kuweka Vipaumbele Vyetu.

Mashirika Yanayopiga Vita Dawa Za Kulevya Mko Wapi??? Makanisa Mko Wapi???? Misikiti Mko Wapi??????? Mnakaa Kimya Tu Nchi Inaangamia??????
Mkeshimiwa Kikwete Kama Unaingia Hapa Tafadhali Anaika Majina Ya Wauza Unga Hawa Hadharani Na Kesi Zao Ziwe Wazi.
 
Mwanakijiji:
Wewe na radio yako naomba ufanye follow up juu ya suala hili la Tanzania kuwalinda wauza unga. Naomba pia ripoti zako upeleke kwenye taasisi za kimataifa kuonyesha uozo wa maamuzi yanayotaka kupitishwa.
Naomba pia uwape changamoto taasisi mbalimbali, NGOs, Makanisa na Misikiti kuona hatari ya maamuzi hayo.
Majina yametolewa, hata kama ni tuhuma hawa ni lazima washughulikiwe. Wao wanafurahia maisha wakati watoto na vijana wetu wanaangamia kwa madawa yao.
 
Kama Rais kapewa majina kasema anawapa muda wajirekebishe badala ya kuayakabishi polisi ili uchunguzi ufanyike na watu wakamatwe na ghafla leo mwanasheria anakuja na hoja hii Bungeni that means Rais ana jambo lake and he is only looking for a political cover up . Sasa ndiyo muda wa kuwana wabunge wazalendo na huu muswada .Vinginevyo Serikali itakwua ina act kwa amri ya Rais kuwaficha wakubwa na hata wachangiaji wakubwa wa CCM . Mungu ibarii Tanzania ili tuje kupata Kiongozi Mzalendo mwisho wa siku na utuokea na mabalaa ya vita ambayo nayaona kwa mbele maana wananchi watachoka kudanganywa siku moja .
 
Mheshimiwa Kikwete taja majina ya wauza madawa. Waandishi wa kenya tunaomba mchore picha kuhusu jinsi Tanzania inavyokumbatia uuzaji wa madawa ya kulevya.

Hussein Abdalah:
Hoja yako nzito kuwa hawa wauzaji wa madawa ndio wachangiaji wakuu wa CCM. Maana yake nini? ni chama kinachofadhiliwa na wauza unga? Ndio maana wafanyabiashara wakubwa wamejificha humo. Tanzania ni nchi ya ubabaishaji mwingi na maneno maneno tu. Hamna kitu hapa.
 
hii inaonyesha jinsi gani wanasiasa wanavyopenda sifa

kwani vyombo vya sheria vinafanya kazi gani?

sasa hii inamaana kesi inaweza kuvunjika kwa sababu ya wanasiasa na midomo mirefu
 
Just for the record, leo nimemsikia Mwanasheria Mkuu wa serikali akihojiwa na BBC kuhusu hili suala, na amesema kuwa kipengele cha hizi kesi za wauza unga kusikilizwa faragha wamekiondoa. Zitasikilizwa hadharani. Na amesema kama baadhi mashahidi ndio itabidi wahojiwe faragha .. basi sheria zilizopo zinatosha, zinacho kipengele hicho.
 
Hello Wazalendo,

Sishangai kesho kuona PCB wanakamata wala unga badala ya polisi kuchukua majina ya Wauzaji na wasambazaji toka kwa raisi. Si wamesema raisi kapata majina? Kwa nini wasiwashughulikie? Kwani walivyompelekea raisi/kamanda mkuu hayo majina hawakufanya uchunguzi? Mbona hawa polisi/wapelelezi wanafanya kazi un-professional? Huu ni utani na ubabaishaji kama kawaida kwa serikali yetu. Wanatupotezea muda tu.
 
Let's hope this will be for real...

JK zeroes in on drug barons.Govt forms secret task force to probe drug millionaires

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


THE government has formed a secret task force to investigate and act on all drug syndicate operations in Tanzania, THISDAY can reveal.

This follows a pledge by President Jakaya Kikwete to deal decisively with the influx of drugs and ’dirty money’ into the country.

Sources within the government confirmed that the task force is already operating round the clock in collaboration with several international institutions.

’’The team is a combination of highly credible officers from the police force, the intelligence and Government Chemist Laboratory Agency. They also have full support from International Police (Interpol),’’ sources said.

According to our sources, the team is currently working on the list of top drug dealers and traffickers which some ’Good Samaritans’ presented to President Kikwete mid this year.

The sources add that the team is already investigating links to the list of shame that includes, among them, senior government officials, prominent politicians, top clerics and businessmen magnates.

As well as the suspected dealers, the team is also investigating all possible peddling routes through which the drugs come into the country.

’’The team is backed by detectives who have already interrogated some influential people in Dar es Salaam,’’ the source said in confidence.

President Kikwete has admitted that the use of narcotic drugs should be checked immediately, and has since confirmed that he has started acting on a dossier that contains details on how the drugs syndicate operates in Tanzania.

The President revealed this during a recent meeting with editors early last month, at which he assured Tanzanians that the government would tackle the problem from the grassroots level.

Sources said the government is investigating the alleged drug barons making millions from high-quality imports of cannabis, cocaine and heroin direct from Malawi, Pakistan and Afghanistan before re-exporting the bounty abroad through their syndicated routes.

’’The rapid growth of the market is creating overnight multi-millionaires who invest their newfound wealth in other areas of criminality. Most of them are close or within the political system, they are very strong and some even call themselves ’untouchable’, but this time they are in for it, they are no longer safe, not at all,’’ our police sources confirm.

The Inspector General of Police, Said Mwema, is in the process of reforming the Anti-Narcotic Drugs Unit. He recently appointed a new commander, Senior Superintendent of Police (SSP), Godfrey Nzowa to replace SSP Afwilile Mponi, who has been transferred to police headquarters to be assigned other duties.

SSP Mponi’s tenure was tainted early this year when millions worth of drugs were stolen while under police custody at the anti-drugs unit at Kilwa Road in Dar es Salaam.
 
kwa nini wanasiasa wanaingilia kazi za vyombo vya sheria?

where do these people draw the line?
 
Taratibu tutawajua wote!

’Wabunge vinara wa dawa za kulevya waachie ngazi’
2006-11-08 08:46:52
Na Mwandishi Wetu


Wachungaji 4,020 wa makanisa mbalimbali nchini, wamewataka wabunge wanaojijua ni miongoni mwa wafadhili wa vinara wa biashara ya dawa za kulevya nchini, kuachia ngazi haraka kabla ya majina hayajaanikwa hadharani.

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa maombi maalum ya kumuombea Rais Jakaya Kikwete, kupambana na wimbi la waingizaji na wasambazaji wa dawa za kulevya nchini.

Maombi hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Makanisa ya Kisabato nchini (SDA), Dk.Hery Mhando.

Katika maombi hayo, wachungaji hao walimuombea Rais ulinzi, afya na nguvu ya kupambana na wimbi hilo na kuahidi kumpa ushirikiano katika kufichua wanaojihusisha, wakiwemo wachungaji na maaskofu.

Alisema tayari wenyewe wameanza kufichuana na kwamba wanasiasa, wakiwemo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, nao wajisalimishe haraka kwa Rais.

”Haiwezekani kuwa na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi kujihusisha na wahalifu, wakiachiwa kuendelea taifa zima litakuwa la wahalifu,” alisikika mmoja wa wachungaji hao akisema kwenye maombi hayo.

Walisifu hatua ya mbunge mmoja chipukizi, aliyediriki kusimama ndani ya ukumbi wa bunge na kuahidi kuwafichua watu wanaohusika na biashara hiyo.

”Kama wachungaji wanaweza kufichuana, kwa nini wabunge washindwe?,” alihoji mchungaji mmoja.

Walisema kuwa wameamua kufikia hatua hiyo, baada ya kuona Tanzania inaangamizwa na watu wachache wanaotaka utajiri wa haraka haraka.

