Majina ya watoto

nadhani ile dhana ya ndoa ni ndoa ya koo mbili inabadilika kwa kasi sana. Kwahiyo, majina ni viashiria tu vya mabadiliko hayo na jitihada za kulinda mfumo na wengine wakipata uhuru wao!
 
haaaha halifai kumuita mtoto. Loh......

Mie sijali aitwe jina la kiswahili au kizungu, najali maana ya jina.

Kuna majina mengine ya kikabila hayana maana kama mengi ya Kizungu yalivyokuwa hayana

Sasa hapo vipi?

Heri sisi tuloitwa Tunu, Asante, Kweli, Nadra, Subira, Akili, Amani
 
Kuna majina mengine ya kikabila hayana maana kama mengi ya Kizungu yalivyokuwa hayana

Sasa hapo vipi?

Heri sisi tuloitwa Tunu, Asante, Kweli, Nadra, Subira, Akili, Amani

umesahau na haya Kabasa,rugalabamu,shedafa,mkono,kamundu,didi,mwajuma,mwanne,mwanaidi,mzee,kijakazi nk
 
Hili la kuchaguliwa majina katika namna ya kupoteza haki yetu ya "veto" tulilikataa ....tulichofanya tulikuwa tunaandaa majina mawili au matatu ambayo hata sisi wenyewe tupo confortable na then kuwashirikisha wazazi na watu wengine wanao matter kwetu. Hata hivyo kwa vyovyote vile uamuzi wa mwisho kuhusu jina mara zote ulikuwa kwetu.

Mara nyingi nyinyi wenyewe ndani ya ndoa yenu mkiwa hamna msimamo wa pamoja ni rahisi sana kwa watu wengine 'kuleta pua zao' kwenye maamuzi bila hata kualikwa!
 
Hivi ni kwa nini mtu na akili zako uchaguliwe jina la mtoto wako ambaye ni damu yako? je ukichaguliwa mke/ mume napo utakubali!!??
Mtoto anapozaliwa kunakuwa na tangazo la kizazi chukuwa tangazo la kizazi peleka RITA kwenye ofisi ya vizazi na vifo muandike mwanao jina unalolichaguwa wewe na hilo ndio litabaki kuwa jina lake official in any Documents, kama wazazi wako watampachika jina lao hilo halina ubaya na ni hiyari yako kama utataka kuri endorse baadaye pale kwenye Given Names.

Binafsi nimezimudu vyema perssure za kifamilia kutaka kupangia watu maisha, everybody knows me in my family, ujinga ujinga na ukale hauna nafasi kwangu.
Mtu mwingine anaoa kwa Pressure za wazazi eti wasije kufa kabla hawajashuhudia ndoa yake!! huu ni zaidi ya wehu.
 
haaaha halifai kumuita mtoto. Loh......

Mie sijali aitwe jina la kiswahili au kizungu, najali maana ya jina.
Jina lina maana gani!? muite mwanao Tajili basi tuone kama atakuwa tajili kweli. we need the names taste good that's it!
 
Kuna majina mengine ya kikabila hayana maana kama mengi ya Kizungu yalivyokuwa hayana

Sasa hapo vipi?

Heri sisi tuloitwa Tunu, Asante, Kweli, Nadra, Subira, Akili, Amani

ni kweli kabisa...
Nadhani ni vyema kwanza kujua maana ya jina unalotaka kumpa mtoto, liwe la kilugha au kizungu..

Jina ambalo wewe mzazi unalipenda, na ukimpa mtoto jina zuri hata yeye atalipenda....

S kumpa jina kwa sababu tu la babu, au bibi kachagua, au ndo jina oa nani sijui kwenye ukoo. Au kumpa jina mtoto kwasababu tu ni jinala mwanaamuziki maarufu hata kama halina maana..... Au jina la mzungu wa zamani
 
Jina langu halisi ni la shangazi yangu, kiukweli naenjoy sana kwani napewa heshima ktk familia kama Dada wa baba zangu na hata kushirikishwa maamuzi ya familia ila hili lipo ktk kabila letu sijajua kwa makabila mengine
 
unatakiwa kuwa makini na majina, kuna ushahidi wa maandiko matakatifu (Biblia) watu wanaradhana na majina yao, hivyo kama hilo jina lina maana nzuri unaweza kulichua vinginevyo wenye ndoa mna maamuzi ya majina ya watoto wenu, uzoefu wangu, mimi nina watoto watatu na wote tumewapa majina bila kubase kwa upande wa kwetu au wa mke
 
Mimi kwa kweli hii kitu inaniudhi sana haya huyo anaedai jina lake lipewe kipaumbele mlevi ,mwizi mtoto akichukua jina ni pamoja na tabia
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom