Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
Wakiwataja CCM haitapona, hizo ni ndoto tu. Labda CCM itoke madarakani ndio watatajwa:whistle:
Mtz umenena JK anayo majina hayo siku nyingi toka kipindi cha marehemu Amina Chifupa,tatizo la jk ni lielile siku zote nikutojiamini,wala rushwa wakubwa hivyo hivyo hana uwezo nao,ndio wafadhiri wakubwa wa ccm.
Kwani hatuwezi kuwataja humu?
Tuwataje basi!!
Thank u so much, but we need names pse:confused2:
lininames labda kikisha kipindi alichowapa wajirekebishe wasipojirekebisha atawataja
Majina ya vigogo ninayo-JK
03 Oct 2006
By Mwandishi Wetu
Rais Jakaya Kikwete, amekiri kupokea majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kwamba majina hayo yanafanyiwa kazi na watendaji wake.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na taifa kupitia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Alikuwa akijibu swali kutoka mmoja wa wahariri aliyetaka kujua iwapo amepokea waraka wenye majina ya vigogo wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Bila kufafanua, Rais Kikwete alijibu, waraka nimeupata na nimewapa wahusika na wanaufanyia kazi. Inadaiwa kwamba, katika waraka huo ulioandikwa na kikundi kimoja cha wananchi, kimetaja majina ya vigogo zaidi ya 100 wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ama kuingiza nchini dawa za kulevya au kuwa mawakala wa dawa hizo au wauzaji.
Kwa mujibu wa waraka huo, baadhi ya wafanyabiashara waliotajwa ni wa kutoka mikoa ya Tanga, Mbeya, Dodoma, Kigoma, Arusha, Iringa, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar wamedaiwa kuhusika na biashara hiyo.
Aidha, katika waraka huo, umetaja baadhi ya hoteli Jijini Dar es Salaam, kutumiwa kama vituo maalum vya kukutanisha wafanyabiashara wa dawa hizo, kwa ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Kazi ya kuandaa taarifa hiyo yenye kurasa 12, ilifanywa na Shirika moja linalopigania haki na Usawa na Mazingira katika Jamii la Jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa kwamba, taarifa hiyo ya siri, ilikabidhiwa kwa Rais Kikwete kupitia kwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bw. Bakari Mwapachu.
Katika taarifa hiyo, yamo baadhi ya majina ya wabunge, wafanyabiashara maarufu, maofisa wa idara nyeti za serikali kama vile Mamlaka ya Mapato Nchini, Benki Kuu (BoT) na maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi, pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini.
Viwanja vilivyotajwa kwenye waraka huo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro (KIA), Zanzibar (Karume Aiport), Tanga, Arusha na Mbeya.
Mbali na viwanja vya ndege, waraka huo umetaja wafanyabiashara hao kuzitumia Bandari za Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar na fukwe za Bagamoyo kuingiza shehena kubwa za dawa hizo.
Taarifa hiyo pia imetaja majina na namba za magari ya watu yanayotumika kusafirisha dawa hizo na kusambaza kwa walengwa jijini Dar es Salaam.
Pia majina ya kampuni za ndege zinazotumiwa na watuhumiwa hao kuingiza dawa, huku wengine wakitumia mikataba ya usafirishaji wa vifaa vya hospitali pamoja na matairi ya magari.
* SOURCE: Nipashe
Tangu majina hayo yawasilishwe 2006 what has happened?
Tangu majina hayo yawasilishwe 2006 what has happened?