Walisema kwa kuanzia wameanza kuwafichua baadhi ya Wachungaji wanaojihusisha katika biashara hiyo na tayari wameanza kukamatwa na kuhojiwa na vyombo vya dola.

Mhubiri Dk. Mhando, hata hivyo, alitaka matajiri watakaokamatwa kuhusika katika biashara hiyo, fedha zao zitumike kuwatibu vijana walioathirika na madawa ya kulevya.

”Wao ndio waliosababisha vijana hawa kuwa katika hali uzezeta kwa kuingiza madawa nchini, utajiri wa fedha walizozipata zichukuliwe na zitumike kutibu walioathirika,” alisema.

Aidha, mmoja wa maaskofu kwenye mkutano huo wa Jangwani, aliahidi kuwataja wahusika kwa Rais Kikwete, kwa kuwanyooshea kidole.

Katika kuhakikisha vita dhidi ya madawa ya kulevya vinafanikiwa nchini, hivi karibuni Rais Kikwete aliwataka wananchi wanaowafahamu watu wanaojihusisha na biashara hiyo kuwafichua kwa kumpelekea orodha ya majina.

Baadhi ya majina yameshapelekwa kwa Rais Kikwete na miongoni mwao wapo viongozi wa dini, ambao hutumia mwavuli wa taasisi zao za kidini kuingiza madawa hayo.

Mmoja kati ya viongozi wa kanisa moja nchini, ambaye jina lake limo kwenye orodha hiyo, tayari wiki iliyopita alikwenda kumwangukia kwa maandishi Askofu Mkuu wa Kanisa moja kubwa nchini na kumuomba radhi kwa kuhusika na biashara hiyo.

Aidha, habari za ndani zinadai kuwa Padre huyo sasa ameamua kufichua majina kwa kumwandikia Rais Kikwete orodha ya watu wanaohusika kwenye biashara hiyo.

Katika orodha hiyo, padre huyo ametaja majina ya kundi hatari kwa usalama wa nchi linaloingiza dawa za kulevya kwa kutumia jina la serikali.

Inaonyesha iliandikwa Novemba 3, na imewataja vigogo kutoka Tanzania Bara na Visiwani, ambao wanatumia jina la serikali kwa kutumia vyeo vyao kufanya biashara hiyo.

Aidha imewataja baadhi ya mabalozi wa Tanzania nchi za nje, wafanyabiashara maarufu nchini, mabosi wa mamlaka zinazotegemewa na serikali kwa uchumi na viongozi wa dini.

Chanzo cha habari kinasema kuwa, waziri mmoja wa Serikali Awamu ya Nne ni miongoni mwa wafadhili wakubwa wa kituo maarufu cha kugawa dawa za kulevya aina ya mandras na heroin, kilichopo Chalinze, mkoa wa Pwani.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa jana, jina la ’kigogo’ huyo limepelekwa Ikulu, baada ya siri kufichuka kuwa nyumba yake inatumika kuhifadhi dawa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Imebainika kuwa kituo hicho cha Chalinze kinafadhiliwa na baadhi ya wabunge, waliotajwa kwenye orodha iliyopelekwa kwa Rais Kikwete.

Katika orodha ya majina iliyopelekwa kwa Rais hivi karibuni ambayo inafanyiwa kazi, imetaja makundi mbalimbali yanayohusika na biashara hiyo.

Kundi la kwanza ni waingizaji wakubwa wa unga, ambalo lina majina ya wafanyabiashara maarufu wenye makampuni makubwa jijini Dar es Salaam na mikoani.

Kundi la pili ni la wafadhili ambao majina yao hutumika kusafirishia dawa za kulevya ambalo lina ’vigogo’ wa serikali, wakiwemo mawaziri, wabunge na wake wa vigogo na kundi la tatu ni la wauzaji wa jijini Dar es Salaam na mikoa ya Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar, Morogoro, Mwanza, Dodoma, Pwani, ambalo lina watu wa uraia wa nchi mbalimbali.

Kundi hili la tatu hutumia majina ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini kufanikisha biashara yao.

SOURCE: Nipashe
 
Amina Chifupa awaruhusu polisi wamkamate mumewe
na Martha Mtangoo

MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Chifupa Mpakanjia (CCM), amelitaka Jeshi la Polisi kumkamata na kumchukulia hatua za kisheria mumewe, Mohamed Mpakanjia, iwapo itathibitika kuwa anafanya biashara ya dawa za kulevya.

Chifupa (26), mmoja wa wabunge ambao katika kipindi cha hivi karibuni, wamekuwa wakizungumzia sana masuala yanayohusu dawa za kulevya, alilitaka jeshi hilo lifanye hivyo pasipo kujali nafasi yake (Amina) ya ubunge.

Akichangia hoja bungeni jana juu ya Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu, mbunge huyo, aliyeingia bungeni kwa tiketi ya Umoja wa Vijana (CCM), alisema: “Mheshimiwa Naibu Spika, hata kama mume wangu akithibitika kuwa anauza dawa za kulevya akamatwe na afunguliwe mashitaka, asiogopwe eti kwa kuwa yeye ni mume wa mbunge.”

Chifupa, ambaye majuzi alisema yuko tayari kushirikiana na polisi katika kuhakikisha kuwa anapambana na dawa za kulevya hapa nchini, alilieleza Bunge jana kuwa, katika kuonyesha nia yake ya kuwataja watuhumiwa wa dawa hizo, aliamua kwenda kituo cha polisi na kutoa taarifa hiyo.

Lakini baadaye alipewa taarifa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha juu ya watuhumiwa hao wa dawa za kulevya.

“Nilikwenda kituo cha polisi na kutoa taarifa juu ya wauzaji wa dawa za kulevya, baadaye nikapewa taarifa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwakamata watuhumiwa hao.

“Nyumba si hospitali wala si nyumba ya kulala wageni…kwa siku wanaingia na kutoka watu 200 hadi 500, bado unatafuta ushahidi wa mtu kuuza dawa za kulevya, ushahidi gani huo unaotafutwa?” alihoji mbunge huyo.

Pia mbunge huyo, aliitaka serikali kuongeza kiwango cha adhabu ya sh milioni moja hadi kifungo cha maisha kwa mtu atakayepatikana na hatia ya kuhusika na dawa hizo za kulevya.

“Mtu anauza dawa hizo, anapata fedha nyingi zaidi ya mabilioni, halafu anaambiwa alipe faini ya sh milioni moja, hii adhabu haimfai… anatakiwa afungwe kifungo cha maisha na si kulipa faini hiyo,” alisisitiza Chifupa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jioni, Chifupa alisema amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na kuwapo kwa maneno yanayomhusisha mumewe na biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya, jambo alilodai kuwa halina ukweli wowote.

“Unajua kumekuwa na maneno kwamba Medi (Mohammed) anafanya biashara hiyo ya unga wakati si kweli, na ndiyo maana nikalazimika kusema maneno hayo,” alisema Chifupa.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Komu (CHADEMA), aliitaka serikali iwadhibiti wawekezaji kwa kuwa wamekuwa wakichukua madini na wanyama na kupeleka nje, na kuwaacha Watanzania, walio wamiliki halali wakiwa hoi.

“Serikali iwaangalie sana hawa wawekezaji, wanakuja wanatula migongo, wanatuacha hivi hivi,” alisema.

Awali, msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Halima Mdee (CHADEMA), akisoma maoni ya upinzani juu ya muswada huo, alisema ili kufanikisha kudhibiti vitu haramu, ni vema serikali ikajiuliza kama ina nia ya dhati na utashi wa kisiasa, wa kuhakikisha kwamba sheria hiyo inafanya kazi na si kama sheria nyingine zinazopitishwa kutokana na jumuiya ya kimataifa kufanya hivyo, na kisha kuziacha zikiozea kabatini.

“Ukiyaangalia kwa umakini mazingira husika yanatugusa baadhi yetu, kama si wote katika maisha yetu ya kila siku, ndiyo maana narudia kusema kwamba, kwa muswada huu kutekelezwa kunahitajika nia ya dhati na utashi wa kisiasa na kuutekeleza,” alisema.

Mdee alisema fedha haramu na rushwa vitapungua ama kwisha kabisa, pale mazoea yatakapobadilishwa katika utendaji wa kazi na kuweka mbele maslahi ya Watanzania, badala ya maslahi ya mtu binafsi au kundi fulani katika jamii.

Aliishauri serikali kuwa na utaratibu utakaokiwezesha chombo hicho kuwa na uhusiano wa kazi na vyombo vingine, vinavyofanya kazi zinazoendana na chombo hicho, ikiwamo Taasisi ya Kuzuia Rushwa na vyombo vingine vya aina hiyo.
 
Majina yanaota kutu ofisini kwa JK, huku watu wakiumia. Naye Mheshimiwa sana AC anaomba mumewe akamatwe. Kesho tutasikia kingine na kingine na kingine. "Who will close this loop' ?
 
Sawa sawa...
1.[B]Jinsi ya kuwakamata[/B]..
Inabidi Uanzishwe Mfumo Mwingine wa Jeshi la polisi

Wa- tofauti kabisa na -Wa -usalama wa raia(taifa)
Ambao Mara zote Itawashika watuhumiwa-kwa vigezo vya ushaidi...

Mimi Hata sijui vizuri Mifumo yetu ikoje...?
Itakua kazi sana Kuwakamata...Na kutokomeza Huu ulevi..

Nahisi hata humu kuna wavuta Bangi
 
Jamani haya si maoni yangu lakini katika pita pita yangu nimeikuta kule kwenye forum ya Mengi(Dar hotwire) hii habari kwangu ni mpya lakini nadhani huku kutakuwa na mitazamo tofauti....


mwanzilishi wa topic hii huko anajiita SUPER TALL


MAMA REKWATARE ETI LEADER WA KUUZA "UNGA"
« on: Nov 13th, 2006, 6:20pm »
--------------------------------------------------------------------------------
Jamani nimesikia tetesi eti yule mchungaji mama Rekwatare pia yeye yupo katika top 10 ya kuuza madawa ya kulevya ......i mean " UNGA".......ama jamani mama wa watu anazingiziwaaa?
Ama bongo ukishakuwa na hela hela basi utazushiwa hili na lile....ama kuna ukweli ndani yakeee......maana watu wengi hujivalisha ngozi ya kondoo kumbe nje ni...........mhhhhh naombeni jibu tafadhalini.



Kisha kajibuwa na KILLUMINATI....Reply #4 on: Dec 1st, 2006, 6:08pm

Ni kweli hata KAKOBE naye nimesikia yumo....na zile trip zake anazokwenda KUHUBIRI nje ndo hapo hapo anapopata upenyO wa kufanya mambo yake.....sasa sijui Kikwete ataanza wapi ataishia wapi....maana kama namuona hapa amebaki mdomo wazi na madenda yanamtoka kwa mshangao.




SOURCE:http://196.41.49.109/cgi-bin/forum/YaBB.cgi?board=np;action=display;num=1163431212

Naona watu washachoka kusubiri listi ya "SIRI" aliyonayo JK
 
Data nzito hizo mzee, naona tuendelee na issue maana wenye majina wapo! Hao hawamo kwenye majina bro kumi bro, ninarudia tena ukiyataka niombe kwa ustaarabu nitakupa kwenye PM, FULL STOP!
 
Mzee ES,

Nimejaribu kukutumia PM na huu ndo ujumbe nilokutana nao baada ya meseji yangu kugoma The following errors occurred when this message was submitted:

1. Mzee Es has exceeded their stored private messages quota and can not accept further messages until they clear some space


Nilikuwa na ombi binafsi.
 
Back
Top Bottom